Mahakama yakana kuandika Barua kuzuia mjadala wa Tegeta Escrow Account bungeni

Mahakama yakana kuandika Barua kuzuia mjadala wa Tegeta Escrow Account bungeni

Wabunge wa upinzani walikuwa wazua kuwa kuna barua kutoka mahakamani iliyozuwia mjadala wa Escrow bungeni.

Mwenyekiti wa Bunge Mheshimiwa Azzan Zungu, amethibitisha sasa hivi bungeni kuwa hakuna barua kutoka mahakamani iliyozuwia mjadala huo au mwingine wowote ule bungeni na mjadala utakuwepo kama ilivyopangwa awali.

Hapo sasa!

hebu tuache wendawazimu,
naibu spika aliruhusu mjadala wa barua ambayo ofisi yake haijaipokea??
 
Wabunge wa upinzani walikuwa wazua kuwa kuna barua kutoka mahakamani iliyozuwia mjadala wa Escrow bungeni.

Mwenyekiti wa Bunge Mheshimiwa Azzan Zungu, amethibitisha sasa hivi bungeni kuwa hakuna barua kutoka mahakamani iliyozuwia mjadala huo au mwingine wowote ule bungeni na mjadala utakuwepo kama ilivyopangwa awali.

Hapo sasa!

FaizaFoxy;

Ukweli ni kwamba barua ya Mahakama ilishaandikwa na ilikuwa imepokelewa ofisi ya Spika. Baada ya joto kupanda kutoka kwa Wabunge wa kutokubaliana na upuuzi huo wa kutaka kulizuia Bunge kujadili hoja ya Escrow wameamua kui-withdraw hiyo barua.

Watakuwa wamepima upepo wa Bunge wakaona itakuwa soo. Kwa hiyo mama usikurupuke kuwa hakukuwa na barua. Tunajua siasa za ma-CCM za kukanusha kila kitu hata kama kipo na kinaonekana wazi. Usifikiri kuwa watu wote wanakubaliana na upuuzi wa CCM wa kulinda ufisadi. Nina hakika kuna watu ndani ya Bunge walishaiona hiyo barua na kuwatonya baadhi ya Wabunge wa upinzani.
 
Wabunge wa upinzani walikuwa wazua kuwa kuna barua kutoka mahakamani iliyozuwia mjadala wa Escrow bungeni.

Mwenyekiti wa Bunge Mheshimiwa Azzan Zungu, amethibitisha sasa hivi bungeni kuwa hakuna barua kutoka mahakamani iliyozuwia mjadala huo au mwingine wowote ule bungeni na mjadala utakuwepo kama ilivyopangwa awali.

Hapo sasa!

Majibu ya Mtoto wa mkulima ndo yaliibua hasira za wabunge... perception ikabadili hali ya hewa kila mtu akahisi kuwepo barua.

Mjadala ukiwapo, aibu yao itakuwa haisemeki... Andaa pop corn na juice ya ukwaju tu FaizaFoxy
 
Pinda jana alikuwa ndani ya ukumbi wa bunge na hakukanusha wala kukubali kuhusu barua waliyozuwa upinzani. Leo Azzan Zungu kaweka wazi hilo baada ya Machali kuliongelea tena.
Ni dhahiri basi Pinda jana alikuwa anajaribu kupima upepo, kwa kuwa tulimsikia sote 'akimuonya' Naibu Spika Ndugai kuwa awe makini na maamuzi yake, ili yasije yakaingilia uhuru wa mhimili mwingine wa mahakama.

Lakini mara tu baada ya kutoa tamko hilo alionja joto la jiwe, baada ya bunge zima, kumzomea kwa nguvu, na cha kushangaza zaidi hata wabunge wenzake wa CCM waliungana na wabunge wa ukawa, kumzomea Waziri mkuu wao!
 
Sijui kutakuwa na episode kama katika series hii Kali na YA kusisimua chini YA Sterling Tumbili na Jamba Mwizi???
 
We mwanamke huwa unatia kinyaa hata kwenye mambo ya msingi unaongea utumbo........ Jirekebishe ndugu yangu khaaaa

Mkuu usimize akili kubishana na takataka! Tutajua nani "tumbili" na "mwizi".....
 
Mkuu usimize akili kubishana na takataka! Tutajua nani "tumbili" na "mwizi".....

