Mahakama ya kadhi ndani ya Katiba - Tanzania

Mahakama ya kadhi ndani ya Katiba - Tanzania

Sasa ikiwa ninyi mnaotaka mahakama ya kadhi kwa ajili ya mambo yenu ya kidini, lakini pia hamuwezi kuheshimu maamuzi hayo, ni nani hasa anayependa hiyo mahakama? Nilidhani waislam mnaitaka kwa sababu itawatendea haki nyote, kinyume na sheria za serikali. Sasa kama ndivyo, waislam wenyewe hawawezi kutii amri za ki mungu wenu, unataka serikali iwaongezee imani?

Kama haifanyi kazi maana yake waislam hawaitaki na ndiyo maana hawaitii. Sasa wewe ni nani unayewalazimisha wenzako kwenye hili jambo? Una maslahi gani makubwa kuliko waumini wenzako?

Achaneni nayo muendelee na mahakama za kawaida ambazo hazijawabagua na wala hamjazuiliwa na mtu kwenda.


mahakama ya kadhi haiwahusu wakristo na tunachotaka waislam itambuliwe kwenye katiba kama zinavyotambuliwa mahakama zingine kama za ardhi,biashara,kazi nk pia kama taasisi na swala la kugharamia gharama ni jambo jingine na ni jukumu letu tutaju sisi pa kuzipata. lakini mbona nyinyi wakristo munapewa pesa kupitia mkataba wa MOU uliosainiwa na lowasa mwaka 1992 ?? sisi hatujapewa mkataba huo mpaka leo?
Umuhimu wa kutambuliwa kwa mahakama ya kadhi ni nyingi ila nitataja moja kwa kuwa leo kdhi kashateuliwa na muft kupiti bakwata laki hatambuliki
endapo kwa mfano imetokea kadhi ametoa hukumu kati ya JUMA na HASSAN kwamba mali hii ni ya JUMA kwa mujibu wa mafundisho.lakini HASSAN hataki kukabidhi utatumia njia gani kumlazimisha HASSAN kutoa mali kumpa JUMA wakati kadhi hatambuliki kisheria??
na mambo hayo yanatokea leo kesi nyingi zinazohusu kadhi zimepelekwa bakwata na hukumu inatoka lakini inakuwa tabu kutekelezeka
 
CHUAKACHARA

Umesema jambo sahihi kabisa. Sasa hivi ccm inavuta hewa kwa msaada ya risasi za jeshi la polisi tu.

Ninachoamini ni kwamba hawa polisi ni binadamu kama sisi. Wanachokifanaya ni utill wa amri za mwajiri. Lakini pia wana hisia na dhamira. Amini tu, ipo siku nguvu ya dhamira na nafsi itashinda kiapo cha utii. Wataigeuka serkali dharimu, watachoka kuua ndugu zao. Wataungana na umma wa wa Tanzania ili kudai taifa huru. Ndipo aibu ya iliyokuwa ccm itakapokuwa dhahiri machoni pa dunia nzima.

Ninachoelewa, kuna waslam wengi tu ambao wanaona mbali na wako kinyume na mpango wa ccm kuwawekea mahakama ya kadhi kwa sababu ya sauti za watu wachache wanaotaka kuwaonea wengine.

Hadi hapa ccm imekosa control kwa taifa na tayari imeshaasisi machafuko makubwa sana iwapo hapatakuwa na hekima ya kubadilisha mwelekeo wa kisiasa na kidini hapa tz.

Mungu yupo upande wetu mwanangu. Tutashinda.
Tabby

CCM wajue kuwa wanaipeleka nchi kwenye vita ya dini! Madhehebu mengine ya kikristo yakidai mahakama zao kwenye katiba watawakatalia! Au wakidai lolote liwe kwenye katiba watakuwa na kigezo gani cha kuwakatalia. Let us wait and see. Labda kwa vile CCM ina risasi, itaua wakristo!
 
CHUAKACHARA

Umesema jambo sahihi kabisa. Sasa hivi ccm inavuta hewa kwa msaada ya risasi za jeshi la polisi tu.

Ninachoamini ni kwamba hawa polisi ni binadamu kama sisi. Wanachokifanaya ni utill wa amri za mwajiri. Lakini pia wana hisia na dhamira. Amini tu, ipo siku nguvu ya dhamira na nafsi itashinda kiapo cha utii. Wataigeuka serkali dharimu, watachoka kuua ndugu zao. Wataungana na umma wa wa Tanzania ili kudai taifa huru. Ndipo aibu ya iliyokuwa ccm itakapokuwa dhahiri machoni pa dunia nzima.

