Mahakamani kuna siri gani? Niliwahi kwenda kwa Mganga wa Kienyeji ili Hakimu na mashahidi washindwe kuongea au kuzungumza Mahakamani

Uongo wa kiwango cha Juu, hawakukumbuki wewe kabisa, Ila kuna records, kuna arrest order Na wewe ulichagua option two!

Uongo narudia tena uongo! Kuna watu Wenye fedha nyingi wamefungwa life time and mganga angekuwa an easy option!

Hakuna Mganga anayeweza kufuta Kesi, simply hayupo, Na hawa Ma police Nina uhakika wana fungu la kujiweka Sawa!

Uongo uongo uongo Na uzandiki
Katika maisha huwezi kujua Kila kitu Mkuu. Kwa hiyo usijione unajua yanayotokea Kila mahali. Tumeshuhudia Nyukj wakivamia Mahakama Kila siku kesi Fulani inaposikilizwa na kulazimika kuahirishwa. Uliza watu wa Wanging'ombe Njombe au Nkasi Rukwa Wana visa viwili vinavyofanana.
 
Jinai haifi hata hao Askari wakihama record zinabaki majalada wanakua nayo siku kamzizi kakiisha utashangaa unakuja kukamatwa na askar mwngne kabisa ambae humjui kashakabidhiwa jalada lako
 
Mkiona mtu kateuliwa kuwa jaji /hakimu basi mnasema kala shavu hivi najuwa wanayoyapitia.

Kuna dada mmoja alinisimulia mme wake alifungwa kwa kesi ya magendo na dawa za kulevya walimkamata navyò.kaswekwa ndani muda ukapita. Eti kuna mtu akamwambie aende kwa mganga wamtengeneze hakimu siku ya hukumu asikumbuke chochote.

Sasa huko alokwenda kwa mganga mambo walofanya naogopa hata kuandika hapo. Mimi siwezi fanya hicho kitu hata kama mme nampenda kiasi hicho bora nihonge pesa tu.

Alienda kwa mganga wakafanya waliyofanya siku ya hukumu dada huyo mahakamani anamiona mme wake , pale mahakamani kuna dawa nayo aliweka.

Eti wakati wa hukumu hakimu akasema " huyu nae bado huko hapa kesi yake haina mashiko na aondoke atakuwa anakuja kureport hapa kila siku😂😂😂 mwanaume akatoka na kesi ya madawa ikaishia hapo.

Ilikuwaje huyo dada akanisimulia? Siku moja akawa anamuongelea mme wake eti tangu waachane hajawahi fanikiwa eti au ni maneno alomwambia wakati wanaachana?

Huyo dada anasema baada ya mme wake kuachiwa, wakarudi nyumbani baada ya miezi 7 akamfumania na rafiki yake ndo chanzo cha kuachana.

Sasa anasema wakati anaondoka na watoto wake alimwambi mmewe haya maneno, " wewe mwanaume kwa sababu yako nilienda kwa mganga nikafanya vitu ambavyo sikuwahi fanya ili utoke jela unawezaje kulala na rafiki yangu kitandani kwangu? Hutokaa ufanikiwe" akaondoka na watoto. Anasema mpaka leo mmewe hana hata mia.

Mimi kila siku nakuwa mahakamani nachekaga sana. Kwenye milango ya kuingia mahakamani wanasema ndo watuhumiwa/ ndugu za washitakiwa ndo wanawekaga madawa.hayo madawa yanawalenga mahakimu/ majaji wala sio sisi watu wa kawaida.uchawi upo.
Mahakama za saivi za kisasa mno sababu majaji na mahakimu wanaingia kwenye milango tofauti na watu wengine
 
NA wewe unaamini kwamba anaumwa? Kwanini shahidi wa 14 hayupo na haeleweki lini atakuja? Huoni kama hili jambo lipo so calculated? Bro acha kujidanganya, yeyote mwenye akili timamu anajua pale mahakamani kwa kesi ya Mbowe ni maelekezo, maigizo tu unless hufikirii vizuri (hili la kufikiria vizuri, sio ujumbe wako, ni kwa mtu anaedhani ili kitu ni kweli while maigizo ). Ujumbe wako kuhusu mambo ya kamati una ukweli kwa 100% but sio kwa issue hi ya Mbowe, again hivi unawajua maofisa wengi wa serikali? Wale hawalogegi, wanao wazee wao wanawalinda full time, usijidanganye eti unaweza waendea kwa waganga wale
Watu hawa walogi hakimu ili kumzuru ila Wana mloga ili hasi mfunge mtuumiwa awe huru
 
Wanabodi,

Nayaandika haya sio kwa kufurahisha bali ni mambo yaliyonikuta na sitaki kuyakumbuka kabisa lakini kwa yaliyomtokea shahidi namba 13 wa upande wa jamuhuri Kamanda Swilla kwa kuugua ghafla kizimbani na muda mwingi kuomba ruhusa kwenda washroom au maliwato siyo mambo ya kucheka huwa yanatokea.

