Mahakama yathibitisha Stella Moses aliyepoteza maisha akiwa Kituo cha Polisi Mburahati alijinyonga

Mahakama yathibitisha Stella Moses aliyepoteza maisha akiwa Kituo cha Polisi Mburahati alijinyonga

Eti ooh mwanao kajinyonga hao dawa yao sio mahakama dawa yao unafunga safari ukirudi ni kutazama maiti za wahusika
 
Sawa, mahakama imethibitisha alijinyonga, je vitu / vifaa alivyotumia kujinyonga vilipitaje wakati mtuhumiwa kabla ya kuingizwa mahabusu anatolewa vitu vyote vinavyoweza kuleta au kuharibu amani humo ndani?

Wakati anajiua alikuwa selo ya peke yake? Inawezekanaje mtuhumiwa kujinyonga mpaka kufikia mauti wenzie wakiwa wanamtazama?

Alifika na majeraha, je hatuna utaratibu wa kuwafikisha hospital watuhumiwa wakiwa chini ya ulinzi tunawashikilia hivo hivo wakiwa wagonjwa / mahututi?

Anyway apumzike kwa amani.
Hujasoma vizuri, imeandikwa juu hapo, "alitumia nguo zake" kujinyonga.
 
Nilipoona tuu jina kingai akili imeniambia kuna udanganyifu hapo, kwa tabia ya askari wa uswahilini huyo mdada walimpiga hadi akafariki wakaziba noma kwa kumnyonga ili ionekane alijinyonga, kwa sababu swali la kujiuliza hayo majeraha ya kichwani na sehemu zingine mwilini yalitoka wapi 🤔🤔 yule kingai na askari wake watachomwa moto kabla hawajafika jehanamu,

hua nikisia askari amepigwa au ameuliwa hua nafarijika moyoni kwa madhira waliyo nipatia wale washenzi,😡😡😡 hata nikipita sehemu nikute askari anafanyiwa jambo lolote baya hakika nitapita kama naaga maiti😡😡😡
Mahabusu wengine waliokuwa jirani lazima wanaujua ukweli.Mahakama imeonesha udhaifu na uhalifu mkubwa.Kabisa.
 
Police waache ujinga wa kukamata watu wanaodaiwa! Deni sio jinai. Police washungulika na jinai tu. Huu ni uonevu kukamata watu wanaodaiwa kisa polisi wamepewa bakshishi.
 
Hivi unazijua taratibu za mtuhumiwa kuwekwa mahabusu wewe?Ina maana yeye aliruhusiwa kuingia na nguo nyingi?Au alivua aliyovaa akatumia kujinyonga?
kwa mwanamke, anaingia na kanga zake, chupi, na nguo zote kama kawaida. anaweza kutumia hizo kwa kuzichana na kutengeneza kamba. swali linakuja, alikuwa mahabusu peke yake? mahabusu huwa zinatengenezwa kwa namna ambayo hakuna sehemu hata ya kushikiza kamba, utakuta mlango tu kwengine kote kunateleza huwezi hata kutundika chochote wala kupanda ukuta. sasa yeye alijitundikia kwenye nini na alikuwa peke yake mahabusu yote?
 
Hujasoma vizuri, imeandikwa juu hapo, "alitumia nguo zake" kujinyonga.
Alikuwa selo ya peke yake mpaka anavua hizo nguo anatundika na anajitoa uhai?

Ni nguo za aina gani pamoja na material ili kuangalia uwezo wa kushikilia mwili wa mtu mzima mpaka kutoka roho?

Maswali ni mengi mkuu, wanaoshtaki wamesema watakata rufaa basi tusubiri majibu naamini wahusika watakuja na majibu
 
kwa mwanamke, anaingia na kanga zake, chupi, na nguo zote kama kawaida. anaweza kutumia hizo kwa kuzichana na kutengeneza kamba. swali linakuja, alikuwa mahabusu peke yake? mahabusu huwa zinatengenezwa kwa namna ambayo hakuna sehemu hata ya kushikiza kamba, utakuta mlango tu kwengine kote kunateleza huwezi hata kutundika chochote wala kupanda ukuta. sasa yeye alijitundikia kwenye nini na alikuwa peke yake mahabusu yote?
There you are!Hakuna hata sehemu iliyo karibu kuning'iniza kitu au mtu kutoka juu gravity itokee.Sasa alijinyongaje?Alijinyonga kwa kuegemea kiubavu lango/geti la mahabusu?Kujinyonga si sawa na kupigwa electrical shock kwamba ingechukua sekunde mbili tu.Alikuwa peke yake humo mahabusu hadi afanye maandalizi ya kuchanachana gagulo ili apate kamba ndefu ya kujinyongea?Comical case!
 
lakini pamoja na yote hayo, kwa uzoefu wangu pia, ni ngumu kwamba polisi watakuwa walimpiga. askari sio rahisi sana kumpiga hadi kufikia kumuumiza mwanamke. wanaopigwa wanakuwaga wanaume ila wanawake hawawapigi aisee. sema inawezekana alitoka na shida labda alipigwa huko alikotoka na hakutibiwa au wameamua kumfichia siri mtu wa nje aliyemsababishia madhara though pia ni ngumu polisi kukubali kubeba msala kama huo au sijui nini, ngumu kuamini chochote.
 
Ila ni mambo ya aibu na kufikirisha kwa hili lililotikea hasa ikikumbukwa mambo ya awali kama ya Zombe na wahalifu wenzake,ya Mtwara na hata akitajwa Kingai tu.🤔
 
Allah ndiye anajua zaidi, kamwe sitajitia upofu kwenye mambo ya dhahiri, ALLAH atanihukumu
Hapa sote tunaliongelea hili jambo tukiwa "ghaibu", hakuna dhahiri hapa labda useme ulikuwepo kwenye tukio.

Tunachohitaji ni details zaidi na mahakama ya rufaa itaamuwa vipi, kama nilivyoandika juu huko.

Tusisukumwe kuhukumu kwa hisia zetu.
 
Afadhali umeandika hivi kuliko awali wote tulichagua uoande kwa hisia na mazingira.
 
Hivi unazijua taratibu za mtuhumiwa kuwekwa mahabusu wewe?Ina maana yeye aliruhusiwa kuingia na nguo nyingi?Au alivua aliyovaa akatumia kujinyonga?
Hapa hatupo kuhukumu wala kutetea, kuna wakili mzuri sana anae, nimeona juu huko, hivi wewe unataka kuanza kutufundisha nini zaidi?

Kwanza uelewe mwanamke anavaa nguo ngapi, ni tofauti na mwanamme, hususan mwanamke aliyekwenda kujisalimisha mwenyewe polisi, akielewa kuwa kuna kulazwa ndani huko.

Tusijichukulie kazi za watu mikononi mwetu, chochote kinawezekana, tuwawachie mawakili na mahakimu wafanya kazi zao.

mana hapo kuna mpaka ushahidi wa "corona" siyo kesi ya mchezo mchezo hiyo wala tusiigeuze kuwa siasa kwa ujinga wetu tu.
 
Back
Top Bottom