Umuamuzi huo umetolewa leo August 22,2024 mbele ya Jaji Mwenda wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha katika kesi namba 59630 ya mwaka 2024 kufuatia maombi yaliyopelekwa Mahakamani na Mpeleka maombi Isaya Ole Posi ya kuiomba ipime na kutazama kama amri ile ilikuwa halali au la hasha au kama ilitolewa na Mtu mwenye Mamlaka ya kisheria kufanya hivyo.
Wakili wa kujitegemea Peter Njau akimuwakilisha Mteja wake Isaya Ole posi amesema Mteja wake alikuwa Mwathirika wa kuondolewa katika eneo hilo jambo ambalo aliamua kwenda Mahakamani kupinga kitendo hicho.
MBWA WAMEANZA KUBWEKA
Updates
Akiongea kwenye Maria Space,
Isaya Ole Posi mkazi wa Ngorongoro aliyetajwa kwenye kesi hii kama alifungua kesi Mahakama Kuu Kanda ya Arusha amekanusha kuwa alipeleka maombi hayo
=============
###Maria Sarungi Tsehai###
🚨 TAHADHARI ‼️🚨
Hii kesi haieleweki ilifunguliwa lini na nani - isije ikawa danganya toto wamaasai warudi kwao alafu wiki ijayo tutasikia Feleshi huko mahakama ya Rufaa katupilia mbali maamuzi ya Mahakama Kuu ya Arusha!
Kuweni makini ndugu zetu
Tunachotaka sheria IFUTWE!
#StopMaasaiEviction
===================