Mwaka 2005 Katika purukushani za uchaguzi na kikiri kakala za hapa na pale nilishtakiwa mahakamani kwa kosa ya matumizi mabaya ya pesa yaani rushwa na kuharibu kumbukumbu za ushahidi.

Kwa kuwa Mimi Gussie ni Mkinga automatic Rafiki zangu wengi ni wakinga hivyo kwa kuwa kuna mambo mengi tunasimuliana nikaona isiwe shida kuomba msaada wa ushauri kwa wakinga wenzangu kuhusu kesi inayonikabili Mahakamani.

Wakinga wenzangu Walinipa machaguo mawili

1. Kuifuta kesi kwa njia ya giza yaani mafaili na kumbukumbu zote kwenye Kompyuta na Polisi zipotee kabisa na hata jina langu lisionekane kabisa

2. Watu walionishtaki wakiniona wanikimbie sehemu yeyote ili au washindwe kuzungumza kitu mbele yangu na mahakamani

Mimi nilichagua chaguo namba mbili kwani hawa watu walionishtaki Nilitaka hata Ikifika uchaguzi mwingine waniogope na kunikimbia kila wakiona sura yangu au Uwepo wangu au washindwe kuongea mbele yangu

Nilisafiri toka Dar es Salaam mpaka Mbeya kuelekea Malawi huko kwa Mganga wa Kienyeji, Mganga alinipatia chupa ndogo ukubwa wa chupa ya glycerine yenye mafuta ndani yake na yenye vipande vidogo dogo vya miti ndani yake pamoja na unyoya sijui unyoya wa ndege gani sikumuuliza Mganga, huu unyoya ulikuwa ndani ya hicho chupa unaelea elea tu.

Mganga huyu wa Malawi pia alinikabidhi leso ndogo ambayo kona moja ameifunga ndani ya sehemu aliyofunga sikujua aliweka dawa gani, na Mimi sikuuliza

Kazi ya mafuta ilikuwa pale ninapoenda polisi najipaka kidogo tu usoni au kwenye paji la uso na kuongea maneno ninayotaka mimi mwenyewe, Siku niliporudi tu nikaelekea polisi kwa confidence kabisa kwani walikuwa wananitafuta sijaonekana Mahakamani na wala sijaripoti kwao Polisi, Mimi kabla ya kufika Nilitamka kuwa polisi wa Uchunguzi wanisahau kabisa.

Kweli nilipofika tu polisi, kila polisi pale kituoni alikuwa ananiuliza umekuja kufanya nini hapa, Moyoni nikawa nawaza ni hawa hawa au Wengine. Mwisho wa siku niliamua kuaaga mwenyewe na kurudi zangu nyumbani kwani hakuna polisi aliyenikumbuka au kushughulika na Mimi.

Niliamua kurudi tena pale polisi siku ya pili kwa kutumia ile leso niliyopewa ambayo niliambiwa kazi ya ile leso ni kufukuza nuksi na lolote baya juu yangu, Nilitakiwa kuweka ile leso mfukoni mahala popote kama nikihisi kutakuwa na tatizo au naenda kuonana na mpinzani au adui yangu au mtu yeyote aliye kinyume na malengo yangu, Kumbuka hii ni leso ya kawaida isipokuwa kwenye kona moja tu ndio imefungwa dawa kwa ndani ambayo sijui, Kwa kutumia hii leso pia natakiwa "kunuia" kwa lugha ya kiganga au natakiwa kusema lile ninalotaka lifanyike kwa wakati wowote ule kwa kuigusa leso mfukoni mwangu.