Ninachoelewa, kuna waslam wengi tu ambao wanaona mbali na wako kinyume na mpango wa ccm kuwawekea mahakama ya kadhi kwa sababu ya sauti za watu wachache wanaotaka kuwaonea wengine.

Hadi hapa ccm imekosa control kwa taifa na tayari imeshaasisi machafuko makubwa sana iwapo hapatakuwa na hekima ya kubadilisha mwelekeo wa kisiasa na kidini hapa tz.

Mungu yupo upande wetu mwanangu. Tutashinda.

Uko sahihi, polisi wana ndugu zao, marafiki majirani na wengine. Watachoka kuwaua bila sababu za msingi. Dhamira za polisi zitawasuta na watauona ukweli na watausimamia. Mambo ya imani wayaache kila dini iyasimamie. Kutafuta kura kwa njia za kuhatarisha amani ni hatari.
 
Sasa ikiwa ninyi mnaotaka mahakama ya kadhi kwa ajili ya mambo yenu ya kidini, lakini pia hamuwezi kuheshimu maamuzi hayo, ni nani hasa anayependa hiyo mahakama? Nilidhani waislam mnaitaka kwa sababu itawatendea haki nyote, kinyume na sheria za serikali. Sasa kama ndivyo, waislam wenyewe hawawezi kutii amri za ki mungu wenu, unataka serikali iwaongezee imani?

Kama haifanyi kazi maana yake waislam hawaitaki na ndiyo maana hawaitii. Sasa wewe ni nani unayewalazimisha wenzako kwenye hili jambo? Una maslahi gani makubwa kuliko waumini wenzako?

Achaneni nayo muendelee na mahakama za kawaida ambazo hazijawabagua na wala hamjazuiliwa na mtu kwenda.

Tambua kila jamii inamafisadi,matapeli,walevi,wazinzi,mashoga, nk.Na vyote hivyo vinakatazwa kwenye vitabu dini zote.hatuwezi kuachana na jambo ambalo mungu analitaka na ni lazima kwa sababu mungu kaagiza wanaokataa ni hao kwenye red.Na watu au familia haziwezi kwenda mahakamani pale endapo itatokea kutokuelewana kunakosababishwa na hao niliopigia mstari au kwa jambo lingine lolote hususani dhulma hivyo mahakama pekee ndo kimbilio la wanyonge.Pia ugumu wa kutekelezeka unakuja kwa hivi ...Kwanye mahakam zote kunakuwa na madalali wa mahakama au polisi aidha wa magereza au wa askari wa kawaida ambao husaidiwa kutekelezwa kwa hukumu, husubiri hukumu ya mahakama wamsaidie muhusika pale inapotokea aliyeshindwa hataki kutekeleza amri ya mahakama sasa kama mahakama haipo kwenye katiba ni dalali gani wa mahakama au polisi atakayekubali hilo.Kubwa tunachotaka ni kuwa mambo ya ndoa na mirathi lisiwe la kiserikali labda kwa wale waliofunga ndoa BOMANI.Hata nyinyi mkitaka daini hatutawaingilia waswahili wanasema PILIPILI USIYOILA YAKUWASHIANI????
 
Mimi binafsi sina kinyongo ikiwa dini moja itafadhiliwa na serikali kuendesha mahakama yao ya wafuasi wa dini hiyo.
Kama sijakosea ni mpk wale ma sheikh kwenye mahakama hizo watakao kua wana suluhisha na kutoa judgment mshahara wao utatoka serikalini.
Kuna maneno ya mtaani kua serikali ya ccm imeamua kufanya hivyo ili ipate support kutoka kwa waislamu wa bakwata ambao ni pete na kidole na ccm kupitisha katiba ya kichina.
Sasa niende kwenye mada yangu wakristo wamegawanyika ktk madhehebu mbali mbali kuna waroman catholic, wa lutheran, wa pentecoste, wasabato na makanisa mengine.

Wa adventista wasabato kabla na baada ya uhuru wamekua na kilio cha kutaka siku ya sabato iheshimiwe; HAKUNA WASABATO BILA KUTUNZA SABATO.