Inakera sana mkuu kwa issue sensitive kama hii mtu anaongea ushuzi tu.... Hili suala lina mgusa kila mtanzania bila kujali hali wa itikadi..... Anyway jamii hii ina wapuuzi wengi sana
 
Ni dhahiri basi Pinda jana alikuwa anajaribu kupima upepo, kwa kuwa tulimsikia sote 'akimuonya' Naibu Spika Ndugai kuwa awe makini na maamuzi yake, ili yasije yakaingilia uhuru wa mhimili mwingine wa mahakama.

Lakini mara tu baada ya kutoa tamko hilo alionja joto la jiwe, baada ya bunge zima, kumzomea kwa nguvu, na cha kushangaza zaidi hata wabunge wenzake wa CCM waliungana na wabunge wa ukawa, kumzomea Waziri mkuu wao!

Waziri Mkuu kumwambia "Naibu Spika Ndugai kuwa awe makini na maamuzi yake, ili yasije yakaingilia uhuru wa mhimili mwingine wa mahakama." Ndiyo maana yake kuna barua ya kuzuwia mjadala? Unanchekesha.
 
Moderator hukutenda haki kuihamishia nyuzi yangu huku, hii nyuzi inaongelea mahakama nyuzi yangu inaongelea bunge.

cc Paw Invisible
 
Last edited by a moderator:
Majibu ya Mtoto wa mkulima ndo yaliibua hasira za wabunge... perception ikabadili hali ya hewa kila mtu akahisi kuwepo barua.

Mjadala ukiwapo, aibu yao itakuwa haisemeki... Andaa pop corn na juice ya ukwaju tu FaizaFoxy

Muandalie tu ila usisahau kuweka na DOMPO ya Dom maana TAMTHLIA mpaka iishe kuna tutakao wasikiza karibuni.SI wameshaanza kuwekeana SUMU.Ngoja tukae mkao wa sinema kuendelea.
 
Mh kumbe wote tumelogwa na Marehemu.

Hivi Pida kwa nafsi yake aliyonayo katika nchi naye alikua anajibu issue ya barua ambayo haipo? Mbon nashindwa kuelewa hapa.Pnda si ndio President Kwasasa?

who is fooling who?
Kumbe kina lisu wameitisha press kwakitu ambacho hawana uhakika nacho.
ndo maana pinda akasema busara itumike lakini mahayawani wakamzomea mzee wa watu.
hawa wabunge mabwege hawajui kuwa kina lisu ni watundu na wako kazini kusaka utawala nao kama makondoo wakadandia maneno ya kina lisu bila hata uhakika kama barua ipo ama haipo.
huyo naibu spika nae bila hata kuconfirm uwepo wa barua ama laa akawa anapelekwapelekwa kama zuzu.
mambo ya kutungwa kwenye blogs wanaenda kujadili bungeni
 
Another episode of the ESCROW saga. In the end the ones responsible will still be in the streets holding their ranks.
 
Waziri Mkuu kumwambia "Naibu Spika Ndugai kuwa awe makini na maamuzi yake, ili yasije yakaingilia uhuru wa mhimili mwingine wa mahakama." Ndiyo maana yake kuna barua ya kuzuwia mjadala? Unanchekesha.
.........Maana yake ni kwamba PM anajinyea nyea, anajua hachomoki hata kwa kutumia nyundo. Siku zote mwizi hutetea wezi wenzie na safari hii wezi wote mwisho wenu umefika. Hata baadhi ya wabunge wa CCM akili zao zimeanza kurudi na kuungana na UKAWA kwenye huu wizi wenu.

Yule alieita wenzake Tumbili safari hii mbona kakaa kimya na maneno yake ya khanga?
 
Moderator hukutenda haki kuihamishia nyuzi yangu huku, hii nyuzi inaongelea mahakama nyuzi yangu inaongelea bunge.

cc Paw Invisible
..Moderator umefanya sahihi kama uzi wa huyu dada umeuhamishia huku, hakuna kuanzisha mada tofauti zinazoongelea kitu kimoja na lengo moja kwa kutumia majina tofauti ya Mahakama na Bunge.
 
kwani wanasiasa wa sikuhizi wanazo huko upstair.wanachukua mambo ya media na kwenda kupoteza mda kujadili fununu.

ata kafulurila alinukuu jf askofu na gazeti la dira ; shame on na mfuko wa jimbo kushindwa kuajili wataalamu
 
Back
Top Bottom