Mahakama yamkuta Lady JD na hatia ya kumtukana Ruge Mutahaba

Huyo ruge ana roho mbaya sana,hataki kuona dada wa watu akifanikiwa,hicho kiradio chao cha clouds fm kinampa kiburi mjini
 
Aisee.

Clouds wanapenda sana ugomvi.

ngoja ruby nae awatukane kwenye blog yake.
 
Nadhani picha imeanza baada ya E-FM kuomba madai kutoka kwa Paul James.
 
Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni imemkuta na hatia mwanamuziki Judith Wambura maarufu Lady Jaydee kumkashifu Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga pamoja na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba.

Hukumu hiyo imesomwa mahakamani hapo kufuatia kesi iliyokuwa imefunguliwa na viongozi hao wawili wa Clouds Media Group wakimtuhumi Judith Wambura kuwakashifu na kuwaharibia taswira zao na kampuni yao katika jamii.

Awali mahakama hiyo ilipanga kusoma hukumu ya kesi hiyo ya madai Oktoba 13 mwaka huu lakini Hakimu Lyamwike aliiahirisha hadi Novemba 2 mwaka huu kwa maelezo kuwa hakuwa amemaliza kuiandikia hukumu.

Katika kesi ya msingi, Joseph Kusaga na Ruge Mutahaba waliiomba mahakama itamke kuwa maneno yaliyotolewa na Judith Wambura kubitia blog yake ni kashfa na yanaathiri taswira yao katika jamii, pia mahakama imuamuru aombe radhi kupitia vyombo vya habari na alipe fidia kutokana na madhara ya jumla kwa jinsi mahakama itakavyoona inafaa.

Judith Wambura aliandika waraka katika blog yake na kwenye baadhi ya magazeti uliokuwa na kichwa cha habari “Wosia wangu ikitokea nimetangulia kufa kabla ya Ruge na Kusaga.”

Wakati akijibu shtaka hilo, Wambura ambaye alikuwa mtetezi pekee wa upande wake alikiri kuandika waraka huo, hivyo mahakama imemtaka aombe radhi kwenye chombo cha habari chenye coverage kubwa hapa nchini na ikiwezekana duniani pia

Kwa hisani ya MPEKUZI
 
clouds ni chombo cha ccm,ni kama idara yao ya uenezi
 
Mdau kumbe anga hizi pia unapita........
 
Kwani aliwakashifu kutumia nini mpaka waombwe kupitia media kubwa ?
 
Kivipi alikuwa mtetezi pekee wa upande wake, inamaana hakuwa na wakili?
 
Back
Top Bottom