Mahakama ya Ubelgiji yasema jino la shujaa Lumumba wa DRC linapaswa kurudishwa

Mahakama ya Ubelgiji yasema jino la shujaa Lumumba wa DRC linapaswa kurudishwa

MakinikiA

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2017
Posts
5,104
Reaction score
6,827
Patrice Lumumba aliuawa 1961

Patrice Lumumba aliuawa 1961
Mahakama mjini Ubelgiji imeamuru kwamba jino lililochukuliwa kutoka kwa maiti ya shujaa wa Uhuru wa taifa la DRC wakati huo ikiitwa Congo Patrice Lumumba linapaswa kurejeshwa kwa familia yao, vyombo vya habari nchini Ubelgiji vimeripoti.

Lumumba aliyekuwa waziri mkuu wa Congo baada ya kujipatia Uhuru kutoka kwa Ubelgiji 1960, aliuawa 1961 baada ya kutekwa na wapiganaji waliotaka kujitenga.

Serikali ya Ubelgiji ilihusika katika kifo chake na mwaka 2002 iliomba msamaha rasmi. Vitengo vya ujasusi vya Uingereza na Marekani pia vinadaiwa kuhusika.

Jino la Lumumbua linadaiwa kuchukuliwa na afisa wa polisi wa Ubelgiji aliyekuwa anasaidia kuuzika mwili wake , chombo cha habari cha AFP kimeripoti.

Baadaye jino hilo lilichukuliwa na mamlaka ya Ubelgiji , AFP kinaongezea. Mahakama hiyo ya Ubelgiji ilisema kwamba jino hilo sasa linafaa kupewa mwana wa kike wa Lumumba Juliana Lumumba , ambaye aliandika barua kwa mfalme huyo wa Ubelgiji akiomba lirudishwe, mtandao wa Brussels Times uliripoti.

Kulingana na mtandao huo uamuzi huo wa mahakama siku ya Alhamisi unafuatia uamuzi mwengine wa ofisi ya kiongozoi wa mashtaka wa kijimbo kwamba mabaki ya Lumumba yanaweza kurudishwa kwa familia yake,

:Wajerumani walijaribu kuchukua fuvu la Mkwawa wakalishindwa wakaamua kulirudisha Iringa
 
Mahakama mjini Ubelgiji imeamuru kwamba jino lililochukuliwa kutoka kwa maiti ya shujaa wa Uhuru wa taifa la DRC wakati huo ikiitwa Congo Patrice Lumumba linapaswa kurejeshwa kwa familia yao, vyombo vya habari nchini Ubelgiji vimeripoti.

Lumumba aliyekuwa waziri mkuu wa Congo baada ya kujipatia Uhuru kutoka kwa Ubelgiji 1960, aliuawa 1961 baada ya kutekwa na wapiganaji waliotaka kujitenga.

Serikali ya Ubelgiji ilihusika katika kifo chake na mwaka 2002 iliomba msamaha rasmi.

Vitengo vya ujasusi vya Uingereza na Marekani pia vinadaiwa kuhusika.

Jino la Lumumba linadaiwa kuchukuliwa na afisa wa polisi wa Ubelgiji aliyekuwa anasaidia kuuzika mwili wake , chombo cha habari cha AFP kimeripoti.

Baadaye jino hilo lilichukuliwa na mamlaka ya Ubelgiji , AFP kinaongezea.

Mahakama hiyo ya Ubelgiji ilisema kwamba jino hilo sasa linafaa kupewa mwana wa kike wa Lumumba Juliana Lumumba , ambaye aliandika barua kwa mfalme huyo wa Ubelgiji akiomba lirudishwe, mtandao wa Brussels Times uliripoti.

Kulingana na mtandao huo uamuzi huo wa mahakama siku ya Alhamisi unafuatia uamuzi mwengine wa ofisi ya kiongozoi wa mashtaka wa kijimbo kwamba mabaki ya Lumumba yanaweza kurudishwa kwa familia yake,
 
Yani wamekiri kua wameshiriki kutoa uhai wa mtu halafu wanakuja na jino moja why?

Hayo meno mengine ya watu walioshiriki kumuua lumumba yako wapi?
Jino ni la Lumumba na lilichukuliwa na askari wakati wa mazishi yake
 
Yaani waanze kurudisha jino halafu mabaki ya mwili wanafikiria lini watarudisha, lol
 
Nacho maanisha kwanini tumekua wepesi kuridhika na kuwasamehe kirahisi kwa unyama waliokiri kuufanya?

Vipi ingekua ni sisi tumemuua legend wao unafikiri kukiri kwetu kosa kungetosha kufanya wao waridhike?
Wangetaka fidia mkuu ila ndio hivyo mwenye pesa hakosei 🙆
 
Nacho maanisha kwanini tumekua wepesi kuridhika na kuwasamehe kirahisi kwa unyama waliokiri kuufanya?

Vipi ingekua ni sisi tumemuua legend wao unafikiri kukiri kwetu kosa kungetosha kufanya wao waridhike?
Ooh ok ok nimekupata vema sasa
 
Alafu hao wauaji wa ubelgiji ndiyo ngome ya Lisu!!

Yani Lisu anaturudisha miaka ya 1961 leo.
 
Wazungu kwa sifa, maisha ya mweusi hayana thamani, askari anajiweka ukumbusho (souvenir).
Serikali ya ubelgiji walilipa kiasi gani na kwa nani baada ya kukiri mauaji?
 
Lije tu kwa kweli jino la Limumba wenyewe tuna kazi nalo 😂😂😂
 
Wazungu nao bhana sasa hilo jino walienda kufanyia nini!
 
Warudishe madini waliyoiba na uhai wa watu walioupoteza sio jino, sasa anarudisha jino mwili wa Mwenye jino haujulikani ulipo.
 
Wazungu nao bhana sasa hilo jino walienda kufanyia nini!
Walienda kulitambikia ili kuwaloga wakongo kila siku wawe wanaumana, sio unaona wanaumana kila siku vita haziishi😂😂😂😂😂😂😂😂😂

Utan tu. Ila ata kwa mzungu napo kuna ushirikina
 
Back
Top Bottom