Mahakama ya kadhi ndani ya Katiba - Tanzania

Mahakama ya kadhi sio huduma ya jamii ni huduma ya waisilamu. Huduma ya jamii haichagui Dini unless hujui maana ya jamii. Kwa kiingereza wanasema "public service". Public ya tanzania ina wakristo, waisilamu, wapagani, na wengine wengi wenye Imani zao. Sasa kadhi inawahusu hawa wote? Hii kadhi haiwezi kupeewa ruzuku kwa pesa za umma.
 
Vipi wapaganh? Je katiba itakuwa imevunjwa kwa serikali kuhudumia mambo ya dini?
 
Kwa hiyo waislam wasitibiwe kwenye hospitalier za wakristu..?? Maana wakristu hutawaona kwenye hizo mahakama. Na shule je..?
 
mimi sijajuwa tatizo hapa ni mahakama ya kadhi AU RUZUKU YA mahakama ya kadhi ebu wana thread mniweke sawa.
 
Tatizo hapa waislamu wanachotaka hasa ni MKWANJA aka RUZUKU maana toka ngazi ya kata mpaka taifa mahakama hizo zitaajiri hivyo kuwapatia waislamu wengi ajira maana hawawezi kuajiri MAKAFIRI kwenye mahakama zao.
mimi sijajuwa tatizo hapa ni mahakama ya kadhi AU RUZUKU YA mahakama ya kadhi ebu wana thread mniweke sawa.
 

Maaskofu
Wahamasishe waumini sasa waimini wao wakitose chama cha mapinduzi kutokana na udhaifu walionao.
CCM ni opportunist watatusababishia uvunjwaji wa amani kwani chama kimechoka.
 
Umesema kweli. Lakini pia matatizo yanayotokana na dini kupewa nguvu za kisiasa na kusimama kwenye sheria za nchi yanapotokea, yanawakumba watu wote hata waislam wenyewe. Hii unaweza kuithibitisha kwa wimbi la wakimbizi wanaokaribishwa nchi za Ulaya na Canada wakikimbia machafuko huko kwao, ingawa tena wanaanza kuhamisha vyanzo vya matatitzo hayo kuvipeleka kule wanakaribishwa.

Pamoja na Maaskofu, ni vizuri wapenda amani wote wa nchi hii wakiwemo dini zingine zote kwa kuwa nchi hii inadini nyingi, waislam wenye uelewa, makabila na kila kundi, kuikataa hii serikali ya ccm ambayo inalilia kusababisha dhahama katika nchi kwa kukosa dira wala kibali kwa wananchi.

Ccm ikataliwe kwa nguvu zote.


Maaskofu
Wahamasishe waumini sasa waimini wao wakitose chama cha mapinduzi kutokana na udhaifu walionao.
CCM ni opportunist watatusababishia uvunjwaji wa amani kwani chama kimechoka.
 

Umesema kweli mkuu
Jambo linalonipa shida ni njinsi viongozi wetu wanavyo shindwa kutoa maamuzi katika mambo ya siyo hitaji kumungunya midomo.
1.Katiba iliyopo iko wazi kuhusu maswala ya nchi na dini. Nchi yetu haina dini japokuwa wananchi wake wanaimani zao.
Hivyo basi maswala ya dini yafanyie kwenye dini na taasisi husika.
2. Katiba ni ya nchi, na nchi hiyo haina dini sasa swala la udini ndani ya katiba linaingiaje.
3. Mahakama ya kadhi itashughulikia nini na manufaa yepi kwa nchi kama siyo kikundi fulani.
Kwanini kikundi hicho na vingine vinavyokuja visifanye shughuli zao kwenye taasisi zao bila kubebesha mizigo jamii.
4. Kwa sababu ya udhaifu wa viongozi wetu wamefikisha nchi mahala wanaamua vitu kwa uoga, k.m wamegawa mali za umma kwa waislamu kwa lengo la kujipendekeza kwao jambo ambalo sasa limewafanya waislamu kujiona kuwa wana haki ya kufanya lolote.
Ninaimani kama kawaida ya wakristo kutotaka mabishano yasiyo kuwa na tija la sivyo nawe utaonekana uko kama unaye lumbana naye wataendelea kuelimisha umma na kukosoa serkali kwa njia ya ustaarabu kama ilivyo desturi yao.
 
hawa maccm wanataka kuleta mauaji n akuleta vita tanzania naona wamechoka kukaa kwa utulivu tuliona
sijui wana nini akatika mavichwa yao wewe mahakama ya kadhi si mambo ya dini yale na uliona wapi serikali
ikawa ana dini au wenzetu waslam ni watawala wameunganika na ccm nini?
 
Nasema hivi bila kuingia kwenye civil war hatutoheshimiana kwa kuwa kila upande unajiona upo juu zaidi ya mwingine.
 
Unapo jenga hoja simama pandemic zote na ujipime kama hoja unayojadili inamaslahi gani mapana kwa nchi yako.Ni vyema ukajiuliza ni kwaajili ya nani ? Kwa faida ya nani? Na gharama zitakuwa za nani? Tunapoiangalia mahakama tafsiri yake ni taasisi inayoshughulika na kutafsiri sheria na kutoa maamuzi ya khaki kwa jamii iliyokubaliana kwa mujibu wa sheria mama kwa maana ya Katiba. Hivyo kila mahakama inapaswa kuundwa na jamii husika kwa maslahi ya jamii hiyo kwa kufuata kanuni na mashari ya jamii husika bila kuadhiri jamii nyingine zenye malengo na pengine itikadi tofauti. Katika kuendesha taasisi kama hizi kunahitajika gharama hivyo gharama ya taasisi hiyo iendeshwe kwa gharama za wenye taasisi hiyo bila kuingiliwa kwa namna iwayo yote na kindi lingine ambalo pengine hata hawajui na kufahamu kwa kina miiko ya taasisi anzishwa. Faida yake ni tasisi hiyo kuondoa kupangiwa au kulazimishwa kutoa maamuzi kwa kisingizio cha kuchangiwa fedha.
 
Binafsi napinga kwa nguvu zote iyo mahakama ya kadhi...Leo hii waislamu waje na yao ya kadhi, wakristo nao waje na yao, wahindu nao, wale wa dini za asili nao ..
sasa mahakama za hii nchi zitakuwa zinafanya nini??
Hii ndio mianya ya kuvuruga amani nchi hii
..
No to Mahakama za Kidini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…