Mahakama yatoa hati ya kumkamata Zacharia Hans Poppe, kuunganishwa kesi ya utakatishaji fedha

Mahakama yatoa hati ya kumkamata Zacharia Hans Poppe, kuunganishwa kesi ya utakatishaji fedha

Mkuu hizi timu zinawaingizia Pesa sana,maana wanazikopesha,then hela yoyote ikiingia kwenye timu wanachukua,pia ukisikia mchezaji kasajiliwa milioni 150 labda ujue ni milioni labda 60 tu,zingine wanakula wao.Hizi teams ndo maana kila mtu anazihitaji hata mabadiriko inakua ngumu kutokea cos ni mitaji ya watu
Watatubu safari hii.
 
Kwenye akaunti yake kuna laki sita teh teh

yule mhindi wa iptl ana tamaa ya hela sana, sasa hvi usingekuta yupo mahabusu.... Seth ana puto tumboni mda wowote litapasuka
Hanspope alijiongeza

Ova
 
Benki wanajuaje mkuu,au kuna kiasi kikifika account inakuwa pending??[/QUOTE]
Bank wao hawana shida sana maana wewe si unawapelekea hela watazipokea kama hela zenyewe unaziingia hapa nchini tofauti na zile unazoingiza kutoka nje ambazo zina utaratibu wa kuziingiza...kimsingi historia ya akaunti yako ndio itawafanya wakushitukie hasa utakapotaka kutoa kwa kasi ya ajabu ndipo wataanza kuonyesha mashaka lakini kama tangu umefungua mara unaingiza laki mara milioni mara milioni 1, na hata kitokea umeingiza milion 30 hawawezi kuwashangaza sana tofauti na mtu ambaye akaunti yake haina mihamala ya kueleweka ...but all in all akaunti yako itakuwa at risk mpaka pale mamlaka zingine zitakapokushitukia nyendo zako za matumizi na kuanza kuangalia ela unayomilki na record yako TRA maana mtu yoyote mwenye shughuli rasmi lazima atasomeka TRA.

Na
 
Ni kweli ukisemacho

Ila,sehemu ya pesa ya kirahisi rahisi namna hiyo manyang'au ni mengi ni rahisi sana kugaragaraza heshima yako uliyojenga miaka nenda rudi kwenye jamii na kwenye biashara yako..

Shida yangu mimi ni jinsi watu hawa hawapendi kuchafuka kufanya biashara bila mambo ya cut corners...Sijui kwanini watu hawapendi kuchafuka hasa huku mitaroni wakafanya biashara halali wakapata an honest dollar with a long term respect?Sijui kwanini...jibu hua sipati kabisa!

Hebu angalia Poppe ataozea jela sasa!

Na jinsi chattle ana hasira nae alimsema vibaya kwenye media miaka hiyo,hatamuacha hata unywele!Masifa ya kupenda media na migazeti!Hata kama unampiga waziri yanini ukamseme kwenye TV tena kwenye primetime new bulletin?Masifa sasa yana come back at him!

It is sad but true!
Nina uhakika 100% pope hana makosa labda afungwe kwa kuonewa
 
Mnakumbuka sentensi ya Mkuu kuwa TLS ni chama cha Umma ? Hivyo kuwa na control 100% ya maisha yetu kila kikundi kitawekwa chini ya mashushu wa ccm
Alianzwa Manji akaondoka Yanga.
Wakaenda TFF wakaondolewa kina Malinzi...huyu msomali akaitwa akaambiwa sio msomali kalegea sasa ameshatiwa mikononi
Wakaja Simba wakaanza na Akina Aveva na Kaburu wakaona Zakaria naye lazima atoke.
Hivyo hizi ni njama mpya dhidi ya club huru ambazo zina ushawishi mkubwa Tanzania na EA.
Haya hayajaanza leo ..miaka ya Mwanzo ya 1970s , Simba na Yanga zilikua maarufu sana kuliko TANU.
Kuanzia wachezaji wake na Viongozi hali hii iliwakera wakubwa na Mwalimu njama zikapangwa ikaanza Yanga waka gombanishwa ika vunjika pande mbili ..kundi kubwa likaunda Pan Africa ..yanga ilishuka daraja kwa mara ya kwanza.
Simba nayo haikusalimika ..fitina zikatiwa ika katika vipande viwili na kuzaliwa Red Stars .
Karume naye hakuwa nyuma ya club hizi..in fact majengo yote yamejengwa kwa msaada wa karume Rais wa kwanza wa Zanzibar
Labda tumuombe brother Mohamed Said atuwekee kidogo siasa za simba na yanga
 
