Bush Dokta
JF-Expert Member
- Apr 11, 2023
- 24,831
- 45,154
Hahahahaa......Mambo mengine inabidi tucheke tu hata kama yanahuzunisha.
Utangulizi
Marekani ina Majimbo 50 na jumla ya Wananchi( raia) wapatao Milioni 330+ kwa mujibu wa Takwimu za 2022.
Tanzania ina wananchi wapatao Milioni 65+ kwa mujibu wa Takwimu za 2022.
Wakati Marekani ina idadi ya Raia inayozidi ya Tanzania zaidi ya mara tano sisi Tanzania tuna idadi ya Majaji takribani mara nne ya ile ya marekani.
Tafakuli:
Wakati Nchi yetu kwa sehemu kubwa inaongozwa na bajeti inayotegemea mikopo kuhudumia wananchi na sehemu kadhaa ya kodi zinazokusanywa itakushangaza kuwa Tuna idadi kubwa ya Wateule na vigogo wa serikali wanaohudumiwa kila kitu kwa pesa hizo hizo za Kasungura kadogo.
Ikumbukwe kwa mujibu wa Sheria inayosimamia maslahi ya Watumishi wa Umma majaji ni miongoni mwa wanaolipwa na kuhudumiwa kifahari kutokana na hadhi yao pamoja na kuwa na mishahara minono.
Sasa tujiulize kwanini sisi wenye maeneeleo kidogo tunaonekana kuwa na matumizi makubwa wakati Nchi zenye watu wengi na shuguuli nyingi zikiwa na matumizi yakawaida na kuacha sehemu ya mapato yao yahudumie wananchi? Sisi tunakwamba wapi?
Ikumbukwe hapa tumeangalia sehemu ndogo tu ktk sekta hii ya watumishi wa Umma
Fikiria matumizi yakoje ktk ofisi zifuatazo
1. Ikulu
2. Ofisi ya waziri Mkuu
3. Ofisi ya Spika wa bunge
4. Ofisi ya DGIS
5. Ofisi ya CDF
6. Ofisi ya Makamu wa Rais
7. Ofisi ya IGP
8. Ofisi ya Takukuru
Hata tungekopa kiasi gani, hata wananchi walipe kodi kiasi gani tunadhani zitatosha?
Mapendekezo:
Chama cha mapinduzi kiangalie upya namna bora ya kusuka na kuunda serikali ili kulinda na kuweka akiba kwa ajili ya kutoa huduma bora kwa Wananchi badala ya kuwa na matumizi makubwa kwa watu wachache tu Mwisho wa siku tuko mwaka wa 60 madarakani bado changamoto za maendeleo na ustawi wa raia ziko pale pale.
Na nyie viongozi na vigogo mnaokula Jasho letu basi kuweni na huruma hata kidogo basi.
Nawatakia utumishi mwema na uchapa kazi watumishi wote wa umma waadilifu kwa Ajili ya Mama Tanzania.
========
Ufafanuzi juu ya Mfumo wa Mahakama nchini
Mfumo wa Mahakama wa Tanzania una Mahakama ya Mwanzo (Primary Court), Mahakama ya Wilaya (District Court), Mahakama ya Hakimu Mkazi (Resident Magistrate's Court), Mahakam Kuu (High Court) na (Mahakama ya Rufani (Court of Appeal), hii inamaanisha kuna Mahakama za aina 5 na mahakama ya Rufani ndio ya daraja kubwa kabisa, kwamba ukifika mahakama hiyo maamuzi yao ndio ya mwisho kwa Tanzania
Mahakama ya Rufani Tanzania ina Majaji 31 na Marekani ina majaji 179 na kwenye upande wa Supreme Court ndio ina Majaji 9.
Kenya wana mfumo wa Supreme Court ambayo ina Majaji 7, na hii ni baada ya kufanya mabadiliko kwenye katiba yao mwaka 2010 baada ya vurugu za uchaguzi. Mahakama hii Kenya kwa kiasi kikubwa ni kwaajili ya kusikiza kesi za Uchaguzi kwenye nafasi ya Urais.
Uganda pia wana Supreme Court, ambako wao wana Majaji 10, na kwao pia Mahakama hii kwa kiasi kikubwa inasikiliza kesi zinazohusu Uchaguzi wa Urais.
Ili kuwa na Supreme Court nchini Tanzania inabidi mabadiliko yafanyike kwenye Katiba kwasababu Mfumo wa Mahakama unatengenezwa kutokana na Katiba.