Mahakama yatupilia mbali kesi ya Kikatiba ya kupinga kuhojiwa kwa Profesa Assad na Kamati ya Bunge

Mahakama yatupilia mbali kesi ya Kikatiba ya kupinga kuhojiwa kwa Profesa Assad na Kamati ya Bunge

Hivi hiyo kamati ya kinga sijui na hadhi ya bunge wakikuita kukuhoji then ukienda kuitikia wito halafu ukiwa mbele yao ukagoma kuongea chochote au wakikuuliza chochote unawajibu sina LA kusema , wakikuuliza jingine unawajibu no comment hivyohivy hadi mwisho, wanaweza kukupa adhabu?
Na niadhabu ya namna gani ? Au inakuwaje let's say kwa mtu ambaye ana mishe zake binafsi tu
 
Huenda CAG Msitaafu Prof Mussa Assad akafika tena mbele ya kamati ya bunge kuhojiwa kutokana na kesi yake iliyofunguliwa na Zitto Kabwe ya kupinga kuhojiwa kutupwa na mahakama.

Prof Assad ana tuhuma za kuliita bunge la Tanzania kuwa ni dhaifu na halijiwezi kwa chochote pia wabunge wa bunge hilo ni mazuzu.
===

Mahakama Kuu ya Tanzania imetupilia mbali kesi ya kikatiba ya kupinga kuhojiwa aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad katika Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka kwa tuhuma za kuliita Bunge la Tanzania dhaifu.

Uamuzi huo umetolewa na jopo la majaji watatu wa mahakama hiyo, lililooongozwa na Jaji Dk Benhajj Masoud, akishirikiana na majaji Elinaza Luvanda na Yose Mlyambina.

Katika uamuzi huo ulioandikwa na Jaji Luvanda kwa niaba ya jopo hilo, wa Oktoba 7, mwaka huu ambao Mwananchi limeuona nakala yake leo Jumatatu, Oktoba 25, 2021, mahakama hiyo imeitupilia mbali kesi hiyo ikisema kuwa haina mashiko ya kisheria na kwamba mdai hakuwa na hoja za msingi.

Shauri hilo la maombi mchanganyiko namba 01 la mwaka 2019, lilifunguliwa na Kiongozi wa Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe Mahakama Kuu, Masjala Kuu, dhidi ya Spika wa Bunge, Job Ndugai na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Katika shauri hilo Zitto alikuwa akipinga uamuzi wa Spika Ndugai kumtaka, CAG Profesa Assad kufika mbele ya kamati hiyo kuhojiwa kutokana na kauli yake aliyoitoa wakati akihojiwa na Redio ya Umoja wa Mataifa, nchini Marekani Januari 7, 2019, kuwa Bunge la Tanzania ni dhaifu.

Zitto ambaye alikuwa akiwakilishwa na wakili wa kujitegemea Jebra Kambole alikuwa akidai kuwa kitendo cha Spika kumuita CAG kuhojiwa kwenye kamati ya Bunge kwa kauli hiyo hakikuwa halali na kwamba kilikuwa kinyume cha Katiba.

Wakati wa usikilizwaji wa shauri hilo wakili wa Zitto, Kambole alidai kuwa CAG alikuwa akitoa maoni yake kuhusiana na majukumu yake kama CAG nchini Tanzania na kwamba alikuwa akitumia uhuru wake wa kujieleza unaolindwa na Katiba ya nchi na mikataba ya Kimataifa.

Alisisitiza kuwa mamlaka hayo ya Bunge kumuita mtu yeyote chini ya Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki ya Bunge yana ukomo kwa kuwa kuna baadhi ya watu wana kinga ya kisheria, akiwemo CAG ambaye alidai kuwa halazimiki kutimiza maelekezo ya mtu au idara yoyote ya Serikali.

Badala yake wakili Kambole alidai kuwa taasisi yenye mamlaka pekee ya kuhoji jambo lolote linalofanywa na CAG ni Mahakama na si Kamati ya Bunge.

Mahakama katika uamuzi baada ya kurejea Sheria na Kanuni za Bunge nayo imekubalinana na hoja za Serikali kupitia kwa Wakili Mkuu wa Serikali (Solicitor General-SG), Gabriel Malata ikisema kuwa Bunge au Kamati ya Bunge ina mamlaka ya kumtaka mtu yeyote kufika mbele yake.

“Ni kweli kwamba CAG analindwa chini ya masharti ya Ibara ya 143(6) ya Katiba. Hata hivyo haki hiyo hapa ina mpaka kwa kumlinda CAG wakati tu anatekeleza majukumu yake.” imesema mahakama hiyo katika uamuzi huo, kwa tafsiri isiyo rasmi na kunukuu Ibara hiyo ndogo ya 6 ya Ibara ya 143 ya Katiba.

Mahakama hiyo imesema kuwa ingekubali kuwa CAG alikuwa anatoa maoni yake katika dhana ya uhuru wa kujieleza, lakini ikasema kuwa kipimo cha hilo ni kama kauli hiyo aliyoitoa wakati wa mahojiano hayo ilikuwa inahusiana na utendaji kazi wake kama CAG nchini Tanzania.

