Mahakama kuu yatupilia mbali ombi la kusimamisha mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa TFF

Mahakama kuu yatupilia mbali ombi la kusimamisha mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa TFF

Mbona hata wazazi wake wote wamezaliwa humu.tupe ushahidi km Karia ni muhamiji.
Wamezaliwa humu wapi!! By the way, Karia ni kabila gani? Ukiniuliza mimi nitakuambia mimi ni Msambaa wa Tanga! Jamali Malinzi alikuwa ni Mhaya wa Kagera! Je Wallace Karia ni Mdigo wa Tanga siyo!!
 
Unataka atoke Bukoba?

Si ndiye Malinzi huyu huyu aliwahi kushika nafasi hapo TFF na madudu yake hata hayasemeki?
Mimi nataka TFF iongozwe na wenye mpira wao. Na siyo hawa wanasiasa wapigaji, kwa mgongo wa kuwa na elimu ya shahada ya chuo kikuu.
 
kwahiyo yule rais na makam wake waliokuwa wanatafutwa na utopolo kuchukua nafasi baada ya UCHAGUZI KUFUTWA wanaenda wap
 
Hili NILILITEGEMEA.....

Nikijaribu kuingia katika mawazo ya ndugu Ally Salehe ninamaiza ya kwamba alitaka tu KUUFUFUA MJADALA WA MABADILIKO YA KATIBA YA TFF baada ya UCHAGUZI KUPITA.....

Ndg.Ally Salehe apongezwe kwa KUMFUNGA PAKE KENGELE.....

KWA MTAZAMO WANGU ,ndg.Ally Salehe AMESHINDA.....

#MabadilikoYatakujaTFF
#UchaguziUjaoBaadaYaKariaKumalizaUtakuwaBoraZaidi

#KaziIendelee
 
Wamezaliwa humu wapi!! By the way, Karia ni kabila gani? Ukiniuliza mimi nitakuambia mimi ni Msambaa wa Tanga! Jamali Malinzi alikuwa ni Mhaya wa Kagera! Je Wallace Karia ni Mdigo wa Tanga siyo!!
Kwa hiyo uwo ndio ushaidi nimesema nipeni ushaidi kama Karia nimuhamiaji.unaniletea habar ya kuwa wewe ni Msambaa .msimuhukumu mtu kisa hamumpendi tu.leo Obama ametawala ilihali mzazi mmoja hakuzaliwa kule.bado mpo kwenye ujima.
 
Kwani ni uongo siyo Msomali? Sasa inakuwaje mtu atoke zake Somalia huko, halafu aje awawekee vikwazo vya kipuuzi Wazawa na wachezaji walio lipambania hili Taifa katika medani za mpira wa miguu, kuliongoza Shirikisho lao?
Siyo yeye aliyeweka hizo kanuni,wadau wa mpira walitakiwa wazikatae siku nyingi kabla ya kipindi cha uchaguzi.
 
Mahakama Kuu Jiji Dar es salaam leo Julai 2, 2021 imetupilia mbali ombi la kusimamisha mchakato wa uchaguzi mkuu wa viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) uliopangwa kufanyika Agosti 7, 2021 Jiji la Tanga

Jaji Edwin Kakolaki alifikia uamuzi huo baada ya kukataa ombi la "matengenezo ya hali ya sasa (Maintenance of status Quo)" ambayo iliwasilishwa na mawakili wa mwombaji Ally Saleh ambaye alikuwa mmoja wa wagombea nafasi ya Urais katika Shirikisho hilo.
Kiongozi, kilichokataliwa ni ule udharula wa kesi yenyewe. Itaendelea tarehe 9 June. Maana uchaguzi bado uko mbali kuna muda wa kutosha kuamua kesi kabla ya tarehe ya uchaguzi.
Umeiweka kama vile kesi inetupws kabisa. Sio sawa!
 
