Mahakama yalitia hatiani MwanaHalisi

Mahakama yalitia hatiani MwanaHalisi

Kwahiyo Kasheshe unaamini kuwa Richmond haina uhusiano wowote na Rostam?
Ni vigumu kuamini au kutoamini (ingawa kwenye macho ya sheria hadi sasa inaaminika kuwa RA ahusiki na Richmond) kwa sababu Kubenea na gazeti lake wametunyima haki ya kupata uhakika wa kisheria (kutilia uzito kile tunachokiamini kutokana na simulizi zetu).
Kinachonifanya nimlaumu Kubenea ni kuwa mara nyingi tumekuwa tukihimiza watu waende mahakamani kama njia ya kupata uthibitisho wa madai ambayo yanabishaniwa. RA hapa aluienda na hii ilikuwa nafasi adhimu kabisa ya Kubenea na Mwanahalisi kupigilia msumari wa moto kwenye suala la kumhusisha RA na Richmond, lakini hawakwenda mahakamani. Kinachonifanya nianza kuingiwa na wasi wasi kuhusiana na ushahidi wa Kubenea ni sababu wanazozitoa za kwa nini wawlishindwa kwenda kuwasilisha maelezo yao, haziingii akilini sawasawa
 
ilisemwa mara nyingi hapa tatizo la Kubenea ni shule. Haya mambo ya kutaka kupata umaarufu kwa kutumia migongo ya watu matokeo yake ndio haya sasa kaangukia pua!

Kilichobaki asubiri dona la Ukonga na Rostam atakuwa anamlipia hizo 2500 za "kumhifadhi" kule.

Maskini ndege mjanja kanasa kwenye tundu bovu....
 
Huyu Mmafia Kubenea hata baba yake pale Dongo Kijijini hajamjengea nyumba hata ya makuti,anakufa njaa. je ataweza kulipa bilioni 3. akienda kwao kijijini Dongo-Mafia huwa anakodi baiskeli na huwa anakwenda kwa majahazi kweli ataweza kulipa hiyo pesa.
Hiyo mahakama kuna kamchezo kanafanyika kwani haiwezi mara amwagiwe tindikali tukamchangia kwenda kutibiwa leo huyo FISADI-PAPA tumzidishie pesa zingine. Ninachotaka arudishe pesa zetu alizofisadi.
Tanzania uonevu mtupu,sasa naweza kusema mwenye pesa ndiyo mweye HAKI.
Wasomi angalieni tumieni taaluma zenu kuleta haki na maendeleo na siyo kuishi kiujanjaujanja a.k.a mention town --- nyinyi wasomi tunawategemea sana mutuletee maendeleo na kama mishahara yenu midogo daini hata kugoma siyo kuonea watu.
kwa ishu hii ningekuwa warabuni ningejitoa MUHANGA yaishe.
 
Zahir Salim, Fisadi Mtoto na wengine wote wanaomsujudia 'Rais' Rostam:

Hivi mnaamini kweli Marando -- mwanasheria wa Kubenea kashindwa na Rostam?

Haiwezekani! Kuna kitu hapa kinachezwa: Kwa wale waliobahatika kuiona hiyo hukumu ya jaji Makaramba wataona ni dhahiri Rostam kachezewa mchezo, maana anadhani yeye (RA) ni mjanja kuliko Watanzania wote. Sherehe anazofanya kupitia magazeti yake na Habari Leo ni temporary tu. Ngoma bado mbichiiiiii!

Kategewa ndoano na imemnasa barabara mdomoni -- kwa hiyo bado analo la Richmond, lazima aanikwe kwa njia za haki.

Hukumu yenyewe ya kurasa 3, ambayo 'hukumu' hasa ni mistari 13 tu haiwezi ikawa ndiyo hukumu ya shauri hilo, kwani shauri halikusikilizwa kabisa. Akina Mrando hawakuwa wanafika shaurini kwa makusudi, kwa sababu maalum: waligutuka kwamba hawawezi kupata haki chini ya jaji huyo -- tena jaji mmoja.

Kwa hivyo rufaa nadhani itakuwa imewasilishwa -- ya kutaka shauri lisikilizwe na jopo la majaji watatu -- na sheria za kesi za madai inaruhusu hivyo. Na hapo ndipo RA atagundua kuwa kama yeye anajua huu, wengine wanajue hii. Ndipo atakapofahamu kwamba maharage siyo mboga bali ni dawa ya tumbo tu!

