JAYJAY
JF-Expert Member
- Oct 31, 2008
- 9,120
- 9,727
Tangu kuanzishwa operesheni za usafi ambazo zimegeuzwa kuwa za kukimbizana na Machinga hiyo mahakama ndio imegeuzwa machinjioni.
Watu wanakamatwa na kupelekwa hapo mara utasikia wanataka laki 5, mara laki 4 yaani haijulikani faini halali ni ipi! Ni ujanja ujanja wa kitapeli tu ndio unaoendelea hapo.
Inashangaza dada anayetembeza deli la maandazi na chai kuambiwa alete laki tatu. Mwingine kakamatwa kwa kutupa sigara chini anadaiwa naye alete Laki Tatu.
Mimi naomba kushauri "ziwekwe taarifa rasmi za adhabu na faini kwa makosa mbalimbali" maana huo ndio mwanya wanaoutumia hao maofisa hapo mahakamani kuwapiga raia. Bahati mbaya zaidi hata risiti zenyewe hazieleweki au unakuta zina majina tofauti na mkosaji kuonesha kuwa ni za magumashi.