Mahakama ya Rufani: Maamuzi ya Rais kuhusu Wafanyakazi wa Umma ni ya mwisho

Dominic A. Kalangi alikuwa mfanyakazi wa Shirika la Posta (Tanzania Posts Corporation), mwaka 2017 ajira yake ilisitishwa Kwa utovu wa nidhamu.
 
Dominic A. Kalangi alikuwa mfanyakazi wa Shirika la Posta (Tanzania Posts Corporation), mwaka 2017 ajira yake ilisitishwa Kwa utovu wa nidhamu.
Mahakama katika hukumu hiyo haijatoa uamuzi kwa kesi ya Dominic tu bali hata kwa kesi za watumishi wengine wa umma zilizopo CMA, na vilevile imezuia kabisa watumishi wa umma wenye migogoro ya kazi na waajiri wao kuwasilisha migogoro hiyo CMA
 
Rais wa Tanzania ni Malkia & Mfalme.

Katiba ni lazima iangaliwe upya.
 
Ipoje hiyo Mkuu? Ingekuwa vema ukafafanua ili nipate uelewa kuhusu hiyo judicial review mara baada ya uamuzi wa Rais.
Sawa mkuu ipo hivi;

Maamuzi ya Rais ni Administrative order na kwakua ni final kwenye ranks za utawala basi njia pekee ya kuya challenge ni kwa kupitia Mahakama ambapo mhusika atapeleka maombi mahakama kuu akiiomba ifanye marejeo ya maamuzi ya Rais na kutoa amri kama yapo sahihi au la.
 
Nashukuru kwa ufafanuzi Mkuu, maana kuna ndugu yangu ni Mhanga, amekata Rufaa kwenda kwa Rais mara baada ya kutoridhishwa na maamuzi ya Tume ya Utumishi wa Umma, Rufaa amekata tangu mwaka 2019, lakini bado hajajibiwa mpaka sasa.
 
Nashukuru kwa ufafanuzi Mkuu, maana kuna ndugu yangu ni Mhanga, amekata Rufaa kwenda kwa Rais mara baada ya kutoridhishwa na maamuzi ya Tume ya Utumishi wa Umma, Rufaa amekata tangu mwaka 2019, lakini bado hajajibiwa mpaka sasa.
Kama hajaridhika na maamuzi ya Rais anaweza omba judicial Review Mahakama kuu.

Public Service Act inasema kwamba ili kutumia any other avenues lazima uexhaust zile zilizokuwa provided kwenye hiyo act.

Maamuzi ya Rais ndio final kwa watumishi wa umma ila sio ya mwisho kisheria.

Bado unaweza itumia mahakama na njia ya kuitumia ndio hiyo ya judicial review.
 
Hiki kifungu kineanza lini?na je waliofukuzwa kazi kabla ya kifungu hiki wanafanyaje?
 
Tarehe 19.05.2022, nimefungua Review katika Mahakama ya Rufaa Tanzania, iweze kurejea uamuzi wake huo kwa kuwa ni batili na umeleta shida kwa umma (jamii) hususani watumishi wa umma. Ni maombi namba 265/07 ya 2022, ninasubiri tarehe ya kusikilizwa tukaweke mambo sawa ili haki waliyoporwa watumishi wa umma irejeshwe kisheria.
 
Tunaomba uweke hapa hayo maombi yako,plz!!
 
Sasa hapo uhuru wa mahakama kama muhimili huru uko wapi?
Rais ni mwajiri wa ngazi ya juu wa watumishi wa umma,sasa iweje mwajiri umpe mamlaka ya kuamua lipi ni sahihi na lipi si sahihi? Alafu mtu atwambie kwamba mahakama ipo kwa ajiri ya kutoa haki
Ngoja niishie hapa ila kuna mambo mengi hayana majibu ya wazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…