Mahakama ya kadhi ndani ya Katiba - Tanzania

Mahakama ya kadhi ndani ya Katiba - Tanzania

Hatuwezi kuruhusu kila kikundi cha dini kiwe na mahakama yao! Hii itakuwa ni vurugu!
Mwisho wapagani watataka mahakama yao, wakristo ya kwao hadi walevi watataka mahakama yao.
Hakuna mjadala, no mahakama ya kadhi hapa tz.
Cc@Faizafoxy

Hahaha...hawa jamaa wanaogopa kweli wakiskia mahakama ya kadhi...utadhani wameskia AL QAEDA...au AL SHABAAB.
 
Badala ya kukazana kujenga shuke nzuri, referal hospitals, and the like mnakazana na kadhi! Nauliza Kadhi ni hospital? kadhi ni shule ? kadhi ni university? Kadhi ni barabara ya lami? Kadhi ni mgodi wa madini?

Hao jamaa hawapendi kusoma wewe c unaona mishule yao inavyofanya vibaya au hulijui hilo.Haitaki kabisa elimu na wengi wao hawajasoma sasa unaposema kuhusu shule hauwezi eleweka kiurahisi.
 
katiba bila kadhi aipiti ng'o

Kwani isipopita unamtishia nani? Kwani hii katiba inayotumika sasa ina mahakama ya kadhi? Wanasiasa wameshasoma akili zenu fupi... kwa taarifa yako katiba itapita, uchaguzi utapita na mtabaki na ngonjera zenu za ajabu ajabu. Time will tell.
 
Waislam wala hatuna papara, sisi tartiiiiibu tu mpaka kieleweke.

Leo mnaweza kulijadili la mahakama ya kadhi, hiyo ni hatua kubwa sana kwetu.
 
Mjomba wewe kiboko unataka mahakama za kimila.sasa mila za kabila gani?maana nina wasiwasi kila jengo litakuwa na kamahakama.
 
samahanini wakuu naomba mnijuzu maana hadi leo sjapata kuelewa kwamba
"mahakama ya jamhuri ya muungano wa tz inakoseaga wapi mpaka ikapelekea watu waone wanahitaji mahakama ya kadhi?"

Sijui kwa kweli inapokoseaga. Maana sheria za Jamhuri ya Tanzania zinaruhusu kuachana kwa kupeana talaka lakini nashangaa eti kuna dini zingine zinakataza kuachana!!!! Sijui nani anampinga nani.....? Serikali ya Tanzanzaia (mahakama) inapotoaga talaka mahakamani huwa inapinga dini ama dini inapokataza kuachana kwa talaka (muishi mpaka kifo kiwatenganishe hata kama mmeudhiana) ndo huwa inaipinga serikali ya Tanzania?
Maswali kama haya yakijibiwa tutajua mahakama ya kadhi ina kazi ama haina kazi.........
 
tutaipata ni haki yetu .imetajwa ndani ya kitabu.wengine hawana.watatungaje?.mungu yupo tutapata tu? maadam imeshushwa itakuwepo .hao wanaoona ni kitu cha mzaa watashangaa iko siku.
 
Hatimae wabunge wa Bunge maalumu la katiba wamekataa mahakama ya kadhi kuwa kwenye katiba. Lakini wameona kwamba mahakama hiyo iwepo lakini iendeshwe na wahusika. Wanasema hata kwenye katiba ya Zanzibar hakuna mahakama ya kadhi. Wamesema mahakama inaweza kuwepo lakini si lazima iwe ndani ya katiba. Kuweka mahakama ya Kadhi kwenye katiba ni kuilazimisha serikali ihudumie.

Hii ni habari njema kwa nchi yetu kwani maswala ya dini ni bora yawe nje ya serikali maana nchi hii ina wapagani, waislam, wakristu, na watu wanaomini katika mila zao, hivyo si jambo jema kwa imani moja kuhudumiwa na kodi za imani zote.

Source: ITV
 
Ili kumaliza mvutano uliopo kati ya wakristo na waislamu napendekeza Waislamu wapewe hiyo mahakama ya kadhi kama wanavyodai. Tena wapewe na ruzuku ya uendeshaji wake.

Kwa upande mwingine yale madhehebu ya kidini (wakiwemo Wakristo na Waislamu) yaliyo na huduma muhimu za jamii na hasa mahospitali, vituo vya afya na dispensaries wapewe ruzuku na serikali ili kuziendesha hizo huduma za kijamii kadri ya uwezo. Hii itamaliza malalamiko na mgogoro kwa pande zote mbili.

Iwapo vyama vya siasa vinapewa ruzuku za uendeshaji wa shughuli zao, siyo vibaya serikali ikiweza kufanya hivyo kwa huduma za jamii zinazofanywa na madhehebu ya dini ili kuleta usawa na kudumisha amani.
 
Hili wazo binafsi nimelipenda sana. Hapa jambo muhimu ni kudumisha amani na upendo katika nchi yetu.
 
Hili wazo binafsi nimelipenda sana. Hapa jambo muhimu ni kudumisha amani na upendo katika nchi yetu.
Unajua CCM wanataka kutumia kete ya udini na hoja ya mahakama ya kadhi ili kuendelea kubaki madarakani. Sasa kama kweli wana dhamira njema watende haki kwa dini zote. La sivyo UKAWA walitumie hili suala la ruzuku kwa mahakama ya kadhi, na ruzuku kwa huduma za jamii kwa dini zote, kama sehemu ya ilani yao ya uchaguzi.
 
Back
Top Bottom