Mahakama za Tanzania ni tatizo au Serikali imekosa mwelekeo?

Kesi ya yule mama kule Iringa aliyekutwa na vipande vya vyama pori ukilinganisha na kesi ya mwamba mmoja kule Kanda ya ziwa aliyekutwa na silaha za kuua wanyama pori ziliivua nguo mahakama ya Tanzania.
Makonda sio kwamba ana akili Sana, Ila watu wa chini wameona Ni Bora kwenda kutafuta haki kwa makonda kuliko mahakamani.
Mahakama ingekua chombo kinachotoa haki, hizi kangaroo court za michongo za Makonda tusingeziona.
 
Sidhani kuwa, ni kweli. Kazi za ujaji huwa hawaombi wanateuliwa na Rais. Kaz za uhakimu ndio wanaomba na kufanya interview.
 
Tanzania hakuna mahakama,bali Majengo yenye jina la mahakama.Majaji na mahakimu ni vilaza wa kutupwa.

Mtu kama Biswalo ni Jaji,hiki ni kichekesho.
Majaji sio wote vilaza.
Kuna majaji waliojijengea heshima kubwa Sana. Kina jaji Kisanga, majaji waliomtanguliza Mungu mbele.
Ila Kuna Hawa wengine wanaopewa kesi za michongo, Hawa hawana maadili, kiapo waliapa bure tu, wanaumiza watu kisa V8.
Ukiangalia utakuta MTU anaupata ujaji akiwa 50+ years. Hivi huyu hata serikali au fisadi amhonge bilioni atazifaidi lini huku ana changamoto ya presha, kisukari na nguvu za kiume?
Tumrudie Mungu jamani dunia Ni mapito tu. Unamtesa MTU halafu baada ya miaka Saba, umestaafu. Inakusaidia Nini?
 
Mahakama na bunge zote zimeoza.hii mihimili Bora ifutwe ubaki mihimili wa rais.mihimili yote hii inafanya kazi kulingana na mhimili wa urais unavyotaka hata kama ni mambo ya hovyo.
 
Kaitukana vipi? Onyesha hilo tusi.
 
it's true tuna tatizo na mfumo wetu wa utoaji haki.
Ukiangalia pia kesi ya akina Mbowe (ya ugaidi) ilivyokuwa ikienda, iliweza pia kuleta maswali ya kujiuliza.
True

Naunga mkono hoja ubarikiwe sana
P
 
Kaitukana vipi? Onyesha hilo tusi.
Huyo Chiembe ndiyo huyo Jaji aliyetajwa na Silaa,jiwe gizani limempata hadi kakurupuka usingizini!![emoji23][emoji23][emoji23]
 
Sidhani kuwa, ni kweli. Kazi za ujaji huwa hawaombi wanateuliwa na Rais. Kaz za uhakimu ndio wanaomba na kufanya interview.
Yea upo sahihi ni hakimu. Kwani jaji si kiingereza au
 
Shidaa jaji mkuu anaamini sana hizi mahakama za chini yaan kumeoza mbaya kuna kesi tulikuwa nayo pale moshi yaan utapeli wa wazi kila ukifika kalenda kalenda tukaenda Dodoma na barua tukaelekezwa kwa jmfawidhi gafla. Tukaitwa kesi inamalizika...huku cijui mahakama za mwanzo nk kuna mashetani na majini kazi akufai

Mbaya mtu akiona anashindwa anakimbilia kwa mawakili sasa wale ukikuta hakimu.legevu mnalia so wakati mwingine mkiona usumbufu kasanuen andiken barua peleken Dodoma copy takukuru simple
 
Mahakama za Tanzania ni AIBU TUPU. zimemfanya mpaka yule MHALIFU Daud Bashite aka Paul Makonda aonekane ni wa maana. Majaji na Mahakimu mnasoma hapa JISIKIENI AIBU

Mtu ZEROBRAIN, Cheti FEKI cha Form IV lakini anafuatwa na wananchi akatatue kero zao. Yote hii IMESABABISHWA NA mahakama kukosa maadili na kuwa wapokea RUSHWA
 
jana waziri wa ardhii kaweka live kuna jajii kateuliwa ana saponins wizi wa viwanja kwa tapeli mmoja mfanyabiashara

Waziri kaenda mbali kasema hii kesi kainunua na atahakikisha wanarudisha mali za watu

Ajabu
Jaji huyohuyo alikuwa n wakili wa kisheria anaemsaidia hiy tapeli kabla ajateuliwa jaji

sasa ndie aliemsaidia kupora baadhi ya malizawatu kwenda kwa huyutapeli
 
Vetting kwa baadhi ya teuzi haizingatii vigezo........ ndiyo maana kuna gape kubwa kwenye baadhi ya nafasi ikiwemo Mahakama
 
Hii nchi inahitaji factory reset. Chama kilichoko madarakani kwa muda wote hapa nchini ndio sababu hasa ya mahakama kukosa meno. Wao ni wafaidika wakubwa wa udhaifu wa mahakama, na mamlaka ya urais yametumika sana kuharibu uhuru wa mahakama.

Hawa viongozi wa ccm wanaojifanya kuigiza kuwa wanaona mahakama haitendi haki, usishangae hata wao wasiwe tayari kuona mahakama kufanya kazi yake kwa uadilifu pindi mahakama ikiwa dhidi Yao. Hizo mahakama zilitumika waziwazi wakati wa Magufuli kufunga wapinzani kwa maagizo yake. Katika mazingira hayo ni kama mahakama ilipoteza uwezo wake wa kutoa haki.
 
Mahakama na bunge zote zimeoza.hii mihimili Bora ifutwe ubaki mihimili wa rais.mihimili yote hii inafanya kazi kulingana na mhimili wa urais unavyotaka hata kama ni mambo ya hovyo.
Kweli kabisa, nikimuona mwanaccm yoyote analaumu udhaifu wa mahakama namuona kama ni mnafiki tu, maana wao ni sehemu ya wafaidika wa huo udhaifu wa mahakama.
 

Practically, mimi nadhani mahakama hupokea kesi ktk categories mbili;

1. Kesi zenye uhusiano na watawala;
Mfano kesi za kupinga matokeo ya uchaguzi, kesi ambazo ndani serikali ina maslahi ndani yake e.g hii ya kina Halima Mdee a.k.a COVID-19.
Kwa kesi za namna hii hufanyika mambo mawili wa ama maamuzi (hukumu) kutolewa haraka lakini sheria ikipindishwa kuipendelea serikali au kiongozi fulani wa serikali au shauri kupigwa danadana tu mahakamani miaka na miaka kwa kisungizio cha hiki au kile..

2. Kesi ambazo serikali haina maslahi nazo na mara nyingi ni kati mtu na mtu, taasisi na taasisi, mtu dhidi ya taasisi na zile za jinai zote;
Kesi hizi huwa chini ya jaji au hakika. Ni yeye huamua ahukumu kwa haki au la. Mara nyingi, hukumu ya haki huweza kupindishwa kama hakimu/ Jaji atakuwa under the influence of bribe or corruption from one side kwa kusudi la kupata upendeleo..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…