Sabato inatunzwaje inaheshimiwaje hebu niwapeleke kwenye amri kumi za Mungu ya nne inasema hivi

''[4] Ukumbuke siku ya sabato uitakase siku sita fanya kazi utende mambo yako yote; lakini siku ya sabato ni ni ya Bwana, Mungu wako siku hiyo usifanye kazi yo yote wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako,wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako.maana kwa siku sita Bwana Mungu alifanya mbingu na nchi na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibaria siku ya sabato akaitakasa."

Waislamu watapewa mahakama ya kadhi kwa gharama za serikali kutokana na uhusiano wa BAKWATA na CCM lakini wasabato hata bungeni nahisi hakuna mbunge hata mmoja msabato, labda Upendo Peneza ndio mMabato nayemjua aliyeko kwenye uwanja wa siasa tena ni mgombea tu wa BAVICHA, hii inadhihirisha kuwa wasabato hawana uwakilishi bungeni.

Mashuleni ,vyuoni wanafunzi wamekuwa wakifukuzwa kutokana na kukataa either kufanya kazi au mitihani siku ya sabato yani Jumamosi hili limeendelea kwa muda mrefu na sijaona serikali ikitoa tamko.

Ijumaa jua likizama mpaka Jumamosi jua likizama ndio siku ambayo amri ya nne inaongelea nilioweka hapo juu.

Sasa serikali kabla ya kushurutishwa mchague kufuta dini ya kisabato au wapewe ruhusa ya kufuata taratibu za dini bila kubugudhiwa au kufukuzwa ktk taasisi za kielimu na makazini.

Mwisho kabisa niwape ongera BAKWATA kwa kupata mahakama ya kadhi. Nawasihi mtumie vizuri kodi zetu kwa kutoa haki.
 
Nchi gani duniani inafuata taratibu hizo za kisabato? naomba ushahidi tafadhali kabla ya kuendelea na mjadala kuunga mkono au kupinga.
 
R.i.p muslim
 

Attachments

  • 1409118363610.jpg
    1409118363610.jpg
    31.6 KB · Views: 118
Nchi gani duniani inafuata taratibu hizo za kisabato? naomba ushahidi tafadhali kabla ya kuendelea na mjadala kuunga mkono au kupinga.
usitake kufanya kila kitu kwa kuangalia kama kiliwahi kufanya ama laa!
You can also be the first one to do it.
 
Hizi mada zenye udini ndani yake mimi huwa naziita za kijinga kabisa.
 
Tatizo lako ni ushabiki na husda, huna la ziada. unataka kuishawishi jamii wa watanzania hasa wakristo kuwa mahakama ya kadhi italeta vita!? huenda ww ndio hujafanya utafiti juu ya hili. Znz, Kenya, Uganda, SA na hata Uingereza kutaja kwa uchache zinamahakama ya kadhi. je umeshawahi sikia kuwa mahakama hizo zimesababisha vita? mahakama ni chombo cha haki na kuwekewa utaratibu maalum kwa uendeshaji wake. By the way hiyo mahakama ww haitakuhusu sasa jasho la nn? hata hvy wewe endelea tu kutetemeka na pengine jiny...kabisa, lakini wapaswa kujua kuwa watu wa aina yako ndio watakao iingiza nchi kwny shida na si mahakama.

hizo nchi ulizotaja ni tofauti na Tanzania ambayo ina waislam waliogawanyika sana,hiyo mahakama ikianzishwa na kusimamiwa na serikali na makadhi kuanza kulipwa hebu niambie makadhi watatoka wapi bakwata au wapi?,aisee kutakuwa na fujo tu,maana hata makadhi waliopo sasa hawakubaliki na wanaharakati.
 
ila kweli ukristo mzuri maana wanaruhusu kuoana jinsia moja na kupata watoto kingine wako kwenye mchakato mapandre waoe la mapandre likifaulu la masister watu wanataka dini ambayo inabadirika kama kinyonga

acha uzushi ni ukristo gani unaoruhusu ushoga na ndoa za jinsia moja! weka aya toka kwenye biblia,ndg ikisikia shehe kabaka basi mashehe wote wabakaji sio hivyo hio ni tabia yake tu.hakuna dini inayoruhusu maovu kama hayo si uislam wala ukristo.
 
Ndugu zangu, nimeshtushwa sana na habari niliyoisoma hata jukwaani kwamba ccm inaandaa sura mpya katika katiba ya nchi itakayosimamia mahakama ya kadhi.

Sichukii dini na imani za watu lakini ninaangalia amani na mwelekeo wa tiafa hili kwa sasa. Kwa muda wote katia historia ya nchi yetu, serikali haijawahi kuwa na dini lakini raia wake wamepewa uhuru wa kuabudu dini wanazozitaka ili mradi wasivunje sheria.

