JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Ruvuma imewaachia kwa dhamana wachungaji wawili James Michael Komba na Beatus Aron Mwambuchi wa mchungaji kanisa la TAG lililipo Lizaboni Manispaa ya Songea wanaotuhumiwa kwa kosa la uhujumu uchumi.
Akisoma hukumu ya maamuzi ya maombi ya dhamana ya watuhumiwa hao Hakimu mkazi wa mahakama hiyo Asha Waziri amesema watuhumiwa hao namba tatu na namba nne wanahaki ya kupata dhamana na mtuhumiwa namba moja Celestine Faustin Ntaganira Bijampola na Stella Anton Musabila, dhamana yao imekataliwa hivyo wataendelea kukaa ndani.
Watuhumiwa wote wana makosa 13 ikiwemo kosa namba moja la kumiliki genge la wahalifu na kufoji nyaraka mbalimbali, Mtuhumiwa namba moja Celestine Ntanganira anasimamia magari yanayobeba makaa ya mawe zaidi ya 400 na kumiliki miradi mbalimbali.
Leo Februari 28, 2025 ni mara ya pili kwa Celestine kupandishwa mahakamani huku wachungaji hao wawili wakipandishwa kwa mara ya kwanza kesi imeahirishwa mpaka Machi 6, 2025 kwa ajili ya kutajwa.