Mahakama yatupilia mbali ombi la Jacquiline Ntuyabaliwe (Mjane wa Reginald Mengi) kuutambua wosia alionao

Mahakama yatupilia mbali ombi la Jacquiline Ntuyabaliwe (Mjane wa Reginald Mengi) kuutambua wosia alionao

Huyo anajichosha yeye km alishindwa kumpukutisha akiwa hai ss hivi kazima km mshumaa bora akitulize.!!
Mwenzie madame Ritha kajipigia mipunga na watoto kasomeshewa ss hivi mwanae boss DSTV hana stress.!

Nikikumbuka walivyokimbilia nje kufunga ndoa kimya kimya huku bi mkubwa hajui lolote.!!
Akajiona kayapatia kumbe wachaga wanamchora😂😂😂
Hivi anawajua wachaga vizuri kwenye mali??
Yeye aendelee na danga lake la Dubai huko huku wachaga wamekaba kila kona.!!
 
Mjane wa Reginald Mengi aangukiapua tena mahakamani, mahakama yatupilia mbali rufaa yake

Mjane wa aliyekuwa mfanyabiashara maarufu Reginald Mengi Jacline Tuyabaliwe ametangulia pua baada ya mahakama kutupiliwa mbali rufaa yake .

Jackline Ntuyabaliwe aliitaka mahakama iutambue waraka wa wosia wa marehemu Mengi ambao ulikataliwa na mahakama kuu.
---
Mahakama ya Rufani imetupilia mbali shauri la maombi ya marejeo lililofunguliwa na mjane wa Reginald Mengi, Jacquiline Ntuyabaliwe na wanawe wawili, ambao wamekuwa wakipambana kutetea wosia unaodaiwa kuandikwa na Mengi ambao Mahakama Kuu iliubatilisha.

Katika shauri hilo, Jacquiline na wanawe anaowasimamia, Jayden Kihoza Mengi na Ryan Saashisha Mengi walikuwa wanaiomba mahakama irejee na hatimaye itengue uamuzi uliotupilia mbali shauri la maombi ya mapitio, walilolifungua awali mahakamani hapo wakipinga hukumu ya Mahakama Kuu, iliyoukataa wosia huo.

Hata hivyo, katika shauri hilo la maombi ya marejeo namba 748/01 la mwaka 2022, mahakama hiyo katika uamuzi imewakatalia maombi ya kuurejea uamuzi huo ikisema sababu zilizotolewa hazina mashiko.

Katika uamuzi huo uliotolewa na jopo la majaji watatu waliosikiliza shauri hilo, Rehema Mkuye (kiongozi wa jopo), Abraham Mwampashi na Zainabu Muruke, mahakama imesema sababu walizozitoa si miongoni mwa zile za kuomba mahakama kufanya marejeo ya hukumu yake, bali zinahusu rufaa.

Uamuzi huo ulioandikwa na Jaji Muruke kwa niaba ya jopo hilo, ulitolewa Agosti 5, 2024 na unapatikana katika tovuti ya Mahakama iitwayo Tanzlii.

PIA SOMA

- Jacqueline Mengi aendelea kudondokea pua rufaa, mahakama yaondoa maombi yake ya kutaka kuurudisha wosia
 
Kwa vile alikua mke halali, basi ndio apewe 99% ya mali za mzee Mengi, halafu 1% inayobaki wapewe wale watoto wakubwa wa marehemu kama waraka wake unavyosema!!! Feminist mna shida sana ya ubongo!!!
1% mbona nyingi ?

Mali zote angeweza kumuachia mbwa!

Angeweza kuzigawa kwa serikali. Hamjawahi kusikia marehemu mwenye watoto na mjane kaiachia serikali hospitali, shule na viwanja ? Hamjawahi ?

Urithi ni maamuzi ya marehemu.

The legal question is two fold:
1/ wosia ulikuwa wa ukweli au wa kufoji?
2/ kama ni wa ukweli, kuna warithi walioachwa kinyume cha sheria, mfano watoto wa kike na wana haramu ?

Vigezo hivyo vikitimia, mjane ana haki ya kudai 99%, au yote peke yake, kama ndivyo marehemu alivyotaka.
 
Alishindwa kutumia fursa mapema ,akae ale alicho nacho mbona anavyogombania aliyevipambania kafa kaviachaa yy Kwan ataishi milele mpk awe na tamaa na kusumbua watt wa marehemu badala awaache wale matunda ya baba Yao ..

Mahakama imemkata na jamii nayo pia imegoma kumuonea huruma malaya
 
Huyu mmama ndio anatoa taswira halisi ya hv viumbe na tamaa walonayo.

Imagine kamkuta Mengi yupo na mali zake lakini anakaza shingo kupewa percent kama walitafuta wote.

Binafsi huwa nafurahishwa sana na maamuzi ya mahakama kama haya dhidi ya wanawake wezi kama hawa.
 
Back
Top Bottom