Wana-JF Ngoma bado mbichi nawakakishieni -- RA bado yuko kitanzini tu kuhusu Richmond, watanzania tuzidi kumbana huyu hadi kieleweke. Hata akisajili mawaziri wangapi na kuvinunua vyombo vyote vya habari vya serikali, umma ni lazima uibuke mshindi dhidi ya mdosi huyu aliyetuibia mamilioni!
 
Naomba kuuliza, huyo Jaji Robert Makaramba ni kati ya wale majaji waliochaguliwa hivi karibuni na JK? Kuna yeyote anaweza kutuwekea Profile yake?
 
Then taaluma ya ujaji nayo imevamiwa sikihizi hivyo mtu anweza kuhongeka. Si mnamkumbuka yule wakili alieshiriki kukwapua pesa za Deep GREEN finance akapewa ujaji kama asante kwa wizi!!?? Pole Kubenea nilishasema hapo nyuma adui yetu ni mwerevu mno na amejiandaa kupigana, huenda hata hao kina Mnyere na Marando wamepewa mpunga ili kuzunguka mteja wao.
Kama gazeti mwanahalisi litafungiwa moja kwa kwa moja litakuwa pngo kuubwa kwa watanzania wote wapinga ufisadi, kwani ndio gazeti pekee Tanzania lililoanza kutaja jina la Rostam kama mtuhumiwa wa ufisadi kama alivyotangaza Dk. Slaa. Yaani, ni aibu jinsi wanahabari wetu walikuchuna utadhani hawakusikia hilo jina! Ukiwafikiria hata ambao tunawaona kama wakongwe na wajasiri kama ki Jenerari Ulimwengu! waaapi, kwa Rostam walikaa kimya!
 
... shauri halikusikilizwa kabisa. Akina Mrando hawakuwa wanafika shaurini kwa makusudi, kwa sababu maalum: waligutuka kwamba hawawezi kupata haki chini ya jaji huyo -- tena jaji mmoja.

Kwa hivyo rufaa nadhani itakuwa imewasilishwa -- ya kutaka shauri lisikilizwe na jopo la majaji watatu -- na sheria za kesi za madai inaruhusu hivyo.

Then taaluma ya ujaji nayo imevamiwa sikihizi ...

Naomba kuuliza, huyo Jaji Robert Makaramba ni kati ya wale majaji waliochaguliwa hivi karibuni na JK? Kuna yeyote anaweza kutuwekea Profile yake?

Jaji kakosea nini? Kubenea hakuleta utetezi ndani ya siku 21 kama sheria inavyosema.

Kuna mtaalam mmoja hapo juu kadai Kubenea alifanya makusudi ili akasikilizwe na majaji wengine.

Sasa tuambieni enyi wataalam wa sheria. Maana mnazunguka zunguka ukuti tu, kosa la jaji ni lipi hapo?
 
Unajua hapa kuna watu wanajismesha tu,ni haki yao kwa kuwa wanadhani sheria ni kwa ajili yao,wajicheleweshe wenyewe then watake mahakama iwambembeleze kupeleka ushahidi wao.
 
"Jaji kakosea nini? Kubenea hakuleta utetezi ndani ya siku 21 kama sheria inavyosema.

Kuna mtaalam mmoja hapo juu kadai Kubenea alifanya makusudi ili akasikilizwe na majaji wengine.

Sasa tuambieni enyi wataalam wa sheria. Maana mnazunguka zunguka ukuti tu, kosa la jaji ni lipi hapo?"

_____________________

Nanyi pia mnazungukazunguka tu. Kwani nani, au wapi imeelezwa jaji kakosea? Jaji hakukosea, katoa order yake kufuatana na sheria na taratibu zilizopo na kutokana na mazingira yaliyokuwepo baada ya kuombwa kufanya hivyo na upande wa mdai --RA.

Kinachosemwa ni kwamba katika order hiyo hakuna mahala imeelezwa kwa maneno ambayo mtu anaweza kuyanukuu kwamba RA hahusiki na wala siyo mmiliki wa Richmond. Jaji hakufikia uamuzi huu kwa sababu hakulisikiliza shauri lililoletwa.

Makosa yako kwa kina Kubenea na ndiyo maana inasemekana kuwa huenda kafanya hivyo makusudi kulinda masilahi ya upande wake katika shauri hilo. Hizi ni mbinu za wanasheria tu ambazo hutumiwa kutimiza malengo.

Ila cha kuongezea tu ni kwamba kutokana na hukumu hiyo RA anatamba nayo na kujinadi kuwa Mahakama imemsafisha katika sakata la Richmond!!!
 
Back
Top Bottom