“Tunafahamu kwamba mahojiano yalihusiana na taarifa za CAG na mapendekezo yanayotolewa humo. Lakini hakuna mahali popote paliposemwa kwamba madai ya udhaifu wa Bunge ni miongoni mwa mapendekezo yake, ili kuwa na haki hiyo.” imesema mahakama hiyo.

Imesema kuwa kama taarifa ya CAG ingekuwa na maoni hayo miongoni mwa mengine kuwa Bunge ni dhaifu, basi kauli ya CAG ingekuwa imelindwa na Ibara ya 143 (6) ya Katiba.

Chanzo: Mwananchi
Huyu babu kwa kulalamika! Sina hamu. Aliteuliwa na rafiki yake Kikwete akasahau kuwa mwendazake hakuwa na urafiki bali uchapakazi
 
Maneni ya Pro Assad [mazuzu],
unaweza sema niyaukweli:

Wabunge before mwezi March Covid19 haipo, tutumie nyungu inatutosha...

..Mwenda zake kaenda..

Wabunge mwezi March adi leo hii, wananchi tuchome chanjo Covid19 inaua, njia pekee ni chanjo, tena zipo nyingi tumepewa bure.

Ili Bunge bana, cjui kuna watu gani Mule ndani...
 
Jafar Musa Assad kwanini aite wabunge mazuzu? Hivi kweli wabunge wetu ni mazuzu? Haya ni matusi makubwa sana.

Aitwe haraka bungeni, na ahojiwe na asulubiwe haraka, hii itatia heshima kwa watu wengine kuheshimu bunge letu.

Musa kwanza sio jina lake, kaiba jina alifeli itakuwa huyu huko shuleni, akaacha jina lake Jafar.. Pia ahojiwe hilo jina la Musa kapataje? Vetting upya ifanyike plz.
Heshima ni yeys kuwasema Watanzania wanaotaka kufanywa Mazuzu na hao Mazuzu wanaongalia matumbo yao bila kujali kesho ya Watanzania itakuwa vipi,

Huo ndio uzuzu na sehemu ya Mazuzu yanashabikia Uzuzu bila kuangalia wengine bali kushibisha matumbo yao na haoo yenyewe yanakuwa akili yameziweka pembeni na kubaki Mazuzu ila yakiuokosa Ubunge na vyei vingine ndio uzuzu unawaondoka na kuwa na akili kama za Assad Mussa
 
Jafar Musa Assad kwanini aite wabunge mazuzu? Hivi kweli wabunge wetu ni mazuzu? Haya ni matusi makubwa sana.

Aitwe haraka bungeni, na ahojiwe na asulubiwe haraka, hii itatia heshima kwa watu wengine kuheshimu bunge letu.

Musa kwanza sio jina lake, kaiba jina alifeli itakuwa huyu huko shuleni, akaacha jina lake Jafar.. Pia ahojiwe hilo jina la Musa kapataje? Vetting upya ifanyike plz.

Na wewe ni zuzu kama wao
 
Umeaoma taarifa lkn? Kwanza ni taarifa ya zamani sana na alisha hojiwa undoa UZUZU WAKO
 
Hivi Assad asipokwenda itakuwaje? Bunge litatuma polisi? Na kwa nini mlalamikaji ndiye awe anamhoji mlalamikiwa?
 
Maneni ya Pro Assad [mazuzu],
unaweza sema niyaukweli:

Wabunge before mwezi March Covid19 haipo, tutumie nyungu inatutosha...

..Mwenda zake kaenda..

Wabunge mwezi March adi leo hii, wananchi tuchome chanjo Covid19 inaua, njia pekee ni chanjo, tena zipo nyingi tumepewa bure.

Ili Bunge bana, cjui kuna watu gani Mule ndani...
Ndio mazuzu hao
 
Jafar Musa Assad kwanini aite wabunge mazuzu? Hivi kweli wabunge wetu ni mazuzu? Haya ni matusi makubwa sana.

Aitwe haraka bungeni, na ahojiwe na asulubiwe haraka, hii itatia heshima kwa watu wengine kuheshimu bunge letu.

Musa kwanza sio jina lake, kaiba jina alifeli itakuwa huyu huko shuleni, akaacha jina lake Jafar.. Pia ahojiwe hilo jina la Musa kapataje? Vetting upya ifanyike plz.
Mazuzu kwa ubora wenu

Sent from my SM-N9150 using JamiiForums mobile app
 
Huyu babu kwa kulalamika! Sina hamu. Aliteuliwa na rafiki yake Kikwete akasahau kuwa mwendazake hakuwa na urafiki bali uchapakazi
Uchapakazi alikuwa nao ndio maana alitaka 1.5T ilifanyika nini baa da ya jiwe kuona hivyo akatumia umadarakati wake kupitia kwa mazuzu wamfanyie hila na kumfukuza kazi.

Leo zuzu moja limeshakufa yamebakia mengine likiwemo sipika.

Sent from my SM-N9150 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom