Mahakama ya Rufaa yasisitiza Mchechu kulipwa Sh Bilioni 2.5 na kampuni ya Mwananchi Communication Ltd

Mahakama ya Rufaa yasisitiza Mchechu kulipwa Sh Bilioni 2.5 na kampuni ya Mwananchi Communication Ltd

Siku hizi serikali watu hawaii kama zamani watu wanaiba kihalali kabisa kwa vifungu vya sheria.......unda kampuni jipe tenda kazi imeisha.

Huyu mchechu ana mzigo wa hatari...picha kinaanza nyumbani kwake kuna nyumba mbili kubwa na ndogo ukienda kajamba nani humuoni unaishia nyumba ndogo ucheze na walinzi.
Ni dhambi kwa mkulima wa mpunga kumiliki mchele?
 
Mahakama ya Rufani ya Tanzania leo imetoa uamuzi wake katika Rufaa Namba 658 ya mwaka 2023, iliyowasilishwa na Mwananchi Communications Ltd pamoja na Mhariri wa The Citizen Newspaper, dhidi ya Nehemia Kyando Mchechu, na kutupilia mbali maombi hayo kwa kukubaliana na maamuzi ya Mahakama Kuu yaliyotolewa tarehe 3 Machi 2023 mbele ya Jaji Mgonya.
20250605_120541.jpg

Katika uamuzi huo uliotolewa mbele ya jopo la Majaji watatu wa Mahakama ya Rufani, mahakama hiyo ilipitia hoja kuu tatu zilizowasilishwa katika rufaa hiyo.

Hoja hizo ni pamoja na:
• Iwapo Mahakama Kuu ilikuwa na mamlaka ya kusikiliza shauri hilo,
• Iwapo mdai (Mchechu) aliweza kuthibitisha madai yake ya kudhalilishwa,
• Iwapo Mahakama Kuu ilitumia utaratibu sahihi kutoa nafuu na fidia zilizotolewa

Majaji wa Mahakama ya Rufani walikubaliana na hoja zilizowasilishwa na wakili wa upande wa mjibu rufani, Wakili Aliko Harry Mwamanenge, na kueleza kuwa:
• Mahakama Kuu ilikuwa na uwezo halali wa kusikiliza shauri hilo;
• Mdai (Mchechu) aliweza kuwasilisha ushahidi thabiti kuthibitisha kuwa alidhalilishwa;
• Mahakama Kuu ilifuata misingi sahihi ya kisheria katika kutoa nafuu zilizotolewa katika hukumu yake.

Mahakama yaamuru Gazeti la The Citizen kumlipa aliyekuwa Bosi wa NHC, Nehemia Mchechu Bilioni 2

Kwa mantiki hiyo, Mahakama ya Rufani haikuona sababu yoyote ya kubatilisha au kurekebisha maamuzi ya Mahakama Kuu, hivyo ikayathibitisha maamuzi hayo kama yalivyotolewa.

Katika uamuzi wa awali wa Mahakama Kuu, Mwananchi Communications Ltd pamoja na
Mhariri wa The Citizen Newspaper walikutwa na hatia ya kuchapisha taarifa zilizomdhalilisha Nehemia Kyando Mchechu, na mahakama ikaamuru walipe fidia pamoja na gharama nyingine kama ilivyoainishwa katika hukumu ya Machi 3, 2023.

Kwa msingi huo, Mahakama ya Rufaa imefunga kesi hiyo na kuitaka Kampuni ya Mwananchi Communication Ltd kumlipa Bw. Nehemiah Mchechu shilingi Bilioni 2.5 kwa kumdhalilisha

Rufaa hiyo ilisikikizwa chini ya majaji watatu ambao ni Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Rehema Kerefu, Jaji Omar Othman Makungu na Jaji Dkt.Benhajj Masoud
 
Imeisha hioo mwenye nacho aongozewee
 
Mahakama ya Rufani ya Tanzania jana imetoa uamuzi wake katika Rufaa Namba 658 ya mwaka 2023, iliyowasilishwa na Mwananchi Communications Ltd pamoja na Mhariri wa The Citizen Newspaper dhidi ya Nehemia Kyando Mchechu, na kutupilia mbali maombi hayo kwa kukubaliana na maamuzi ya Mahakama Kuu yaliyotolewa Machi 3, 2023.

Katika uamuzi huo uliotolewa mbele ya jopo la Majaji watatu - Jaji Rehema Kerefu, Jaji Omar Othman Makungu na Jaji Dk. Benhajj Masoud - Mahakama ya Rufani ilipitia hoja mbalimbali ikiwemo:Iwapo Mahakama Kuu ilikuwa na mamlaka ya kusikiliza shauri hilo, Iwapo mdai (Mchechu) aliweza kuthibitisha madai yake ya kudhalilishwa, Iwapo Mahakama Kuu ilitumia utaratibu sahihi kutoa nafuu na fidia.

Majaji walikubaliana na hoja za wakili wa upande wa Nehemia Mchechu, Wakili Aliko Harry Mwamanenge, na kueleza kwamba Mahakama Kuu ilikuwa na uwezo wa kusikiliza shauri hilo, na kwamba mdai aliwasilisha ushahidi thabiti kuthibitisha kuwa alidhalilishwa. Pia, Mahakama Kuu ilifuata misingi sahihi ya kisheria katika kutoa nafuu na fidia.

Kwa msingi huo, Mahakama ya Rufani imethibitisha maamuzi ya Mahakama Kuu na kuitaka Mwananchi Communications Ltd kumlipa Bw. Nehemia Kyando Mchechu kiasi cha shilingi bilioni 2.5 kama fidia kwa kumdhalilisha pamoja na gharama nyingine kama ilivyoamuliwa awali.
 
wakishazilipa watakuwa na adabu ya kuandika habari sahihi na si kuchafua watu ili wauze magazeti na hapa pia ndiyo wataelewa umuhimu wa kuwa na waandishi wa habari wenye sifa stahiki.
 
Back
Top Bottom