Mahakama yaitupilia mbali kesi ya Mchungaji Mwingira

Mahakama yaitupilia mbali kesi ya Mchungaji Mwingira

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,299
pic+mwuingira.gif

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeitupilia mbali kesi ya madai iliyofunguliwa na Dk William Morris, raia wa Marekani dhidi ya mkewe Dk Phills Nyimbi na Mchungaji Josephat Mwingira.

Akisoma hukumu hiyo leo Februari 26, 2018, Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba amesema Dk Morris katika kesi hiyo ameshindwa kuthibitisha uhusiano wa kimapenzi kati ya Dk Phills na Mchungaji Mwingira.

Pia, ameshindwa kuthibitisha kuwa mtoto aliyezaliwa ni matokeo ya uhusiano wa kimapenzi kati ya Dh Phills na Mchungaji Mwingira.

Hivyo, mahakama imeitupilia mbali kesi hiyo ya madai na kusema mdai ameshindwa kuthibitisha katika kiwango kinachotakiwa kwa kesi za madai na kumta alipe gharama za kesi na gharama walizotumia wadaiwa.

Baada ya kutolewa kwa hukumu huyo Wakili Respicius Ishengoma amesema watakata rufaa kwa sababu hawajaridhika na hukumu hiyo.

Hukumu hiyo yenye kurasa 54 imesomwa leo saa nane mchana iliandaliwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mhini na kusomwa na Hakimu Simba.

Awali katika utetezi wa Dk Phills Nyimbi, aliieleza mahakama hiyo kuwa hajawahi kuwa na uhusiano na Mchungaji Josephat Mwingira.

Akiongozwa na Wakili Peter Swai kutoa ushahidi katika kesi ya madai iliyofunguliwa na aliyekuwa mumewe ambaye ni raia wa Marekani, Dk William Morris, Dk Nyimbi aliomba mwanaume huyo asilipwe kiasi cha fedha cha Sh7.5 bilioni anazodai kwa sababu hakuwa na uhusiano na Mchungaji Mwingira.

Dk Nyimbi kupitia wakili Swai aliomba Dk Morris asilipwe kiasi hicho cha fedha kwa sababu hajawahi kuwa na uhusiano na Mchungaji Mwingira na kwamba hicho anachodai si madai halali.

Desemba 28, 2011, Dk Morris na Dk Phills walifunga ndoa ya Kanisani na wakati wa uhusiano wao, Dk Phillis na Mchungaji Mwingira wanadaiwa kuingia katika uhusiano wa mapenzi na kubahatika kupata mtoto wa kiume ambaye kwa sasa ana umri wa miaka tisa.

Mlalamikaji huyo alidai kuwa alitoa taarifa katika kituo cha polisi Kibamba ambapo walimueleza kuwa suala hilo ni la uzinzi ama udhalilishaji na haliwezi kuwa la kijinai na kushauriwa kufungua kesi ya madai.

Pia, alidai kwamba, kitendo cha mke wake kuwa na uhusiano na Mwingira ni kwenda kinyume na ndoa yao halali na kwamba kitendo hicho kimeharibu mipango yake ya siku za usoni kiasi cha kumfanya apoteze hata matumaini ya kuendelea kuishi.

Vilevile, alidai kimemuaibisha na kushusha hadhi yake si tu Tanzania bali na duniani, hivyo kumsababisha ateseke kiakili na kiuchumi.

Chanzo: Mwananchi
 
Hahaha tukiwazalisha mnatushitaki, wanawake kutwa kucha kwa wachungaji tuwaombee, maji ya baraka huwa yanabaraka zake kama hizo vumilieni, na hakuna kulipwa.
 
no ease money !wakome kumezea mate sadaka !!
 
Hili shambulio lilitakiwa litoke kabla Mwingira hajaongea leo, vinginevyo ni kutapatapa.
 
Eti bana kwa sababu kamla mke wa MTU kweli acha hizo
 
Yaani alitembea na wake za watu wengi sana, na wengi walikuwa ni wake za waumini wake. Na sijui ana mashetani gani ya kuwaghiribu wake za watu.

Kibaya ni pale alipopewa kiwanja cha mamilioni ya fedha na wakili maarufu hapa Dar ili akitumie kwa manufaa ya kidini. Yeye akajifanya ni rafiki wa familia, kumbe anatembea na mke wa wakili! Wakili alipogundua mke wake analiwa na askofu alimfuata huyu Askofu akamwambia wewe Askofu feki na shetani mkubwa na kiwanja changu nachukua.

Huyu Askofu feki alikataa kuachia kiwanja, pamoja na kwamba amefanya shukurani ya punda kwa kutembea na mke wa muumini aliyempa kiwanja kwa ajili ya dini.

Wakili alienda Mahakamani bwana, lakini alishindwa kesi kwa sababu Mahakama iliona Askofu kutembea na mke wa wakili haibatilishu=i uhalali wa kiwanja kutolewa kuwa sadaka kwa ajili ya huduma ya kidini.

Makubaliano ya kutoa kiwanja hayakusema ukitembea na mke wangu nitakunyanyang'anya kiwanja. Askofu akapeta katika ushetani wake!
 
Hili shambulio lilitakiwa litoke kabla Mwingira hajaongea leo, vinginevyo ni kutapatapa.

Mkuu Acha ubaguzi. Kawaida hapa ukitoka na watu wanafungua maswali. Mara leta CV yake nk. Ndo hayo hayo Hakuna jipya. So credibility ya mtoa mada Pia hutafutwa hapa JF. So Tulia watu wafanye compare and contrast
 
Nimetulia Chief😂
 
Yaani alitembea na wake za watu wengi sana, na wengi walikuwa ni wake za waumini wake. Na sijui ana mashetani gani ya kuwaghiribu wake za watu.

Kibaya ni pale alipopewa kiwanja cha mamilioni ya fedha na wakili maarufu hapa Dar ili akitumie kwa manufaa ya kidini. Yeye akajifanya ni rafiki wa familia, kumbe anatembea na mke wa wakili! Wakili alipogundua mke wake analiwa na askofu alimfuata huyu Askofu akamwambia wewe Askofu feki na shetani mkubwa na kiwanja changu nachukua.

Huyu Askofu feki alikataa kuachia kiwanja, pamoja na kwamba amefanya shukurani ya punda kwa kutembea na mke wa muumini aliyempa kiwanja kwa ajili ya dini.

Wakili alienda Mahakamani bwana, lakini alishindwa kesi kwa sababu Mahakama iliona Askofu kutembea na mke wa wakili haibatilishu=i uhalali wa kiwanja kutolewa kuwa sadaka kwa ajili ya huduma ya kidini.

Makubaliano ya kutoa kiwanja hayakusema ukitembea na mke wangu nitakunyanyang'anya kiwanja. Askofu akapeta katika ushetani wake!
Ulimpanulia miguu ukashuhudia ? Acha habari za mitumba!!
 
Back
Top Bottom