Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR UPO KIHALALI
Mahakama ya Jumuiya Afrika Mashariki imetupilia mbali madai ya kupinga uhalali wa Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yaliyofunguliwa na baadhi ya wanaharakati.
Mapema leo Wakili Mkuu wa Serikali Gabriel Malata ameeleza kuwa mahakama hiyo imetoa uamuzi huo baada ya kukubaliana na hoja zote za upande wa serikali ikiwa ni pamoja na madai kuletwa nje ya muda, pamoja na uhalali wa mahakama kuhoji uhalali wa muungano huo.
Amesema Mahakama ya Afrika Mashariki imezaliwa kupitia makubaliano (The East African Community Treaty) ya mwaka 1999 na kuanza kufanya kazi mwaka 200, hivyo mahakama hiyo haina mamlaka ya kuhoji Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wa mwaka 1964.
Jana kulitolewa maamuzi ktk Mahakama ya Afrika Mashariki, wananchi wapatao 40,000 wa Zanzibar walifungua kesi dhidi ya Serikali ya Zanzibar, katibu Mkuu Kiongozi SMZ, Mwanasheria Mkuu wa Tanzania kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar." Gabriel Malata
Madai yaliyoletwa kuhoji uhalali wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yako nje ya muda, kwa mujibu wa kanuni malalamiko yanatakiwa kuwasilishwa ndani ya siku 60 tangu tukio lilipotokea, sasa kuanzia Aprili 26, 1964 mpaka leo ni miaka 56."-Gabriel Malata
Mahakama ya Afrika Mashariki imesema haina mamlaka ya kuhoji uhalali wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa sababu aliyetakiwa kuhojiwa ni Serikali zote mbili zilizoungana wala si kuhoji Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania." - Gabriel Malata
Upande wa Serikali zote mbili (Bara na Zanzibar) ulipeleka hoja kuthibitisha Muungano huo na mapingamizi ya awali (preliminary objections) kuhusu Mamlaka ya Mahakama (ya Afrika Mashariki) kusikiliza shauri hilo." - Gabriel Malata
Shauri hilo lilidai kama hakuna hati ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, hata Taifa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania halipo sababu hakuna Muungano, hata kutiwa saini kwa Muungano huo ni batili sababu hakuna ridhaa ya watu wa sehemu hizo mbili." - Gabriel Malata
Shauri hilo lilikuwa linahoji; hati ya makubaliano ya Muungano kati ya Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar siyo halali na haipo. Msingi wa hoja hizo wanadai Zerikali ya Zanzibar haijawahi kuridhia hiyo hati ya Muungano." - Gabriel Malata