Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 378
- 766
Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam imeifuta kesi ya mwanahabari Erick Kabendera, aliyokuwa ameifungulia kampuni ya huduma za mawasiliano ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Public Limited.
Uamuzi huo wa kuifuata kesi hiyo utolewa leo Jumanne, Septemba 10, 2024 na Naibu Msajili wa Mahakama hiyo, Livin Lyakinana kwa niaba ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Salma Maghimbi anayesikiliza kesi hiyo, kufuatia pingamizi la awali lililowekwa na Vodacom akidai kesi hiyo ni batili na ilipaswa kufunguliwa ndani ya miaka 3 tangu kutokea kwa jambo linalolalamikiwa
Katika kesi hiyo ya madai namba 12799/2024, Kabendera aliyewakilishwa na Wakili Peter Madeleka alikuwa anaituhumu Vodacom kufanikisha kukamatwa kwake na namna hiyo anayoiita kutekwa na hatimaye kufunguliwa kesi hiyo ya uhujumu uchumi.
Alikuwa anadai kutokana na tukio hilo amepata madhara mbalimbali yakiwamo ya kiuchumi na yasiyo ya kiuchumi, ya kijamii, maumivu ya kiakili na kimaono, ya kutokufurahia maisha, ya maendeleo binafsi na hadhi yake katika jamii na kutokuaminiwa kitaaluma.
Hivyo, alikuwa anaitaka kampuni hiyo imlipe Dola 10 milioni za Marekani (takribani Sh28 bilioni) kama fidia ya hasara halisi na riba kwa kiwango cha Mahakama (asilimia) kuanzia tarehe ya hukumu mpaka kumaliza malipo yote.
SOURCE; MWANANCHI
Soma pia:
=> Kesi ya kutekwa mwanahabari Kabendera, Mahakama kumaliza ubishi wa uhalali wake leo
=> Mwandishi Eric Kabendera aelezea jinsi Vodacom Tanzania ilivyomkamatisha kwa vyombo vya Usalama
=> Kesi ya Kabendera dhidi ya Vodacom yaanza rasmi leo
=> Vodacom inakanusha mtandaoni, Kabendera yuko zake mahakani