Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Leo imetoka taarifa juu ya Mahakama Kuu kubatilisha hukumu iliyotolewa dhidi ya mtu aliyekutwa na hatia ya kufanya vitendo vya uchawi dhidi ya mtoto wa ndugu yake huko Njombe!
Hukumu hii ilitolewa kipindi ambacho vitendo vya uchawi na ushirikina vikiwa vimeshika hatamu kwa kiwango cha kusikitisha hapa Tanzania, hadi jamii ikawa imekosa mahali pa kwenda ili kupata suluhu na tumaini.
Vitendo vya uchawi na ushirikina si tu vimekuwa vikirudisha maendeleo ya jamii zetu nyuma bali vimekuwa vikiongeza mzigo mkubwa sana kwa serikali kwa kuongezeka jamii tegemezi kila kikucha. Vitendo hivi vimeangamiza watu tegemezi kwenye familia mbalimbali na kusababisha umasikini kuzidi kukithiri kwenye jamii nyingi Afrika na hasa Tanzania.
Waliotunga sheria ya kupiga marufuku vitendo vya uchawi hawakuwa wajinga. Kuna kitu waliona na walitaka kizuiwe na sheria ili jamii ipate kukombolewa na kuokolewa. Na mara nyingi nimekuwa nafikiri kuwa Mahakama zetu zinapotafrisi sheria hazina budi kwenda kuangalia sera iliyosabisha sheria husika kutungwa na pia asili hasa ya sheria hiyo ni nini na ilitungwa ili kukabili changamoto zipi kwenye jamii.
Nimesikitishwa sana na uamuzi ulitolewa na Mahakama kuu Iringa na kusema kweli, uamuzi huu sio tu utachochea kuongezeka kwa hizi imani za kijinga hapa Tanzania bali utachochea pia kurudi nyuma kwa jamii za kitanzania ambapo watu wataona sasa kuwa hakuna haja ya kuacha vitendo hivi vya ajabu kwa sababu sheria pia inawafumbia macho.
Hukumu hii pia sio tu itasababisha kuendelea kwa vitendo hivi bali itachochea sana kuongezeka kwa visasi hasa mauaji maana wahanga wataona hakuna tena msaada wanaopata kwenye vyombo vya kisheria.
Nahitimisha kwa kusema Mahakama ijitathimini kwa hukumu zake inazotoa!