Mahakama ya Uhujumu Uchumi: Mvutano mkali kesi ya Mbowe na wenzake. Hatma ya kesi kujulikana Septemba 6

Kama ni kweli usemavyo nasimama na Mh Mbowe Acha Mungu atende vile apendavyo kwani imeandikwa "Usimshuhudie Jirani yako Uongo"
 
Mahakama zetu bado hazijaondokana na ukoloni wa Lugha ya kizungu, sijui nani tena atakuja kuuondoa huu ukoloni ambao kimsingi umekuwa kama "ulaji" kwa wanao kitumikia na kukiabudu kizungu.
sielewi kwa nn wananchi ktk nchi yao wawe wafungwa ktk kutumia lugha yao ya kiswahili na ionekane lugha ya kiingereza ndiyo yenye thamani zaidi mbele ya wananchi ambao Taifa liko huru?!!
 
Dar es Salaam.
Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi Jumatatu tarehe 6, Septemba 2021, inatarajiwa kutoa uamuzi wa pingamizi la mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu wanaokabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi na Ugaidi.

Mbowe na wenzake wanapinga hati ya mashtaka yanayowakabili wakidai kuwa ina kasoro za kisheria na hivyo wanaiomba Mahakama hiyo iitupilie mbali

Katika pingamizi hilo pamoja na mambo mengine wakidai kuwa Sheria ya Ugaidi ambayo wanashtakiwa nayo haijafafanua viambato vya kosa la Ugaidi na kwamba upande wa mashtaka haujazingatia masharti ya lazima ya sheria hiyo ambayo ni kueleza kusudio la vitendo vya ugaidi ambavyo washtakiwa wanatuhumiwa kuvitenda

Hata hivyo mawakili wa Serikali wanaoongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi Robert Kidando, wamepinga vikali pingamizi hilo wakidai kuwa hoja zao hazina mashiko.

Wamedai kuwa hati ya mashtaka iko sahihi na haina kasoro hizo zinazodaiwa na kwamba hati ya mashtaka imekidhi matakwa ya kisheria, ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa ambazo zinawawezesha washtakiwa kufahamu makosa wanayoshtakiwa.

Hivyo, wameiomba mahakama ilitupilie mbali pingamizi hilo ili kesi hiyo iendelee kusikilizwa katika hatua ya awali.

Baada ya kusikiliza hoja za pande zote Jaji Ekinaza Luvanda amesema atatoa uamuzi wa pingamizi hilo la washtakiwa Jumatatu.

Serikali inawakilishwa na timu ya mawakili wa Serikali watano huku upande wa utetezi ukiwa na mawakili zaidi ya 14 wakiongozwa na Peter Kibatala.

Washtakiwa wa kwanza Halfan Bwire Hassan, wa pili Adamu Hassan Kasekwa, wa tatu Mohamed Abdillahi Ling'wenya na wa nne Freeman Aikael Mbowe.

Chanzo: Mwananchi
 
Premiered 36 minutes ago
03 September 2021

KESI Namba 16 /2021 YA UGAIDI INAYOMKABILI FREEMAN MBOWE NA WENZAKE, MAHAKAMA KUTOA UAMUZI MDOGO JUMATATU

KESI YA FREEMAN MBOWE NA WENZAKE, MAHAKAMA KUTOA UAMUZI JUMATATU Ijayo September 6, 2021 ambapo Mahakama Kuu itatoa uamuzi mdogo juu ya pingamizi la upande wa utetezi kuhusu yaliyoandikwa katika hati ya mashtaka iliyowasilishwa na mwendesha mashtaka wa serikali.
Source : Global TV Online
 
Haya mambo ya kisheria ni lazima yaendeshwe kisheria, otherwise itakuwa rahisi tu kuwashtaki watu hata kama shtaka lao halistahili au halina uzito kisheria. Kwa hiyo, ni vizuri toka mwanzoni mambo yaonekane yakienda au yakiendelea kwa kufuata utaratibu wa kisheria.
 
ngoja wadhalilike kwanza
Mungu ibariki CHADEMA

Sent from my Infinix X692 using JamiiForums mobile app
Siku zote Mahakama huwa inahitaji ushahidi, na kama matendo yalifanyika kwa siri kama bwana ndugu unavyosema hatima yake ni nini. Na siku zote kesi yakutengeneza huwa ni ngumu sana hususani unapokutana na Mwamba anayeijuwa sheria na anaipenda kazi yake kindakindaki
 
"Mkiwa na mawazo yanayofanana ni kikao tayari"
Mawakili Mungu anawaona.
 
"Eti mkiwa na mawazo yanayofanana basi ni Kikao" Kweli wamedhamilia kuifuta hii case
 
"Mkiwa na mawazo yanayofanana ni kikao tayari"
Mawakili Mungu anawaona.
Hawa mawakili upande wa serikali / Jamhuri wanatoka North Korea wakatua Tanzania wakati wa mwendazake ambapo kuota ni kosa kubwa pia.
 
Kiswahili kina mapungufu mengi sana hakiendani na sayansi na teknolojia
 
Kama ni kweli usemavyo nasimama na Mh Mbowe Acha Mungu atende vile apendavyo kwani imeandikwa "Usimshuhudie Jirani yako Uongo"
Amina. Wataumbuka tu. Katiba Mpya ndio kosa la Mbowe.

Sasa akirudi mtaani si ndio moto wa katiba mpya utanoga? maana hawakumkamata kwa sababu ya katiba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…