KERO Mahakama ya Rufaa Tanzania (CAT), Utaratibu wenu wa Fi'Fo ni wa KIBAGUZI

KERO Mahakama ya Rufaa Tanzania (CAT), Utaratibu wenu wa Fi'Fo ni wa KIBAGUZI

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Kwayu

Platinum Member
Joined
Nov 8, 2007
Posts
511
Reaction score
108
Mahakama ya Rufaa Tanzania wamekuwa wakijinasibisha kuwa wanatumia kanuni ya FIFO (First In and First Out) kushughulikia mashauri ya madai mahakamani jambo ambalo si kweli.

Nina madai ya rufaa namba 700/2023 ambayo mpaka sasa hata kuwekwa kwenye mfumo wa tehama hayajawekwa, lakini ukiangalia Tanzlii mashauri mengi ya mwaka 2023, 2024, na 2025 yaliyofunguliwa baada ya shauri langu yamesikilizwa na kutolewa hukumu. Mengi ya mashauri haya yaliyofunguliwa na kuamuliwa ni mashauri yanayohusu makampuni. Ina maana sisi watu binafsi hii kanuni haina maana kwetu?

Mheshimiwa Jaji Mkuu, naomba shauri langu Civil appeal no 700/2023 lililofunguliwa mahakama ya rufaa kanda ya dar es salaam lipangiwe session. Sisi watu binafsi pia tuna haki sawa na hayo makampuni.

Zingatieni kanuni yenu ya FIFO kwa haki.
 

Attachments

  • Screenshot_20251204_013401_Chrome.jpg
    Screenshot_20251204_013401_Chrome.jpg
    147.3 KB · Views: 31
Mahakama ya rufaa iweje kesi zilizofunguliwa 2025 zimesikilizwa na kutolewa hukumu wakati sisi wa 2023 bado tuko pending? Wakati hizi mlizotoa hukumu hazikufunguliwa hata kwa hati za dharura?
 
Mahakama ya rufaa iweje kesi zilizofunguliwa 2025 zimesikilizwa na kutolewa hukumu wakati sisi wa 2023 bado tuko pending? Wakati hizi mlizotoa hukumu hazikufunguliwa hata kwa hati za dharura?
Andika certificate of urgency na iwasilishe
 
Back
Top Bottom