Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wakuu,
Baada ya kukamatwa usiku wa kuamkia leo Januari 10, 2025 mwanaharakati Dkt. Wilbroad Slaa na kufikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar Es Salaam, dhamana yake imekwama kwa kile kinachodaiwa hofu juu ya usalama wake.
Akizungumza baada ya kutoka mahakamani hapo Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika, Wakili Boniface Mwabukusi amesema kuwa makosa yaliyofanya Dkt. Silaa kukamatwa ni kutoa taarifa za uongo kupitia mitandao ya kijamii
"Alipost kwenye mtandao wa Twitter(X) akieleza kuna mawasiliano kati ya Rais(Dkt. Samia Suluhu Hassan) na mwamba(Freeman Mbowe) na mawasiliano hayo ni ya kupeana msaada wa kifedha kwa hiyo Jamhuri inasema makosa hayo ni ya uongo na kinyume na kifungu cha 16 cha sheria cha makosa ya mtandao"
Mwabukusi ameeleza kuwa baada ya walipofika mahakamani walikuta Jamhuri imewasilisha kiapo cha kupinga Dkt. Slaa asipewe dhamana kwa sababu ya usalama wake lakini mawakili wa upande wa utetezi hawakuwa wamepewa kiapo hicho hivyo kuhitaji muda wa kukifanyia kazi kiapo ili kuandaa kiapo kinzani.
Wakili Mwabukusi ameeleza kuwa kosa analotuhumiwa nalo Dkt. Slaa ni kosa ambalo lina dhamana na pia kuhusu ulinzi wake wale wanaohofiwa kumshambulia ndio wangekamatwa ili aweze kupewa dhamana na kuwa salama.
Aidha upande wa Jamhuri umesema upelelezi haukuwa umekamilika. Hata hivyo mahakama imeahirisha shauri hilo mpaka jumatatu ya Januari 13, 2025.
,============================================================
Hii ndio kauli aliyoisema Dkt Willbroad Slaa na kusababisha kukamatwa na Jeshi La Polisi