Mahakama za mwanzo ziruhusiwe kupokea ushahidi wa kimtandao

Mahakama za mwanzo ziruhusiwe kupokea ushahidi wa kimtandao

HAKI KWA WOTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2022
Posts
2,783
Reaction score
2,396
Habarini,
Kwa sasa mahakama za mwanzo haziruhusiwi kupokea ushahidi wa kimtandao kama vile nalala za email,whatsapp,fax,nk hadi kuanzia mahakam za wilaya.

Sidhani kama hii ni haki kwa sasa hasa ikizingatiwa kwa sasa mawakili wanaruhusiwa kufana kazi mahakama za mwanzo.

Kuna jambo pia la uwasilishaji wa nyaraka za mahakama kama vile hati za wito ambapo zikiwasilishwa kwa njia ya mtandao ni nafuu zaidi na haraka kwani unakuta mtu yuko mwanza anadai 200,000/= na anayemdai yuko mtwara mahakama inamtaka mdai alipe msambaza nyaraka nauli ya kwenda nakurudi,posho,kiapo,hela ya kazi,nk ili kupeleka wito kitu ambacho ni ghara sana na watu wengi hawamudu.

Kama mahakama imeamua kufanyakazi kimtandao basi ushahidi wa kimtandao ukubalike pia mahakama ya mwanzo ili kupunguza gharama na kuharakisha kesi.
Nawasilisha!
 
Back
Top Bottom