Mahakama yaamuru kupigwa mnada nyumba ya mjane ili kumfidia aliyeumia mguu kwa ajali ya bodaboda

Mjane mmoja aliyejulikana kwa jina la Beatrice Lyimo, mkazi wa Mbezi Makabe, jijini Dar es Salaam, yupo kwenye maumivu makali baada ya mahakama kutoa uamuzi kuwa nyumba yake ipigwe mnada mnamo Machi 10, mwaka huu, ili alipwe fidia abiria aliyekuwa amebebwa na bodaboda kugongwa na gari lililokuwa likiendeshwa na marehemu mumewe, na kusababisha abiria huyo kuvunjika mguu.

Akizungumza na Global TV Online, mjane huyo alisema kuwa baada ya ajali hiyo kutokea maeneo ya Mbezi Magufuli, mumewe alijitolea kuwapeleka hospitali dereva wa bodaboda na abiria, lakini abiria huyo alikataa na kusema kuwa atapelekwa na ndugu zake.

Hata hivyo, mumewe aliendelea kumhudumia dereva wa bodaboda hadi akapona.

Baadaye, walipokea wito kutoka kwa abiria aliyekuwa kwenye bodaboda, na alipokwenda kumuona alimlaumu kwa kutomfuatilia tena.

Mumewe alimueleza kuwa alimwomba kumtibu lakini alikataa, hivyo alidhani kuwa hakuhitaji msaada wake.

Abiria huyo akaomba alipwe shilingi milioni tano, lakini mumewe alikataa na badala yake alipokea barua kutoka kwa mwanasheria wa abiria huyo, akimtaka kulipa fidia ya shilingi milioni 200.

Mumewe aliomba suala hilo liende mahakamani. Shauri lilipofikishwa mahakamani, washtaki hawakufika siku ya kwanza, lakini mumewe alienda.

Kwa bahati mbaya, alipokuwa akirudi nyumbani, alipata ajali mbaya maeneo ya Mbezi Kibanda cha Mkaa na kufariki dunia.

Hivyo, walimuomba mjane huyo kuendelea na kesi, na hatimaye ikaamuliwa kuwa nyumba yake iuzwe kwa thamani ya shilingi milioni 35 ili alipwe fidia ya shilingi milioni 24 kwa abiria aliyekuja kuvunjika mguu, pamoja na shilingi milioni 10 za usumbufu.

Jambo hili linamuumiza sana mjane huyo kwani hana kazi, mumewe amefariki, na pia ana watoto wadogo.

View attachment 3252053
Mcingo mrefu huuuu

Mama nenda kwa mama Samia sheria wakusaidie

Hiloo game ndefu kuanzia toa hukumu
 
Sio mjuzi wa sheria kabisa, lakini, Pana hujuma hapo, malipo ya ajali hufanywa na bima ambayo huwepo kwenye chombo cha moto, kibaya nadhani huyo aliyegongwa ni mchawi mbaya Sana, hilo ni game!, inachezwa na mahakama, na wapuuzi katika kudhulumu.
Serekali izuie ujinga huu.
Ngoja ntawapa mrejesho..Nina kesi Kama hii polisi sijafuatilia Mimi nikiwa mshitaki ngoja nianze kuifuatilia ntakupa mrejesho.
 
Hii kesi na maamuzi yake ni ya kimagumashi sana.

1. Gari haikuwa na bima ?
2. Deni la marehemu linakwendaje kufidiwa na mjane?
3. Kwanini huyo mhanga alikataa kusaidiwa na marehemu kwa gharama za marehemu akiwa hai then aje kumfungulia mashitaka baadae akidai fidia?
Mpwa HAPO KUNA watu wamehaidiwa mshiko ndioo maana ......mama APATE MWANASHERIA MZURI hakimu atajuta hio hukumu
 
Kama huyo mtu alikatwa mguu, basi apewe hela zake kama fidia.
Kinachosikitisha hapo ni neno 'mjane' lakini haki imetendeka.
Ephen Jana jion nilikua natembea..mguu kwenye maungio ukawa unauma Sana.
Kuna siku nakua normal kabisa

Najua siwezi kua na mguu MZIMA Kama zamani..nilipata Maumivu Zaid nimejitibu mwenyewe/ nikakumbuka siku alie nigonga kuomba nikamsaidie kutoa leseni yake nikamjibu USHAWAI KUJA KUNIONA UNAJUA NAENDELEAJE? HAKUJIBU SIITAJI CHOCHOTE TOKA KWAKE NGOJA NIMFANYIE USUMBUFU WA KISHERIA. NTAKUJA KUWAPA MREJESHO.
 
Serikali ikishakuwa legelege mambo kama haya yanakuwa mengi sana

Gali Ina bima na bodaboda Ina bima kwanini asilipwe na bima

Alafu na huyo mke alifuata Nini mahakani kwani kesi inarithiwa
Umeona bima?
 
Mpwa HAPO KUNA watu wamehaidiwa mshiko ndioo maana ......mama APATE MWANASHERIA MZURI hakimu atajuta hio hukumu
Hakimu hawezi kujuta maana kesi haukumu kwa matakwa yake bali kwa uzito wa evidences

Ila hii kesi imekaaje kaaje
 
Ephen Jana jion nilikua natembea..mguu kwenye maungio ukawa unauma Sana.
Kuna siku nakua normal kabisa

Najua siwezi kua na mguu MZIMA Kama zamani..nilipata Maumivu Zaid nimejitibu mwenyewe/ nikakumbuka siku alie nigonga kuomba nikamsaidie kutoa leseni yake nikamjibu USHAWAI KUJA KUNIONA UNAJUA NAENDELEAJE? HAKUJIBU SIITAJI CHOCHOTE TOKA KWAKE NGOJA NIMFANYIE USUMBUFU WA KISHERIA. NTAKUJA KUWAPA MREJESHO.
Watu hujijali wao tu! Usikute huyo mgonjwa alifanyiwa kama wewe ila huyu mama anashikilia bango kitu 'mjane' vyema tungesikia upande wa mgonjwa pia.
 
Akikata rufaa anaweza kushinda asubuhi tu kabla ya dada wa kazi hajatenga chai ya boss wake ili aende kazini.
 
Mjane mmoja aliyejulikana kwa jina la Beatrice Lyimo, mkazi wa Mbezi Makabe, jijini Dar es Salaam, yupo kwenye maumivu makali baada ya mahakama kutoa uamuzi kuwa nyumba yake ipigwe mnada mnamo Machi 10, mwaka huu, ili alipwe fidia abiria aliyekuwa amebebwa na bodaboda kugongwa na gari lililokuwa likiendeshwa na marehemu mumewe, na kusababisha abiria huyo kuvunjika mguu.

Akizungumza na Global TV Online, mjane huyo alisema kuwa baada ya ajali hiyo kutokea maeneo ya Mbezi Magufuli, mumewe alijitolea kuwapeleka hospitali dereva wa bodaboda na abiria, lakini abiria huyo alikataa na kusema kuwa atapelekwa na ndugu zake.

Hata hivyo, mumewe aliendelea kumhudumia dereva wa bodaboda hadi akapona.

Baadaye, walipokea wito kutoka kwa abiria aliyekuwa kwenye bodaboda, na alipokwenda kumuona alimlaumu kwa kutomfuatilia tena.

Mumewe alimueleza kuwa alimwomba kumtibu lakini alikataa, hivyo alidhani kuwa hakuhitaji msaada wake.

Abiria huyo akaomba alipwe shilingi milioni tano, lakini mumewe alikataa na badala yake alipokea barua kutoka kwa mwanasheria wa abiria huyo, akimtaka kulipa fidia ya shilingi milioni 200.

