The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Mjane mmoja aliyejulikana kwa jina la Beatrice Lyimo, mkazi wa Mbezi Makabe, jijini Dar es Salaam, yupo kwenye maumivu makali baada ya mahakama kutoa uamuzi kuwa nyumba yake ipigwe mnada mnamo Machi 10, mwaka huu, ili alipwe fidia abiria aliyekuwa amebebwa na bodaboda kugongwa na gari lililokuwa likiendeshwa na marehemu mumewe, na kusababisha abiria huyo kuvunjika mguu.
Akizungumza na Global TV Online, mjane huyo alisema kuwa baada ya ajali hiyo kutokea maeneo ya Mbezi Magufuli, mumewe alijitolea kuwapeleka hospitali dereva wa bodaboda na abiria, lakini abiria huyo alikataa na kusema kuwa atapelekwa na ndugu zake.
Hata hivyo, mumewe aliendelea kumhudumia dereva wa bodaboda hadi akapona.
Baadaye, walipokea wito kutoka kwa abiria aliyekuwa kwenye bodaboda, na alipokwenda kumuona alimlaumu kwa kutomfuatilia tena.
Mumewe alimueleza kuwa alimwomba kumtibu lakini alikataa, hivyo alidhani kuwa hakuhitaji msaada wake.
Abiria huyo akaomba alipwe shilingi milioni tano, lakini mumewe alikataa na badala yake alipokea barua kutoka kwa mwanasheria wa abiria huyo, akimtaka kulipa fidia ya shilingi milioni 200.
Mumewe aliomba suala hilo liende mahakamani. Shauri lilipofikishwa mahakamani, washtaki hawakufika siku ya kwanza, lakini mumewe alienda.
Kwa bahati mbaya, alipokuwa akirudi nyumbani, alipata ajali mbaya maeneo ya Mbezi Kibanda cha Mkaa na kufariki dunia.
Hivyo, walimuomba mjane huyo kuendelea na kesi, na hatimaye ikaamuliwa kuwa nyumba yake iuzwe kwa thamani ya shilingi milioni 35 ili alipwe fidia ya shilingi milioni 24 kwa abiria aliyekuja kuvunjika mguu, pamoja na shilingi milioni 10 za usumbufu.
Jambo hili linamuumiza sana mjane huyo kwani hana kazi, mumewe amefariki, na pia ana watoto wadogo.