Nikiwa karibu na kituo cha polisi niliigusa leso yangu na kutamka wale wote polisi wanoko walionikamata na kunichunguza naomba wahamishwe kazi pale kituoni kwani wao ndio walikuwa vimbelembele kunisumbua, Nikaingia kituoni counter na kuwaulizia kama wapo nikawakuta, Nikaanza kuwaulizia kuhusu kesi yangu nikaona kila mmoja anamtupia Mwenzake mpira kuwa tuyamalize yaishe huku wakitaka mimi niondoke pale kituoni nirudi nyumbani, Wakanisihi wale polisi basi niwatafuta jioni tuyaongee kwani Mimi wakati huo nilikuwa nafahamika baadhi ya Pub nikila bata, Nikawaambia niwatafuta kesho.

Mambo yalibadilika badala ya polisi kuendelea kunitafuta Mimi, Ikawa mimi ndio nawafuatilia wao ili kujua mwisho wa kesi, Siku iliyofuata wale polisi walinipigia simu wamehamishwa kabisa Mkoa na kutupwa mikoa tofauti.

Baada ya hawa polisi kuhamishwa na hali kupoa kidogo, Nikasafiri tena kuelekea huko Malawi kwenda kutoa report na hatua iliyofikiwa, Kumbuka hizi connections zote za huko ni Mwanamke ndie aliyeniunganishia mpaka Malawi huko hivyo akawa sio rafiki tu ila zaidi ya Rafiki maana hakuna siri ambayo nilikuwa namficha hivyo alinijua ndani nje huyo Mwanamke, Na yeye alifika huko Malawi na kukufahamu huko huyo Dada baada ya watu kumroga akawa ana bleed kila siku karibu miezi mitano bila nafuu mpaka anaongezewa damu mwilini hivyo alidhoofu sana ni kutokana na yeye kuwa na mahusiano na Mume wa Mtu, Aliponea huko Malawi.

Baada ya kukamilisha shukrani huko Malawi, Nikauliza nini mwisho wa yale mafuta na ile lesso, Niliambiwa yale mafuta yakipungua niwe naongeza mafuta ya kawaida tu ya kupikia nayatikisa na kutumia kupaka pale nitakapohitaji kuyatumia

Ishu ya polisi ikawa imeisha sasa ikabaki ishu ya Mahakamani kujua mambo yamekaa vipi huko kwani tayari wambea wameshahamishwa vituo vya kazi hawapo tena

Ishu ya Mahakama Nikaamua kuelekea huko kwetu Ukingani, Nikaelezea hatua niliyofikia na nini kimebaki, Huko kwetu ndio nilikutana na funga kazi ya mwaka, Nilipewa dawa kamzizi kana urefu kama njiti ya kiberiti lakini kanene kidogo, Hiyo dawa kimatumizi haitofautiani sana na zile za Malawi kwani nayo lazima unuie yaani utamke maneno utakavyo nini kifanyike. Wazo langu hapa likanijia kichwani niwafanye watu wa mahakama kuanzia hakimu na Wengine wawe Mabubu yaani washindwe kuongea

Kujaribu uwezo wa huo mzizi kwanza kabla ya kufika kwa pilato yaani Mahakamani Nilitamka nipande gari bure toka Makete huko mpaka Dar bila kulipa nauli njiani, Wakati huo kulikuwa hakuna gari ya moja kwa moja toka Makete mpaka Dar es Salaam, Nilipanda gari toka Makete mpaka Njombe bure kabisa,

Nilifika kwa konda Nikamwambia sina nauli naomba msaada akajifanya kama anataka kuchomoa hivi mara paap akalainika kama bigijii na kwenda mwenyewe kunichukulia ticket kwa Wadada wanaokatisha sijui aliwaambia kitu gani, Nilifika Njombe usiku Nikaamua kutafuna tena kale kamzizi ili nilale guest pale bure kabisa pale Njombe nikisubiri ifike asubuhi nielekee Dar, Baada ya kufika Guest nikamkuta Dada kaunta Nikamwambia Nahitaji chumba lakini sina pesa ya kulipa, Dada akajibu hakuna chumba vimejaa, Nikamwambia sasa tunafanyaje mara paap akalainika kama bigijii akapiga simu guest inayofuata akaongea nao nikalala guest hiyo nyingine bure kabisa bila kulipa kitu

Nitaendelea tena baadae kuelezea

Wale wapambanaji hawawezi kushangaa ninachokisema hapa, Hakuna maisha ya mteremko hapa duniani you have to fight
Duh!!..
 