Ni jambo lisilomithirika, kwa ccm kuiingiza nchi yetui kwenye dhahama hii wakat dunia nzima ikishuhudia tabu ambazo watu wanapata kutokana na kuwa na serikali zenye udini.

Ninaomba ndugu zetu wa ccm, acheni jambo hili. Hamjalifanyia utafiti ila mnafanya kinafiki ili kuwa impress wazanzibar wawape 2/3 na kutafuta kura kwa misingi ya udini. Msitupeleke huko. Mnafanya jambo la hatari kuliko yote mliyowahi kufanya.

Ninaomba suala la kadhi waachiwe waislam wenyewe walisimamie na kulitekelza kuliko serikali kujiingiza katika jambo la namna hii.

Ninatetemeka, nashindwa kuandika.

Wanaoitakia mema Tanzania, wakiwemo wana ccm, waisllam na watu wa dini zote, naomba tusimamie amani ya taifa hili ambayo sasa ccm imeama kuizika rasmi.

SITA UMEFANYA LINI RESEARCH HADI UKA VALIDATE KWAMBA MAHAKAMA YA KADHI ITAONDOA KERO ZA MUUNGANO? UNA MAAGANO GANI NA DAMU YA WANTANZANIA?

Mahakama ya kadhi itatuhusu waislamu wewe inakuuma nini mbona tuna mahakama za kisekula tayari au ni dhambi kwa waislamu kujiamulia masuala yetu kwa misingi ya imani yetu pasipo kuvunja she ria za nchi?
 
Mods Naomba Pls Uzi Huu Ujitegemee,ccm Kama Kawaida Yake Inatapatapa Ili Iendelee Kutawala,baada Ya Kuona Kuwa Wapinzani Wameungana Na Ikijua Kuwa CUF Na Chadema Wana Itikadi Tofauti Za Kidini,imeamua Kwa Makusudi Kuruhusu Mjadala Wa Mahakama Ya Kadhi Lengo Likiwa Ni Kuwafarakanisha UKAWA,ili Ipate Upenyo Wa Kushinda Kiulani Kumbe Ndo Inajichimbia Kaburi,taifa Letu Lina Mikoa 27 Ni Mikoa Mitano Tu Ktk Yote Ambako Ndo Kuna Waislamu Wengi,22 Yote Ni Wakristo Kwa Wingi Na Wapagani,ikijidanganya Eti Ndo Itashinda Huo Ndo Unaenda Kuwa Mwisho Wa CCM,wakristo Wote Kwa Ujumla Wetu Na Wapagani Pia Hatutaichagua ccm endapo Itaridhia Mahakama Ya Kadhi,imani Yao Ya Dini Isiwe Kero Kwetu,Tanzania Hakuna Dini Ila Watu Wake Tuna Dini,kwanini Sasa Mambo Ya Dini Yaingie Kwenye Katiba Inayotumika Na Dini Zote? Basi Na Sisi Wakristo Tudai Ktk Katiba Mpya Kiwepo Kipengele Chetu Cha Kuutambua Uislamu Kama Ugaidi,si Ndo Uhuru Huo Wanaoutaka Waislamu? Tuone Kama Nchi Itakalika Hii.
 
Moderator unganisha huu uzi kuna nyuzi ina mantiki hii imekuja hapa asubuhi, juku ni kujaza server
 
Last edited by a moderator:
Uko sawa wiseboy ila nakukumbusha huku ACACIA GOLD MINE zamani BARRICK mshahara umetoka,tuko STANBIC BANK tunavuta mahela jioni Kakola vururuvururu.
 
Hiii ikipita tuu jamani mahakama ya kadhi ccm kwishneeeeee

Na watajuta kuijadili bungeni hawa ccm
 
Uko sawa wiseboy ila nakukumbusha huku ACACIA GOLD MINE zamani BARRICK mshahara umetoka,tuko STANBIC BANK tunavuta mahela jioni Kakola vururuvururu.

Duh! Kuweni Makini Jamani Kakola Karibia Yote Imeoza Kabisa.
 
Hatuwezi kuruhusu kila kikundi cha dini kiwe na mahakama yao! Hii itakuwa ni vurugu!
Mwisho wapagani watataka mahakama yao, wakristo ya kwao hadi walevi watataka mahakama yao.
Hakuna mjadala, no mahakama ya kadhi hapa tz.
Cc FaizaFoxy
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom