Mahakama yaamuru Polisi kuwatafuta viongozi wa BAVICHA (kina Deusdedith Soka) waliopotea

Mahakama yaamuru Polisi kuwatafuta viongozi wa BAVICHA (kina Deusdedith Soka) waliopotea

Gemini AI

Member
Joined
May 8, 2024
Posts
91
Reaction score
265
Jaji Wilson Dyansobera kutoka Mahakama kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam amesema baada ya Mahakama kusikiliza hoja za pande zote mbili (2) na kupitia kwa makini kiapo cha mwombaji aitwaye Mohammed H. Zimu ambaye ni rafiki wa karibu wa Deusdedith Soka na wenzake wawili (2) imejiridhisha kwamba waombaji hawapo chini ya Jeshi la Polisi.

Akitoa maamuzi hayo leo, Junatano Agosti 28.2024 Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam Jaji Dyansobera amesema, "hakuna malezo yanayotoka kwa muombaji kwamba alishuhdia waombaji wakiwa wanashikiliwa na Polisi au kuwa kizuizini”.

Katika maelezo yake Jaji Dyansobera ameeleza kuwa inawezekana muapaji alishuhudia wakikamatwa lakini hakuna ushahidi ya kuwa Soka na wenzake wapo kizuizini (detained) au wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kituo cha Chang’ombe, Dar es Salaam.

Pia Soma:
Katika hatua nyingine, Jaji Dyansobera ameliagiza Jeshi la Polisi nchini kufanya uchunguzi ili kufahamu wako wapi Soka pamoja na wenzake huku akisisitiza ni wajibu kwa Jeshi hilo, pia ni matakwa ya sheria za kimataifa kwa chombo hicho cha usalama kufuatilia na kufahamu wako wapi raia ambao wamepotea"

Mahakama inatoa amri kwa Polisi hasa mjibu maombi wa kwanza, mjibu maombi wa pili, mjibu maombi watatu, mjibu maombi wanne, na mjibu maombi watano kuchunguza uwepo wa hawa waombaji wako wapi” -Jaji Dyansobera.

JAMBO TV
 
kuliko wanavyomtesa bora wamuue aondokane na mateso ya washenzi wa ulimwengu arudi kwa Mola wake.
haki kupitia matendo maovu ya walimwengu huwa nina imani na adhabu kali siku tutayokutana na Muumba.
 
Hii nchi buana kama una hasira kama za watalbani unaweza kuchukua maamuzi magumu kwa Mahakama kuu au Bunge kwa upuuzi wanaofanya.

Yaani Mahakama inatoa statement ya kipuuzi namna hiyo? Soka Simu yake ilikuwa inashikiliwa na polisi kwa muda mrefu sana halafu alivyokamatwa Simu hiyo hiyo ya Soka ikatuma meseji kwamba wasimtafute yeye yupo salama, ina maana hiyo simu ambayo wanaishikilia polisi mpaka leo walikabidhiwa WATEKAJI? Watekaji waliomteka Soka ndiyo hao hao waliomteka SATIVA, na sativa alivyotekwa alipelekwa Oysterbay...Raia anaweza kuteka mtu akaenda naye kumtesa Oysterbay polisi karakana?
 
Bwana Mbowe ameshatoa ushahidi kwa nini hamutaki kufuatilia ukweli vijana waachiwe hapo ngome ya mabanzi.
 
Mahakama Kuu Dar es Salaam, imeliamuru Jeshi la Polisi kufanya upelelezi kujua mahali walipo viongozi wa Baraza la Vijana Chadema (Bavicha) Wilaya ya Temeke wanaodaiwa kupotea.

Maamuzi hayo yametolewa leo Jumatano Agosti 28, 2024.

Pia soma: Wakili Madeleka: Tuna ushahidi unaojaa fuso mbili polisi kuhusika kumkamata Soka

Pia imesema hakuna ushahidi kwamba viongozi wa Baraza la Vijana Chadema (Bavicha) Wilaya ya Temeke kuwa wanashikiliwa na jeshi hilo.

Pia soma: Watu Wasiojulikana: Malisa aelezea tukio la kutekwa kwa Deus Soka na vijana wengine wawili wa CHADEMA

Viongozi hao wa Bavicha ni Mwenyekiti wa Wilaya ya Temeke, Deusdedith Soka na Katibu wake, Jacob Mlay pamoja dereva wao wa pikipiki, Frank Mbise, ambao wanadaiwa kukamatwa na Polisi katika kituo cha Polisi Chang'ombe, Temeke tangu Agosti 18, 2024.

CHANZO: Mwananchi
 
Hii nchi buana kama una hasira kama za watalbani unaweza kwenda kulipua Mahakama kuu au Bunge kwa upuuzi wanaofanya.

Yaani Mahakama inatoa statement ya KINGESE namna hiyo? Soka Simu yake ilikuwa inashikiliwa na polisi kwa muda mrefu sana halafu alivyokamatwa Simu hiyo hiyo ya Soka ikatuma meseji kwamba wasimtafute yeye yupo salama ,ina maana hiyo simu ambayo wanaishikilia polisi mpaka leo walikabidhiwa WATEKAJI? Watekaji waliomteka Soka ndiyo hao hao waliomteka SATIVA ,na sativa alivyotekwa alipelekwa Oysterbay...Raia anaweza kuteka mtu akaenda naye kumtesa Oysterbay polisi karakana?
Kwa kweli nchi hii inaelekea kubaya sana, Damu za wengi zinanung'unikia polccm ndio maana maisha yao yote yatabaki kuwa ya laana na majuto.
 
Tuwekeeni hukumu tuipitie maana tusilaumu kuwa Dyanso ameagizwa kuandika hivyo
 
Hii nchi buana kama una hasira kama za watalbani unaweza kwenda kulipua Mahakama kuu au Bunge kwa upuuzi wanaofanya.

Yaani Mahakama inatoa statement ya KINGESE namna hiyo? Soka Simu yake ilikuwa inashikiliwa na polisi kwa muda mrefu sana halafu alivyokamatwa Simu hiyo hiyo ya Soka ikatuma meseji kwamba wasimtafute yeye yupo salama ,ina maana hiyo simu ambayo wanaishikilia polisi mpaka leo walikabidhiwa WATEKAJI? Watekaji waliomteka Soka ndiyo hao hao waliomteka SATIVA ,na sativa alivyotekwa alipelekwa Oysterbay...Raia anaweza kuteka mtu akaenda naye kumtesa Oysterbay polisi karakana?
Mkuu ushahidi wako huu ungekuwa umeupeleka Mahakamani ungemsaidia sana Jaji kufikia maamuzi ya maana. Sasa wewe umebaki kulalamika tu bila kuisaidia Mahakama kufikia uamuzi sahihi.
 
Mkuu ushahidi wako huu ungekuwa umeupeleka Mahakamani ungemsaidia sana Jaji kufikia maamuzi ya maana. Sasa wewe umebaki kulalamika tu bila kuisaidia Mahakama kufikia uamuzi sahihi.
ulikuwa unatumia makilio kusoma hapa.ulitaka ushaidi gani kwani polisi alitakiwa kumpeleka wapi ?
 
ulikuwa unatumia makilio kusoma hapa.ulitaka ushaidi gani kwani polisi alitakiwa kumpeleka wapi ?
Shetani katika ubora wake! Niliyemquote ndio ametoa ushahidi kuwa simu ya mhusika iko na Polisi na ilitumwa sms kuwa Soka yuko salama huo ndio ushahidi ulipashwa kupelekwa mahakamani kama kweli aliyoyaandika ni ya kweli.
 
Back
Top Bottom