Wakati Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wakichachamaa wakisema hawatakubali Bunge hilo kuingiliwa na mhimili wa Mahakama, Mahakama hiyo imejiweka kando na tuhuma hizo.
Msajili wa Mahakama Kuu, Amir Msumi, alipotakiwa jana na NIPASHE kuthibitisha kama Mahakama imeandika barua hiyo kwenda Ofisi ya Spika wa Bunge kuzuia suala hilo lisijadiliwe kwa kuwa kiko mahakamani, alisema yeye na wasajili wenzake hawana taarifa kuhusu kuandikwa kwa barua hiyo.
Labda unieleze hiyo barua imeandikwa na nani na lini, kama ni Jaji au Msajili nitajie jina lake ili iwe rahisi kufuatilia, lakini hadi sasa nimepekua kwenye kumbukumbu zetu sijaona barua hiyo, alisema Msumi.
Aliahidi kwamba jana angewasiliana na wenzake wa Mahakma ya Rufani kama kuna barua imeandikwa kutoka mahakama hiyo kwenda bungeni.
Nipashe