... Halina historia yoyote ile ya kucheza mpira hapa nchini,
Kama mtu anacheza mpira halafu hasomi, basi akistaafu soka asitegemee historia yake ya kucheza kuupata uongozi. Uongozi unahitaji usomi, sio bla bla za historia
 
Hizo hoja zilikuwa dhaifu mno, Ally Saleh alikuwa anapoteza muda bure

Alichofanya Karia ni kuwapelekea mahakama Katiba ya TFF tu.

Yaani Karia anaupiga mwingi sana, wapinzani wa Karia wamepigwa nje ndani.
Wamepigwa mbele nyuma....
 
Kama mtu anacheza mpira halafu hasomi, basi akistaafu soka asitegemee historia yake ya kucheza kuupata uongozi. Uongozi unahitaji usomi, sio bla bla za historia
Wewe ni mmoja wa wale wanao amini katika vyeti kama kigezo cha usomi, jambo ambalo siyo sahihi hata kidogo. Tunahitaji TFF iongozwe na wachezaji wenyewe wa mpira wa miguu kama ilivyokua kwa Leodgar Tenga!

Na siyo hawa wanasiasa wapigaji. Wengine hata walikotokea, hatujui! Huku wahusika wakuu wakitengwa kwa vigezo mfu vya vyeti.
 
Acha ushamba sio kila mchezeji lazima aje kuongoza mpira. Pele, Maradona na wengine wengi hawajawahi kuwa viongozi wa mashirikisho yao. Leta Hoja acha uzazwa
 
Acha ushamba sio kila mchezeji lazima aje kuongoza mpira. Pele, Maradona na wengine wengi hawajawahi kuwa viongozi wa mashirikisho yao. Leta Hoja acha uzazwa
Wewe ndiyo kiazi kweli. Nani aliyesema kila mchezaji ni lazima aje kuongoza mpira?

Wenye akili ndogo wote hamuwezi kuelewa nilichomaanisha. Hivyo ni bora mkaficha upumbavu wenu.
 
Wewe ni mmoja wa wale wanao amini katika vyeti kama kigezo cha usomi, jambo ambalo siyo sahihi hata kidogo. Tunahitaji TFF iongozwe na wachezaji wenyewe wa mpira wa miguu kama ilivyokua kwa Leodgar Tenga!
Hoja kama hizi hutolewa na watu wasioenda shule
 
Kuna Mambo watanzania huwa wananiacha hoi sana. Kanuni za uchaguzi zipo wazi muda wote watu wamekaa kimya lakini uchaguzi ushakarbia ndio watu wanakurupuka tu na kuanza kupiga kelele ooh kanuni zinambeba mtu mmoja. Tulikua na muda mrefu sana wakulalamikia hizo kanuni mbovu ili muda wa marekebisho angalao upatikane. Sasa subiri uchaguzi upite utaona watu kimyaa mpk uchaguzi mwingine ndio watalalamikia Jambo lilelile.
 
Kwani ni uongo siyo Msomali? Sasa inakuwaje mtu atoke zake Somalia huko, halafu aje awawekee vikwazo vya kipuuzi Wazawa na wachezaji walio lipambania hili Taifa katika medani za mpira wa miguu, kuliongoza Shirikisho lao?
Ndio maana nakuita MBAGUZI! Unapomuita Msomali wakati ana uraia wa Tanzania na wewe unajinasibu MZaWA una tofauti gani na Kaburu wa Afrika ya Kusini??!?
 
Ndio maana nakuita MBAGUZI! Unapomuita Msomali wakati ana uraia wa Tanzania na wewe unajinasibu MZaWA una tofauti gani na Kaburu wa Afrika ya Kusini??!?
Watanzania tunatambulika pia kwa makabila yetu! Na hilo liko wazi tu. Sasa uniambiee basi huyo Karia ni Kabila gani?

Na huo ubaguzi nimeuanza mimi, au ameuanza yeye mwenyewe kwa kujitengenezea mazingira ya kujimilikisha Shirikisho, huku akiwabagua Watanzania Wazawa na wenye sifa za kuwa viongozi wa TFF?
 
Back
Top Bottom