Mahakama ya Kisutu imewaachia Huru washtakiwa wawili kesi ya kuanguka kwa jengo Kariakoo

Mahakama ya Kisutu imewaachia Huru washtakiwa wawili kesi ya kuanguka kwa jengo Kariakoo

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
557
Reaction score
1,039
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru washtakiwa wawili kati ya sita waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya kuua bila kukusudia baada ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa, eneo la Kariakoo.

Wawili hao ambao ni Zenabu Silam (61) na Ashour Awadhi Ashour (38) wameachiwa huru leo baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) kusema hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi yao.

Hatua hiyo imekuja baada ya Wakili wa Serikali, Christopher Olembelle kumueleza Hakimu Mkazi Mwandamizi, Godfrey Mhini ya kwamba DPP amewasilisha hati ya kutoendelea na kesi dhidi ya washtakiwa hao wawili.

Washtakiwa wanne waliobaki katika kesi hiyo ni Leondela Mdete (49), Soster Nziku (55), Aloyce Sangawe (59) na Stephen Nziku (28) wote ni wakazi wa Dar es Salaam.

Soma Pia: Kesi ya Jengo kuporomoka Kariakoo yaahirishwa hadi Desemba 30,2025

Washtakiwa wote wanadaiwa kutenda kosa hilo, Novemba 16, 2024 katika mtaa wa Mchikichi na Congo eneo la Kariakoo ambapo isivyo halali walishindwa kutimiza majukumu yao na kusababisha vifo vya watu 31.

kariakoo.png
 
Kwa mahakama zetu hizi hapo lazima wamehonga pesa ndefu, ili waachiwe bila hivo wangeendelea kusota hukohuko.
 
Back
Top Bottom