Mumewe aliomba suala hilo liende mahakamani. Shauri lilipofikishwa mahakamani, washtaki hawakufika siku ya kwanza, lakini mumewe alienda.

Kwa bahati mbaya, alipokuwa akirudi nyumbani, alipata ajali mbaya maeneo ya Mbezi Kibanda cha Mkaa na kufariki dunia.

Hivyo, walimuomba mjane huyo kuendelea na kesi, na hatimaye ikaamuliwa kuwa nyumba yake iuzwe kwa thamani ya shilingi milioni 35 ili alipwe fidia ya shilingi milioni 24 kwa abiria aliyekuja kuvunjika mguu, pamoja na shilingi milioni 10 za usumbufu.

Jambo hili linamuumiza sana mjane huyo kwani hana kazi, mumewe amefariki, na pia ana watoto wadogo.

View attachment 3252053
NAKUPA hii CODE UKIGUNDUA UMEGONGA UMMALIZIE KABISA AKIFA FINE HAIZIDI LAKI TANO TU.... au Kwa kuwa huyo dada mchaga atafute namna ammalizie mtafutie Binti huyo mdaiwa Kisha ale naye njama ili ammalizie tu ACHANA NA HURUMA HURUMA NA KUWAZA MTU MSAADA MDOGO HATAKI ANALETA MANJEGEKA
 
Watu hujijali wao tu! Usikute huyo mgonjwa alifanyiwa kama wewe ila huyu mama anashikilia bango kitu 'mjane' vyema tungesikia upande wa mgonjwa pia.
Mbaya zaidi Niki itaji wakili natoka nae tumbo moja toka ntoke.

Alinambia atanipa wakili bureeee. maana huwezi kusimamiwa na wakili ambae ni ndugu/ mnatoka ukoo mmoja.

Nilipanga hili swala niliache ivi hivi Ila ngoja nimpe usumbufu wa kesi mahakamani

Ntatoa mrejesho
 
NAKUPA hii CODE UKIGUNDUA UMEGONGA UMMALIZIE KABISA AKIFA FINE HAIZIDI LAKI TANO TU.... au Kwa kuwa huyo dada mchaga atafute namna ammalizie mtafutie Binti huyo mdaiwa Kisha ale naye njama ili ammalizie tu ACHANA NA HURUMA HURUMA NA KUWAZA MTU MSAADA MDOGO HATAKI ANALETA MANJEGEKA
Mzee naona umeweka roho ya ki CAPITALISTS..

Sisi Nyerere alituzoesha kwa miaka 34 na UJAMAA DOCTRINE 😊😊

Yaani SOCIALISM imetuganda wa TANGANYIKA.
 
Yaaan ku
Napajua sana mkuu.
likuwa na MIRATHI ya watoto WA baba yetu mkubwa baba ndogo akataka kucheza na MALIZAKO na niwakubwaaa

Akaipeleka kesi Moshi akatengeneza cheti cha kifo kafia Moshi kazikiwa moshi wakati kafia dar na kaazikwa dar

Akaandika UPUUZI wake kwenye mgao weweee kumbe alikula Dili na watoto WA kamboo wapate malizaidi then wauze wampe mgao

Hahahaaaa tuliwmondoa hakimu mkuu ACHA kabisa anaitwa

Tulipokuja na MWANASHERIA KUWATETEA akawa ANAKULA helà za mzee akimtia moyo tukanusaa nenda Rudi nenda Rudi ukatumwa BARUA huko juu weweee

Jamaa akambiwa kaa PEMBEN watu wAfanye kazi zao Yuko sunbawanga kwa sasa

Wakamtoa kama msimamizi na sasa wanamalizika ngwe ya kugawana sawa wote

YAAN hizi mahakama ykichexa nazo unalia
 
Marehemu inaonekana alikuwa mwendeshaji wa hivyo asiyefuata sheria za barabara kwa sababu kilichomuua ni ajali. Mama akate rufaa
 
Back
Top Bottom