Kama uchawi tunaamini upo unadhani mahakama na mahakimi ni spesho kutologeka? Uchawi upo kila mahala ubishi wa nini
uchawi upo kila mahali, hata mahakimu wengi tu wachawi na washirikina. tunachosema ni kuhusu kuroga kesi, hilo huwa halifanikiwi kwa uzoefu wangu. hata urogeje kesi huwa haifi hivihivi.
 
Daah kwamba salamu Maria na rozali unakun'gutwa na kufa

Unaushuhuda juu ya hili?
kama ulishawahi kuomba kwa salamu maria umejaa neema, ukapata majibu yaliyothibitika, nyosha mkono juu. au kama uliwahi kuomba kwa lozari ukapata majibu. tunaomba kwa Jina la Yesu Kristo pekee. mambo ya kuomba kwa maria na lozari pamoja na kwamba yalikuwa introduced baadaye kabisa na watu wanaoabudu kimwili, lakini mlikuja kujidanganya kwa mzimu uliowatoto wa Fatima, kwamba mzimu wa maria uliwatokea ukawaagiza wasali kwa lozari. maria kafa na hana communication na dunia hii, anasubiri kuhukumiwa siku ya mwisho. hicho kilichowatokea hakikuwa na uhusiano na Mungu ni shetani aliendelea kuwadanganya ili muendelee kusali kwa salamu maria na rozali.

mitume wale 12 hata kina Paulo walioanzisha ukristo, hakuna hata mmoja aliwahi kusali salamu maria au hata kumtaja tu. hakuna hata mmoja aliwahi kusali rozali. kama ni msomaji wa Biblia tutajie wapi wale mitume kina Petro Yohana etc waliposali kwa maria au rozali? au kuelekeza wafuasi wa Kikristo kufanya hivyo. hakuna, Yesu Kristo alituagiza tusali kwa kupitia Jina lake, ukiomba Kwa Jina la Yesu utapata majibu. Mungu hakusikilizi kabisa kama hautaomba kwa kupitia Jina la Yesu kwasababu Yesu Kristo ndiye kafara/daraja kati yetu na Mungu baba. huu ndio ukweli mchungu na shukuru Mungu umeusikia. I challenge you, nenda kamwulize padre au askofu yeyote a catholic asema wapi kwenye Biblia kuna kusali kwa maria, kuomba maria atuombee, kusali kwa lozari.

hii ni invention ya watu kimwili kwamba ati kwasababu maria ndio alimzee Yesu basi tumheshimu mama kabla hatujamheshimu mtoto, hamjui kuwa Yesu Kristo alikuwepo kabla ya maria na ibrahimu na Musa na wote? Yesu Kristo ndiye lile Neno lililotumika katika uumbaji tangu enzi na enzi haina mwanzo wala mwisho. kuja duniani kupitia maria ilikuwa ni njia tu ya kufanyika mwili wa kibinadamu ili abebe dhambi za dunia na kulipa gharama ya dhambi kwa mateso makubwa aliyopitia. hata baba wa duniani hapa hakuwepo, yeye alifanyika reincanation (spirit changing wearing human body) kwa kuuvaa mwili wa kibinadamu, ayashinde yote ya dunia, ateswe kwa ajili yetu ili kutukomboa. hata kumwona Mungu tunaokoka kwa kumkiri na kumwamini Yesu Kristo, maria tupa kule.
 
Ndio maana unaona mtu hajasoma ila ana cheo kikubwa. Hakimu akijifanya mjanja, siku ya kesi ni mwendo wa kuharisha kama kipindupindu!! Hii ndio Dunia usiyoifahamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
matukio ayo ni machache sana, na yanawapata wale wasio na Mungu tu. nina uzoefu wa Mahakamani wa zaidi ya 11 yrs, ni incident moja tu nilishuhudia mahakimu na majaji wamedhurika. nayo ilikuwa hapo kisutu. nao najua ni kwasababu pengine walitegemea waganga na hawakuwa na Mungu moyoni. ukiw ana Yesu moyoni, hakuna uchawi wala uganga utakaofanya kazi.
 
Wanabodi,

Nayaandika haya sio kwa kufurahisha bali ni mambo yaliyonikuta na sitaki kuyakumbuka kabisa lakini kwa yaliyomtokea shahidi namba 13 wa upande wa jamuhuri Kamanda Swilla kwa kuugua ghafla kizimbani na muda mwingi kuomba ruhusa kwenda washroom au maliwato siyo mambo ya kucheka huwa yanatokea.

