Mahakama yamwamuru Reginald Mengi afike kujieleza kwanini asifungwe kwa kupuuza hukumu ya Mahakama

Mahakama yamwamuru Reginald Mengi afike kujieleza kwanini asifungwe kwa kupuuza hukumu ya Mahakama

Status
Not open for further replies.

Babu wa Kambo

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2016
Posts
559
Reaction score
808
1.jpg

MAHAKAMA Kuu Kitengo cha Biashara imeamuru Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi afike mahakamani kujieleza kwa nini asifungwe gerezani kwa kushindwa kutekeleza hukumu inayohusu malipo ya Sh bilioni 1.2.

Mengi anatakiwa kufika mahakamani hapo Agosti 24, mwaka huu kujieleza kutokana na kushindwa kutekeleza hukumu iliyomtaka kuwalipa wafanyabiashara watatu, Muganyizi Lutagwaba, Eric Mshauri na Charles Mgweo, Sh bilioni 1.2.

Alitakiwa kuwalipa fedha hizo kutokana na mgogoro wa malipo ya uuzwaji wa hisa katika Kampuni ya Douglas Lake Minerals Ltd ambayo kwa sasa inaitwa Handeni Gold Inc.

Kwa mujibu wa hati ya wito wa kufika mahakamani, Mengi anatakiwa kufika mahakamani hapo Agosti 24, mwaka huu ili ajieleze kwa nini asifungwe gerezani kama mfungwa wa madai kama sehemu ya kukazia hukumu hiyo.

Mahakama imetoa hati hiyo kutokana na wafanyabiashara hao kuwasilisha maombi katika hatua ya kukazia hukumu iliyotolewa Januari 28, mwaka huu na Jaji Agathon Nchimbi wa mahakama hiyo.

Katika hati ya kiapo ya wafanyabiashara hao, inadaiwa walifungua kesi dhidi ya Mengi na Kampuni ya K.M. Prospecting Limited, wakidai malipo yaliyokuwa yamebakia ya dola 428,750, 100,000 na 70,000, kwa kila mmoja.
 
Ulisikia wapi tajiri kafungwa..? Anaweza fika mahakamani na kusema mm tajiri huwezi nifunga...!!
 
Sasa kesi ya madai ifunge mtu tena mfanyabiashara mkubwa kama mengi!!!
Haaaah !!
 
Kuna usemi ule unasema "Jela haina mwenyewe" anaweza kwenda hiyo August 24 ukashangaa wanampeleka lupangoo anaweza kaa siku 3 au 4 na akatoka, lakini mwisho wa siku utakuwa ushasekwa ndani.....na ushaionja jela!

Ova
 
Reginald Abraham Mengi needs to think twice.

At the age of 70 with success in most of his business's he is supposed to live a peaceful life without court hassles and media attentions.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom