Mahakama yamkuta Lady JD na hatia ya kumtukana Ruge Mutahaba

Mahakama yamkuta Lady JD na hatia ya kumtukana Ruge Mutahaba

Kwani aliwakashifu kutumia nini mpaka waombwe kupitia media kubwa ?
ww ujielewi soma uelewe vema,mahakama inamua vile inavuoona inafaa,lengo ni kuwasafisha duniani lazima atumie chombo kikubwa aende itv,eatv au clouds uenyewe maana tbc naona ndo ya mwisho kwa kusikilizwa nchini.Huyu dada nae ajifunze aache ugomvi na kujiona vile ni msanii mkubwa anaweza tu kuanzisha ligi na watu.akijua ana amshqbiki watasimama nyuma yake,bila kujua kuwa ili asimame au watu wasimame juu yake inatakiwa atumie vyombo vya habari vikubwa,ona sasa toka aanze ugomvi yuko wapi na ndi ndi ndi yake anajitahidi sana kurudi nankufanya Tour lakini sio kama zamani.Aombe radhi maisha yaendelee na kusaga na ruge wamsamee kama walivyofanya kwa sugu ili wajenge mziki wetu.
 

Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni imemkuta na hatia mwanamuziki Judith Wambura maarufu Lady Jaydee kumkashifu Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga pamoja na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba.

Hukumu hiyo imesomwa mahakamani hapo kufuatia kesi iliyokuwa imefunguliwa na viongozi hao wawili wa Clouds Media Group wakimtuhumi Judith Wambura kuwakashifu na kuwaharibia taswira zao na kampuni yao katika jamii.

Awali mahakama hiyo ilipanga kusoma hukumu ya kesi hiyo ya madai Oktoba 13 mwaka huu lakini Hakimu Lyamwike aliiahirisha hadi Novemba 2 mwaka huu kwa maelezo kuwa hakuwa amemaliza kuiandikia hukumu.

Katika kesi ya msingi, Joseph Kusaga na Ruge Mutahaba waliiomba mahakama itamke kuwa maneno yaliyotolewa na Judith Wambura kubitia blog yake ni kashfa na yanaathiri taswira yao katika jamii, pia mahakama imuamuru aombe radhi kupitia vyombo vya habari na alipe fidia kutokana na madhara ya jumla kwa jinsi mahakama itakavyoona inafaa.

Judith Wambura aliandika waraka katika blog yake na kwenye baadhi ya magazeti uliokuwa na kichwa cha habari “Wosia wangu ikitokea nimetangulia kufa kabla ya Ruge na Kusaga.”

Wakati akijibu shtaka hilo, Wambura ambaye alikuwa mtetezi pekee wa upande wake alikiri kuandika waraka huo, hivyo mahakama imemtaka aombe radhi kwenye chombo cha habari chenye coverage kubwa hapa nchini na ikiwezekana duniani pia


Kwa hisani ya MPEKUZI
Aombe radhi tu, hakuna namna, Mahakama imetoa tafsiri sahihi ya Sheria. Pia watu waache Mihemuko, ninachoamini mtu kama Kusaga ana dhamira njema tu ya kuinua huo mziki wao, Sasa haya mambo yafike hatua Heshima iwepo. Si Lazima watu wote wawe wanamuziki.
 
Habari za Tz za hovyo sana aisee
 
Mahakama nayo kwa kupenda rushwa jde anastahili kushinda vle clouds wanatumia hella ili kumkomoa
 
What goes around comes around...ivi nakumbuka alimkomalia G aombe radhi ile ishu ya kukaa-ZWA na wanaharakati walikuja juu kweli kua kadharirishwa leo waje tena basi binti yao kavurunda huku [emoji23][emoji23] kama kweli komando basi andi ndi ndi akakae segedance maana komando haogopi ngome.
 
Ningekuwa mimi Jide ningeomba msamaha kwa style ya aina yake...ningeomba airtime cloudstv na radio..halafu ningejitilisha huruma mpaka ingenipa kiki ya ajabu[emoji38][emoji38]
 
Komando usiombe radhi utajishushia hadhi yako na utawasononesha wote wasioipenda clouds na ccm
 
Back
Top Bottom