Mwaka 2005 Katika purukushani za uchaguzi na kikiri kakala za hapa na pale nilishtakiwa mahakamani kwa kosa ya matumizi mabaya ya pesa yaani rushwa na kuharibu kumbukumbu za ushahidi.

Kwa kuwa Mimi Gussie ni Mkinga automatic Rafiki zangu wengi ni wakinga hivyo kwa kuwa kuna mambo mengi tunasimuliana nikaona isiwe shida kuomba msaada wa ushauri kwa wakinga wenzangu kuhusu kesi inayonikabili Mahakamani.

Wakinga wenzangu Walinipa machaguo mawili

1. Kuifuta kesi kwa njia ya giza yaani mafaili na kumbukumbu zote kwenye Kompyuta na Polisi zipotee kabisa na hata jina langu lisionekane kabisa

2. Watu walionishtaki wakiniona wanikimbie sehemu yeyote ili au washindwe kuzungumza kitu mbele yangu na mahakamani

Mimi nilichagua chaguo namba mbili kwani hawa watu walionishtaki Nilitaka hata Ikifika uchaguzi mwingine waniogope na kunikimbia kila wakiona sura yangu au Uwepo wangu au washindwe kuongea mbele yangu

Nilisafiri toka Dar es Salaam mpaka Mbeya kuelekea Malawi huko kwa Mganga wa Kienyeji, Mganga alinipatia chupa ndogo ukubwa wa chupa ya glycerine yenye mafuta ndani yake na yenye vipande vidogo dogo vya miti ndani yake pamoja na unyoya sijui unyoya wa ndege gani sikumuuliza Mganga, huu unyoya ulikuwa ndani ya hicho chupa unaelea elea tu.

Mganga huyu wa Malawi pia alinikabidhi leso ndogo ambayo kona moja ameifunga ndani ya sehemu aliyofunga sikujua aliweka dawa gani, na Mimi sikuuliza

Kazi ya mafuta ilikuwa pale ninapoenda polisi najipaka kidogo tu usoni au kwenye paji la uso na kuongea maneno ninayotaka mimi mwenyewe, Siku niliporudi tu nikaelekea polisi kwa confidence kabisa kwani walikuwa wananitafuta sijaonekana Mahakamani na wala sijaripoti kwao Polisi, Mimi kabla ya kufika Nilitamka kuwa polisi wa Uchunguzi wanisahau kabisa.

Kweli nilipofika tu polisi, kila polisi pale kituoni alikuwa ananiuliza umekuja kufanya nini hapa, Moyoni nikawa nawaza ni hawa hawa au Wengine. Mwisho wa siku niliamua kuaaga mwenyewe na kurudi zangu nyumbani kwani hakuna polisi aliyenikumbuka au kushughulika na Mimi.

Niliamua kurudi tena pale polisi siku ya pili kwa kutumia ile leso niliyopewa ambayo niliambiwa kazi ya ile leso ni kufukuza nuksi na lolote baya juu yangu, Nilitakiwa kuweka ile leso mfukoni mahala popote kama nikihisi kutakuwa na tatizo au naenda kuonana na mpinzani au adui yangu au mtu yeyote aliye kinyume na malengo yangu, Kumbuka hii ni leso ya kawaida isipokuwa kwenye kona moja tu ndio imefungwa dawa kwa ndani ambayo sijui, Kwa kutumia hii leso pia natakiwa "kunuia" kwa lugha ya kiganga au natakiwa kusema lile ninalotaka lifanyike kwa wakati wowote ule kwa kuigusa leso mfukoni mwangu.

Nikiwa karibu na kituo cha polisi niliigusa leso yangu na kutamka wale wote polisi wanoko walionikamata na kunichunguza naomba wahamishwe kazi pale kituoni kwani wao ndio walikuwa vimbelembele kunisumbua, Nikaingia kituoni counter na kuwaulizia kama wapo nikawakuta, Nikaanza kuwaulizia kuhusu kesi yangu nikaona kila mmoja anamtupia Mwenzake mpira kuwa tuyamalize yaishe huku wakitaka mimi niondoke pale kituoni nirudi nyumbani, Wakanisihi wale polisi basi niwatafuta jioni tuyaongee kwani Mimi wakati huo nilikuwa nafahamika baadhi ya Pub nikila bata, Nikawaambia niwatafuta kesho.

