Mahakama ya Rufani: Maamuzi ya Rais kuhusu Wafanyakazi wa Umma ni ya mwisho

Mahakama ya Rufani: Maamuzi ya Rais kuhusu Wafanyakazi wa Umma ni ya mwisho

Rais anaposikiliza rufaa ya mtumishi wa umma hafanyi kama Rais (mwanasiasa) bali kama mamlaka ya nidhamu kwa mwajiriwa.

Maamuzi yake yanaweza kupingwa mahakamani wakati akiwa Rais mwanasiasa, anachokisema hakiwezi kupingwa mahakamani isipokuwa tu kikiwa kinavunja Katiba ya nchi.
Mkuu sajo iwapo rufaa itatupilwa mbali inapofika kwa Raisi muhusika akaenda mahakamani halafu makahama akashinda hapo inakuwaje?
 
Mkuu sajo iwapo rufaa itatupilwa mbali inapofika kwa Raisi muhusika akaenda mahakamani halafu makahama akashinda hapo inakuwaje?
Ni ama anarudishwa kazini na kulipwa mishahara yake yote aliyonyimwa, ama mahakama inapendekeza mchakato ufanywe upya kwa kufuata taratibu za kisheria.
 
Ni ama anarudishwa kazini na kulipwa mishahara yake yote aliyonyimwa, ama mahakama inapendekeza mchakato ufanywe upya kwa kufuata taratibu za kisheria.
Mkuu hapo si miaka kumi tena? kuna ndugu yangu nafuatilia issue yake pale tume tu imekula miaka 3 halafu iende kwa Rais miaka mingine 3 mwishoni mahakamani 4 hahaha
 
Mahakama ya Rufaa imejiongoza vibaya kutafsiri hivyo vifungu. Nina imani muda sio mrefu watafanya marejeo au watatoa hukumu nyingine itayorekebisha maamuzi waliyotoa katika Rufaa hii.

Discplinary Matters ni sahihi kupitia mchakato wa ndani kabla ya kwenda CMA au Mahakama Kuu kwa Judicial Review lakini sio sahihi kwa migogoro (disputes) isiyo ya kinidhamu, hii inatakiwa kwenda moja kwa moja CMA maana hakuna sheria inayoelekeza kuwa ishughulikiwe ndani ya taasisi husika au kwamba iende huko Tume ya utumishi wa umma nk. Tume ya utumishi wa umma uwezo wake ni kupokea Rufaa na sio kupokea migogoro iliyo fresh
Swali Mtaalam: Hivi MTU akienda CMA ikamkandamiza mtumishi halafu akaona kaonewa anakwenda wapi baada ya CMA?
 
MAHAKAMA YA RUFANI: CMA HAINA MAMLAKA WAFANYAKAZI WA UMMA

Mahakama ya Rufani ya Tanzania imesema Tume ya Usuluhishi ya wafanyakazi (Commission for Mediation and Arbitration-CMA) haina mamlaka ya kusikiliza na kutolea maamuzi kesi zinazohusu migogoro ya wafanyakazi wa umma.

Kupitia kesi ya rufaa ya madai CIVIL APPEAL NO. 12 OF 2022 TANZANIA POSTS CORPORATION VERSUS DOMINIC A. KALANGI mahakama hiyo ya juu zaidi ya Tanzania imesema migogoro ya wafanyakazi wa umma inatakiwa kuishia ndani ya Serikali, pale mfanyakazi anapofukuzwa kazi na mkuu wa idara au shirika la Serikali anatakiwa kukata Rufaa kwenda Tume ya Utumishi wa Umma, na endapo mfanyakazi atakuwa hajaridhika na maamuzi ya Tume ya Utumishi wa Umma basi anatakiwa akate rufaa kwenda Kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na maamuzi ya Rais yatakuwa ya mwisho, hii ni Kwa mujibu wa Kifungu Cha 25 Cha sheria ya utumishi wa umma Public Service Act (Cap 298 R.E. 2019)

Dominic A. Kalangi alikuwa mfanyakazi wa Shirika la Posta (Tanzania Posts Corporation), mwaka 2017 ajira yake ilisitishwa Kwa utovu wa nidhamu.

Dominic alipeleka malalamiko yake CMA ambapo alishindwa kesi akakata Rufaa Mahakama kuu Mtwara ambapo mahakama kuu ikaamuru Shirika la Posta limlipe fidia ya mishahara ya miezi sita Dominic A kalangi. Shirika la Posta likakata Rufaa Mahakama ya Rufani ya Tanzania

Kwa Mujibu wa sheria Shirika la Posta la Tanzania ni Mali ya umma linalomilikiwa na serikali hivyo wafanyakazi wake ni watumishi wa umma.

"Going by the wording of the above-quoted provision, it is unambiguously clear that all disciplinary matters or disputes involving public servants are exclusively within the domain of the Public Service Commission whose decision is appelable to the President. As correctly submitted by Ms. Kinyasi and as amply demonstrated above, the CMA has no jurisdiction to adjudicate upon such matters."

View attachment 2175700View attachment 2175702
Kumbe bado tuna sheria nyingi za ajabu ajabu zinazokwenda kinyume cha katiba!.
Hili tutasaidia.
P
 
Kumbe bado tuna sheria nyingi za ajabu ajabu zinazokwenda kinyume cha katiba!.
Hili tutasaidia.
P
Njoo uunge mkono katika hili, tayari mwezi Mei 2022 tumefungua maombi ya REVIEW ya hukumu hiyo pale Mahakama ya Rufani (Dar es Salaam) tukiomba hukumu hii kandamizi ibatilishwe kwa kuwa ni batili na yenye makosa kisheria yanayopelekea miscarriage of justice. Njoo uongeze nguvu tupate hearing ya mapema
 
Back
Top Bottom