Mahakama yaifuta kesi ya Kabendera dhidi ya Vodacom

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
378
Reaction score
766
Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam imeifuta kesi ya mwanahabari Erick Kabendera, aliyokuwa ameifungulia kampuni ya huduma za mawasiliano ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Public Limited.

Uamuzi huo wa kuifuata kesi hiyo utolewa leo Jumanne, Septemba 10, 2024 na Naibu Msajili wa Mahakama hiyo, Livin Lyakinana kwa niaba ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Salma Maghimbi anayesikiliza kesi hiyo, kufuatia pingamizi la awali lililowekwa na Vodacom akidai kesi hiyo ni batili na ilipaswa kufunguliwa ndani ya miaka 3 tangu kutokea kwa jambo linalolalamikiwa

Katika kesi hiyo ya madai namba 12799/2024, Kabendera aliyewakilishwa na Wakili Peter Madeleka alikuwa anaituhumu Vodacom kufanikisha kukamatwa kwake na namna hiyo anayoiita kutekwa na hatimaye kufunguliwa kesi hiyo ya uhujumu uchumi.

Alikuwa anadai kutokana na tukio hilo amepata madhara mbalimbali yakiwamo ya kiuchumi na yasiyo ya kiuchumi, ya kijamii, maumivu ya kiakili na kimaono, ya kutokufurahia maisha, ya maendeleo binafsi na hadhi yake katika jamii na kutokuaminiwa kitaaluma.

Hivyo, alikuwa anaitaka kampuni hiyo imlipe Dola 10 milioni za Marekani (takribani Sh28 bilioni) kama fidia ya hasara halisi na riba kwa kiwango cha Mahakama (asilimia) kuanzia tarehe ya hukumu mpaka kumaliza malipo yote.

SOURCE; MWANANCHI

Soma pia:
=> Kesi ya kutekwa mwanahabari Kabendera, Mahakama kumaliza ubishi wa uhalali wake leo
=> Mwandishi Eric Kabendera aelezea jinsi Vodacom Tanzania ilivyomkamatisha kwa vyombo vya Usalama
=> Kesi ya Kabendera dhidi ya Vodacom yaanza rasmi leo
=> Vodacom inakanusha mtandaoni, Kabendera yuko zake mahakani
 
Hivi Madeleka kuna kesi yoyote amewahi kushinda mahakamani ? Huyu ni aina ya wakili ambae hana ethics za sheria anaweza hata ku publish nyaraka za ushahidi twitter ili apate attention tu, ila siyo wakili wa kutegemewa.
 
Ana kesi zinaendelea nchi nzima.
 
Hivi Madeleka kuna kesi yoyote amewahi kushinda mahakamani ? Huyu ni aina ya wakili ambae hana ethics za sheria anaweza hata ku publish nyaraka za ushahidi twitter ili apate attention tu, ila siyo wakili wa kutegemewa.
Kwa nini na wewe usiitafute hiyo attention kama ni mtaji? Acheni kuwaponda wenzenu kwa chuki zenu.Huyu bwana tumeona amesaidia wengi sana kudai haki zao, wewe una legacy gani so far??
 
Kamsaidia nani na kaacha legacy gani? Unajua maana ya Legacy? , huyu alieitumia familia ya Soka kujinufaisha?

Alisema anao ushahidi fuso mbili kuwa soka kakamatwa na Polisi kumbe hana ushahidi wowote nia ilikua ni kula michango ya watu, mahakamani anaambiwa leta ushahidi analeta ushahidi wa post kuwa Soka kabla hajatekwa aliandika nikipotea waulizeni polisi, sasa huo unaweza kuwa ushahidi mbele ya mahakama?
 
Anakesi nchi nzima ila hapati conviction kwasababu ni wakili mwenye mihemko mbele ya mahakama ameharibu kesi nyingi zilizonyooka kwa kukosa utulivu namfahamu vizuri sana
Kumbe mahakama hawaangalii ukweli bali mihemko?
 
Mahakama Kuu Masijala Ndogo-Dar es Salaam imeifuta kesi ya Mwandishi wa Habari za Kiuchunguzi, Erick Kabendera aliyoifungua dhidi ya Kampuni ya Vodacom akiituhumu kufanikisha kukamatwa kwake na Askari Polisi Mwaka 2019 akiwa Nyumbani kwake Mbweni na kisha kufunguliwa kesi ya Uhujumu Uchumi.
1725977086091.png
Uamuzi wa kuifuta kesi hiyo umetolewa leo Septemba 10, 2024 na Naibu Msajili wa Mahakama hiyo, Livin Lyakinana akidai kesi hiyo ni batili na ilipaswa kufunguliwa ndani ya miaka 3 tangu kutokea kwa jambo linalolalamikiwa.

Ikumbukwe, Kabendera aliishitaki Vodacom akiitaka kampuni hiyo kumlipa fidia ya Dola za Marekani Milioni 10 (takriban Tsh. Bilioni 28) akidai baada ya kukamatwa kwake alidhurika kiuchumi, kiakili pia na hasara ya kutokufurahia Maisha, kutoaminiwa kitaaluma, maendeleo binafsi na hadhi yake katika Jamii.

Alikuwa anadai kutokana na tukio hilo amepata madhara mbalimbali yakiwamo ya kiuchumi na yasiyo ya kiuchumi, ya kijamii, maumivu ya kiakili na kimaono, ya kutokufurahia maisha, ya maendeleo binafsi na hadhi yake katika jamii na kutokuaminiwa kitaaluma.

Hivyo, alikuwa anaitaka kampuni hiyo imlipe Dola 10 milioni za Marekani (takribani Sh28 bilioni) kama fidia ya hasara halisi na riba kwa kiwango cha Mahakama (asilimia) kuanzia tarehe ya hukumu mpaka kumaliza malipo yote.

Soma pia:
=> Kesi ya kutekwa mwanahabari Kabendera, Mahakama kumaliza ubishi wa uhalali wake leo
=> Mwandishi Eric Kabendera aelezea jinsi Vodacom Tanzania ilivyomkamatisha kwa vyombo vya Usalama
=> Kesi ya Kabendera dhidi ya Vodacom yaanza rasmi leo
=> Vodacom inakanusha mtandaoni, Kabendera yuko zake mahakani
 
Kamsaidia nani na kaacha legacy gani? Unajua maana ya Legacy? , huyu alieitumia familia ya Soka kujinufaisha?

Alisema anao ushahidi fuso mbili kuwa soka kakamatwa na Polisi kumbe hana ushahidi wowote nia ilikua ni kula michango ya watu, mahakamani anaambiwa leta ushahidi analeta ushahidi wa post kuwa Soka kabla hajatekwa aliandika nikipotea waulizeni polisi, sasa huo unaweza kuwa ushahidi mbele ya mahakama?
Nawashangaa sana wanaomuona mkali kweli, kumbe ni attention tuu!!! Kazi kujisifu
 
Back
Top Bottom