Mahakama ya Rufaa yaamuru Uhamiaji kurejesha passport ya Aidan Eyakuze

Mahakama ya Rufaa yaamuru Uhamiaji kurejesha passport ya Aidan Eyakuze

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Mahakama imetengua uamuzi uliotolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania Oktoba 2019 dhidi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Twaweza, Aidan Eyakuze.

Imeamuru Idara ya Uhamiaji kukamilisha uchunguzi wao na kurejesha Hati ya Kusafiria (Passport) ya Eyakuze ndani ya siku 60 kuanzia Ijumaa (Desemba 4, 2020).

1607435822001.png

8B11AF69-B0B9-4F60-BE7D-273FAC992C33.jpeg

B2CD2C5E-E5F3-420B-B580-E309FB0182D8.jpeg


Pia soma: Uhamiaji washikilia passport ya Mkurugenzi wa Twaweza, Aidan Eyakuze
 

Attachments

Haahaa hiyo mahakama hakuna jipya ilichofanya, na huo uamuzi huenda usitekelezwe
 
Tujikumbushe

Tuesday April 14 2020​

Idara ya Uhamiaji nchini Tanzania imesema uchunguzi wa uraia wa baadhi ya watu wanaotiliwa shaka unaendelea kufanyika na ni mgumu

Uhamiaji wataja "ugumu" uchunguzi wa uraia wa Nondo, Eyakuze​

N SUMMARY​

Baadhi ya watu wanaochunguzwa uraia wao ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Twaweza, Aidan Eyakuze; Askofu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zachary Kakobe na mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ya Chama cha ACT-Wazalendo, Abdul Nondo.

Dar es Salaam. I
dara ya Uhamiaji nchini Tanzania imesema uchunguzi wa uraia wa baadhi ya watu wanaotiliwa shaka unaendelea kufanyika na ni mgumu.

Baadhi ya watu wanaochunguzwa uraia wao ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Twaweza, Aidan Eyakuze; Askofu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zachary Kakobe na mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ya Chama cha ACT-Wazalendo, Abdul Nondo.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumanne Aprili 14, 2020 msemaji wa Uhamiaji, Paul Msele amesema bado idara hiyo inaendelea kufanya uchunguzi kwa kuwa kuna mambo mengi ya kuchunguza na wakati mwingine wanahitaji kuvuka nje ya mipaka ya nchi.

"Uchunguzi wa uraia ni mgumu sana wakati mwingine unahitaji kutoka nje ya mipaka kutokana na aina ya familia mtu aliyotoka na kuna vitu vingi katika kuchunguza uraia wa mtu,” amesema Msele.

Eyakuze aliingia matatani Julai 2018 ikiwa ni siku chache baada ya taasisi anayoiongoza kupewa barua na Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech), ikitakiwa kujieleza kwa nini isichukuliwe hatua kwa kutoa utafiti bila kibali.

Utafiti huo ni ule wa sauti za Wananchi ulioonyesha umaarufu wa baadhi ya viongozi umeshuka.

Mwingine ni Askofu Kakobe ambaye wakati wa sherehe za Krismasi mwaka 2017 alisema kanisani kwake kuwa ana fedha nyingi kuliko Serikali.

Siku chache baadaye aliyekuwa kamishna mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Charles Kichere alisema kuwa Kakobe hayumo kwenye kumbukumbu za ulipaji kodi wa mamlaka hiyo.

Mwezi Aprili, 2018 aliitwa na Idara ya Uhamiaji na kuhojiwa kuhusu uraia wake.

Naye Nondo alihojiwa na maofisa wa Uhamiaji wakati kesi yake ikiendelea Mahakama Kuu. Katika mahojiano hayo, Nondo alitakiwa kupeleka vyeti vya kuzaliwa vya wazazi wake pamoja na vya bibi na babu zake wa pande zote.

Kabla ya kuhojiwa, Nondo ambaye kipindi hicho alikuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) alikamatwa na polisi mjini Mafinga, wilayani Mufindi, Iringa na kufikishwa mahakamani akidaiwa kuidanganya polisi kuwa ametekwa.
Source : Gazeti la Mwananchi
 
Ila jiwe yuko juu ya sheria na yeye ndiye sheria yenyewe aendelee tu kuishikilia.
 
Kosa la huyu jamaa ni kufanya utafiti akiwa ni muajiriwa wa TWAWEZA kuhusu umaarufu wa nanihii na kusema umeshuka toka 90+ hadi 55%.

Jamaa akanuna akaamua afuatiliwe na kumbambikia kesi kwamba si Mtanzania kitu ambacho si cha kweli. Na kampuni yao ya TWAWEZA nadhani imefutwa.
 
Mahakama haina uwezo kupinga maagizo hizo ni sarakasi baada ya uchaguzi kuisha na utafiti wake kutokuwa na madhara.
 
Hata wazee wa escrow wakiusujudia na kuhubusu msalaba mkuu watarejeshewa Uhuru wao.
Ukinisijudia na kuyabusu mawe haya nitakuweka huru
 
Ila jiwe yuko juu ya sheria na yeye ndiye sheria yenyewe aendelee tu kuishikilia.
Zamani Mwenye Pesa Alikuwa Anaweza Kuifanya Chochote Serikali, Lakini Kwenye Utawala Wangu Mwenye Pesa Anaweza Kufanywa Lolote!!! Hakuna NEUTRAL
 
Zamani Mwenye Pesa Alikuwa Anaweza Kuifanya Chochote Serikali, Lakini Kwenye Utawala Wangu Mwenye Pesa Anaweza Kufanywa Lolote!!! Hakuna NEUTRAL
Hata kutekwa nyara na wazungu wanaoongea kiswahili wakati akienda gym!?
 
Jina la Rwanda hili wala si la Kihaya ingawa yanaelekeana. Sijasema ni Rwandese

Ila Rwandese wapuuzi siwakubali wote ninaosoma nao hawaelewi kitu nchini wala roho zao haziko huku. Unakuta kenge anakubishia eti mkoa wa Kagera ulikuwa eneo la Rwanda miaka ile ya mababu kabla ya wakoloni.
 
Back
Top Bottom