Mahakama yamkuta Lady JD na hatia ya kumtukana Ruge Mutahaba

Good People

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2016
Posts
945
Reaction score
1,819
Mahakama ya Kinondoni yamkuta na hatia mwanamuziki nguli wa kizazi kipya Judith Wambura a.K.a Lady Jay Dee kwa kumkashifu mmoja ya wakurugenzi wa Redio ya Clouds Fm.

Aidha Mahakama hiyo imemtaka mwanamuziki huyo kumuomba radhi Bwana Ruge Mutahaba

===========

Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni imemkuta na hatia mwanamuziki Judith Wambura maarufu Lady Jaydee kumkashifu Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga pamoja na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba.

Hukumu hiyo imesomwa mahakamani hapo kufuatia kesi iliyokuwa imefunguliwa na viongozi hao wawili wa Clouds Media Group wakimtuhumi Judith Wambura kuwakashifu na kuwaharibia taswira zao na kampuni yao katika jamii.

Awali mahakama hiyo ilipanga kusoma hukumu ya kesi hiyo ya madai Oktoba 13 mwaka huu lakini Hakimu Lyamwike aliiahirisha hadi Novemba 2 mwaka huu kwa maelezo kuwa hakuwa amemaliza kuiandikia hukumu.

Katika kesi ya msingi, Joseph Kusaga na Ruge Mutahaba waliiomba mahakama itamke kuwa maneno yaliyotolewa na Judith Wambura kubitia blog yake ni kashfa na yanaathiri taswira yao katika jamii, pia mahakama imuamuru aombe radhi kupitia vyombo vya habari na alipe fidia kutokana na madhara ya jumla kwa jinsi mahakama itakavyoona inafaa.

Judith Wambura aliandika waraka katika blog yake na kwenye baadhi ya magazeti uliokuwa na kichwa cha habari “Wosia wangu ikitokea nimetangulia kufa kabla ya Ruge na Kusaga.”

Wakati akijibu shtaka hilo, Wambura ambaye alikuwa mtetezi pekee wa upande wake alikiri kuandika waraka huo.

Chanzo: Swahili
 
Habari wanaJF,

Mahakama ya Kinondoni yamkuta na hatia mwanamuziki nguli wa kizazi kipya Judith Wambura a.K.a Lady Jay Dee kwa kumkashifu mmoja ya wakurugenzi wa Redio ya Clouds Fm.

Aidha Mahakama hiyo imemtaka mwanamuziki huyo kumuomba radhi Bwana Ruge Mutahaba.
 
Awe makini tu maana hapo wanaweza kutaka kumkomoa ili aende segerea,angalau hata kwa siku 3 tu.....kesho yule aliyekushtaki atakuambia ,hata hivyo nilisha kupeleka segedance...

OVA
 
Dada naye inaonekana ni mkorofi kidogo, Kusaga ni mtu wa kwao kwanini wanagombana hakuna wazee kutoka kwao wa kuwasuluhisha?
 
MAHAKAMA YA WILAYA YA KINONDONI IMEMUAMURU MSANII LADY JAY DEE KUWAOMBA RADHI WAKURUGENZI WA KITUO CHA CLOUDS KWA KOSA LA KUWADHALILISHA NA KUWAKEJELI WAMILIKI WA KITUO HICHO CHA HABARI.

-•Katika kesi inayomkabili msanii Judith Wambura Mbibo maarufu kama Lady Jay Dee dhidi ya walalamikaji Joseph Kusaga na Ruge Mutahaba kesi namba 29 ya Mwaka 2013 hukumu yake imetolewa leo na Hakimu wa mahakama ya Wilaya Boniphace Lihamwike kuwa wameridhishwa na ushahidi uliotolewa kuwa msanii huyo alitenda kosa la kuwadhalilisha na kuwakebehi kwa maneno machafu ndugu Joseph Kusaga pamoja na Ndugu Ruge Mutahaba hivyo mahakama ya wilaya ya Kinondoni imeamuamuru msanii huyo kuomba radhi ktk chombo cha habari cha kitaifa au kinachosikika kimataifa pamoja na duniani nzima kuwa maneno yake yalikuwa ya kashfa na udhalilishaji yenye lengo la kuichafua taswira nzuri ya ndugu Kusaga pamoja na ndugu Ruge Mutahaba vilevile Mahakama imemuamuru msanii huyo kulipa fidia na gharama za uendeshwaji wa kesi hiyo. Hukumu ya kesi hiyo ilisomwa leo saa mbili na Nusu asubuhi katika mahakama ya wilaya kinondoni upande wa Msanii Judith Wambura uliwakilishwa na Wakili wake aitwaye Advocate Chacha licha ya msanii huyo kuhudhuria mahakamani hapo na kushindwa kushuka kwenye gari aina ya Noah waliyokuwa wamefika nayo Mahakamani hapo akiambatana na Meneja wake Seven Mosha ambaye alizuiliwa getini na walinzi kutokana na kuvaa nguo isiyozingatia maadili ya Mahakama.

Mwenendo wa kesi hiyo iliyofunguliwa tangu mwaka 2013 kwa msanii huyo akituhumiwa kuwatukana, kuwakebehi pamoja na kuwakashifu ndugu Joseph Kusaga pamoja na Ruge Mutahaba kupitia mitandao ya kijamii na mahojiano aliyokuwa akifanya mara kwa mara na vyombo tofauti vya habari.

Tangu kesi hiyo ilipofunguliwa msanii huyo amekuwa na mwenendo usiokuwa wa kuridhisha na kumfanya kushindwa kesi hiyo ni pamoja na;

1. Kukosa ushahidi wa yale aliyokuwa akiyazungumza yeye binafsi kwamba ametendewa na kufanyiwa na washtaki,

2. Kukosa mashahidi wa kusimama mahakamani kutetea alichokuwa anakisema kwani mpaka kesi inamalizika hakuweza kuleta shahidi hata mmoja. upande wa washitaki uliweza kuleta mashahidi takribani 15 mpaka hukumu ya kesi inasomwa hii Leo.

3. Kutokuhudhuria mahakamani yeye mwenyewe, jambo linalotafsiriwa na wengi kama kutokuwa makini lakini pia kukurupuka kwa yale aliyokuwa akiyasema na kuandika kwani inawezekana kabisa sababu tajwa hapo juu zilimfanya aingie mitini.
 
Lakini akina Ruge kituo chao nimekuwa ndiyo sababu ya kuwaporomosha wasanii.Tumemuona yule Dada wa Bukoba. Aliyeimba chambua kama Karanga akianguka kifo cha mende.Bora Jide alijitambua akaamua kuondoka.Ukweli ukishafika.
 
Alivyo kiburi unaweza ukakuta hata kuomba radhi kutamshinda
 
Du! Aombe tu radhi yaishe,,Hivi na ile kesi ya sugu na ruge imekwishaje na yenyewe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…