Wabongo at it!The police,prosecutors and judges are themselves!Speaking as if they know and saw each and everything,no objectivity at all.
 
Leo April 30, 2018 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa amri kwamba mwenyekiti wa usajili wa Simba SC, Zacharia Hans Poppe na Franklin Lauwo wakamatwe na wafikishwe mahakamani kuunganishwa katika kesi inayomkabili Rais wa Klabu hiyo, Evans Aveva na Makamu wake Kaburu.

Amri hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba baada ya Wakili wa TAKUKURU, Leonard Swai kubadilisha hati ya mashtaka na kuwaongeza watuhumiwa hao.

Swai amedai amewatafuta washtakiwa hao toka mwezi wa tatu bila mafanikio na kuomba hati ya kuwakamata washtakiwa hao ambao hawakuepo mahakamani.

Washtakiwa hao wameongezwa katika kesi ya utakatishaji fedha na kugushi inayomkabili Rais wa Simba, Evans Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ .

Huyu naona alokuwa akitafutwa muda mrefu kuna uzi humu ambao alikuwa anamponda sana mtukufu wakati anatumika Wizara ya ujenzi miaka ya nyuma maneno magumu sana aliongea kuhusu mtukufu,hapa naunganisha dot hapa hachomoki.
 
Mimi naona kuna mkono wa wanasiasa au viongozi wa serikali. Sasa suala la Club tena inayomilikiwa na wanachama, inakuwaje TAKUKURU ndio waendeshe hiyo kesi? Nani mlalamikaji? Hao waliokamatwa ndio wanaotoa hela zao kuiendesha Simba, leo unawashtaki kwa kutakatisha hela? Jamani tuamkeni watanzania huu ni mpango wa baba Jesca na Bashite kumfunga Hanspope!!
 
Yuko Rwanda/Burundi kitambo sana
Alikuwa anakujaga Bongo ila kwa style hii sjui kama atatia mguu.....kwanza afya yke yenyewe Syo nzuri muda sana nlimuonaga anatembea kwa gongo tena lile lenye miguu mitatu chini
Sasa lupango atakuweza kweli

Ova
Huko aliko kimbilia naona siko kabisa maana ndio kwa washkaji zake jiwe angalau angesepea Kenya !
 
Hahahaha Jiwe alikuwa anamtafuta kwenye 18 zake kitambo sana
Sasa kampata nadhani walikwaruzana jiwe akiwa waziri
 
Ana roho Saba kama paka huyo,alihukumiwa maisha na bado akatoboa,wenzake karibu wote walishakufa,mdogo wake alivyotoka jela akatambaa Australia.
Naye huyo mdogo wake alishafariki. Alifia huko huko Australia.
 
Unapata fedha Haramu (mfano za kupora benki, madawa ya kulevya, dili serikalini n.k) halafu unatumia Miradi halali (mfano unaanzisha biashara ya night club, kiwanda) kupumbaza Umma wasijue hela umetoa wapi.

Hiyo ndiyo kutakatisha fedha
Addition on that Kuna mikopo mikubwa lakini inakuwa so halisi. Mfano nakopa 5b naziingiza kwenye ununuzi mazao ya biashara then narejesha ionekane nilipata hela nyingi huko wakati si kweli.
 
Back
Top Bottom