Mambo yalibadilika badala ya polisi kuendelea kunitafuta Mimi, Ikawa mimi ndio nawafuatilia wao ili kujua mwisho wa kesi, Siku iliyofuata wale polisi walinipigia simu wamehamishwa kabisa Mkoa na kutupwa mikoa tofauti.

Baada ya hawa polisi kuhamishwa na hali kupoa kidogo, Nikasafiri tena kuelekea huko Malawi kwenda kutoa report na hatua iliyofikiwa, Kumbuka hizi connections zote za huko ni Mwanamke ndie aliyeniunganishia mpaka Malawi huko hivyo akawa sio rafiki tu ila zaidi ya Rafiki maana hakuna siri ambayo nilikuwa namficha hivyo alinijua ndani nje huyo Mwanamke, Na yeye alifika huko Malawi na kukufahamu huko huyo Dada baada ya watu kumroga akawa ana bleed kila siku karibu miezi mitano bila nafuu mpaka anaongezewa damu mwilini hivyo alidhoofu sana ni kutokana na yeye kuwa na mahusiano na Mume wa Mtu, Aliponea huko Malawi.

Baada ya kukamilisha shukrani huko Malawi, Nikauliza nini mwisho wa yale mafuta na ile lesso, Niliambiwa yale mafuta yakipungua niwe naongeza mafuta ya kawaida tu ya kupikia nayatikisa na kutumia kupaka pale nitakapohitaji kuyatumia

Ishu ya polisi ikawa imeisha sasa ikabaki ishu ya Mahakamani kujua mambo yamekaa vipi huko kwani tayari wambea wameshahamishwa vituo vya kazi hawapo tena

Ishu ya Mahakama Nikaamua kuelekea huko kwetu Ukingani, Nikaelezea hatua niliyofikia na nini kimebaki, Huko kwetu ndio nilikutana na funga kazi ya mwaka, Nilipewa dawa kamzizi kana urefu kama njiti ya kiberiti lakini kanene kidogo, Hiyo dawa kimatumizi haitofautiani sana na zile za Malawi kwani nayo lazima unuie yaani utamke maneno utakavyo nini kifanyike. Wazo langu hapa likanijia kichwani niwafanye watu wa mahakama kuanzia hakimu na Wengine wawe Mabubu yaani washindwe kuongea

Kujaribu uwezo wa huo mzizi kwanza kabla ya kufika kwa pilato yaani Mahakamani Nilitamka nipande gari bure toka Makete huko mpaka Dar bila kulipa nauli njiani, Wakati huo kulikuwa hakuna gari ya moja kwa moja toka Makete mpaka Dar es Salaam, Nilipanda gari toka Makete mpaka Njombe bure kabisa,

Nilifika kwa konda Nikamwambia sina nauli naomba msaada akajifanya kama anataka kuchomoa hivi mara paap akalainika kama bigijii na kwenda mwenyewe kunichukulia ticket kwa Wadada wanaokatisha sijui aliwaambia kitu gani, Nilifika Njombe usiku Nikaamua kutafuna tena kale kamzizi ili nilale guest pale bure kabisa pale Njombe nikisubiri ifike asubuhi nielekee Dar, Baada ya kufika Guest nikamkuta Dada kaunta Nikamwambia Nahitaji chumba lakini sina pesa ya kulipa, Dada akajibu hakuna chumba vimejaa, Nikamwambia sasa tunafanyaje mara paap akalainika kama bigijii akapiga simu guest inayofuata akaongea nao nikalala guest hiyo nyingine bure kabisa bila kulipa kitu

Nitaendelea tena baadae kuelezea

Wale wapambanaji hawawezi kushangaa ninachokisema hapa, Hakuna maisha ya mteremko hapa duniani you have to fight
Ila haya mambo yapo nafahamu ,ila wagaga wa bongo wengi magumashi sana

sent from HUAWEI
 
yanatokea ila yanafanikiwa kwa nadra sana. yangekuwa yanafanikiwa, kwa namna kesi zilivyo nyingi, namna watu wanavyotafuta hela kuhonga hakimu au jaji au kuajiri mawakili, wangeenda tu kwa mganga angemaliza kila kitu. waganga wangekuwa na pesa/wateja wengi. wala msitegemee ujinga huo.mtaliwa hela na mtaenda gerezeni.
 
Back
Top Bottom