Amani Msumari
JF-Expert Member
- Aug 21, 2016
- 1,833
- 979
Watanzania wenzangu, ninawasalimu kwa jina la Tanzania.
Awali ya yote ninapenda kuchukua fursa hii kuwapongeza watanzania wote kwa kushiriki uchaguzi mkuu kwa amani. Hongereni sana.
Dhumuni la bandiko langu ni kuwakumbusha ndugu zangu watanzania kuhusu umuhimu wa amani kutawala nchini na kuwakumbusha kuwa makini dhidi ya wanasiasa uchwara ambao wanahubiri vurugu. Vurugu hazitatuacha salama na tutalia kilio ambacho hatakuwepo wa kutupangusa machozi.
Msimamo Wangu
Msimamo wangu ni kuwa siungi mkono dhuluma dhidi ya kundi lolote lile. Siungi mkono uonevu dhidi ya upinzani. Siungi mkono ubakwaji na ubinywaji wa demokrasia. Siungi mkono mauji dhidi ya raia popote duniani. Naunga mkono utawala wa demokrasia. Naunga mkono amani na utulivu. Zaidi sana, natambua kuwa amani na utulivu ni tunda la haki.
Maandamano yenye lengo la amani yakikatazwa na vyombo vya dola hayawi tena maandamano ya amani
Inashangaza sana kuona wanasiasa uchwara wakihimiza watu waandamane hata pale vyombo vya ulinzi na usalama vinapokataza. Ninashangaa kwani wanasiasa hao wanajua fika ni jambo gani linaloenda kutokea.
Kuna sababu nyingi za kukataza maandamano yenye lengo la amani. Sababu hizo zinaweza kuwa za msingi au za kipuuzi, Ila katika yote, muhimu ni matokeo ya maandamano hayo. Huwezi kusema maandamano ni ya amani halafu mwisho ukaishia kuua watu.
Wanasiasa mara nyingi wanalenga maslahi yao. Huwezi kuwakuta wake zao wala watoto wao kwenye hayo maandamano. Hii inaashiria ubinafsi mkubwa na kuwatumia watu wa hali ya chini kama ngazi zao za mafanikio ya kisiasa.
Rejeeni mifano ya Burundi, Zimbabwe, DR Congo, Libya, Tunisia n.k.
Mwanasiasa yeyote yule anayeshabikia nchi yake kuwekewa vikwazo ni msaliti mkubwa
Mwanasiasa mwenye dhamira ya kuona watu wake wanafanikiwa ni yule ambaye atafanya kila awezalo kuhakikisha watu hao wanataka mafanikio. Wanasiasa wanajua kuwa nchi ikiwekewa vikwazo hasa vya kiuchumi, wanaoumia sio viongozi bali wananchi.
Ukimuona mwanasiasa anaomva nchi iwekewe vikwazo kisa maslahi yake yamebanwa, jua huyo hana mapenzi mema na watu anaosema anawapigania. Huyo anapigana tumbo lake.
Katiba ya Tanzania na sheria zetu za uchaguzi zinasemaje?
Kwa ufupi, bila kujali mazingira yoyote (rejea: sio kuathiri mazingira ya vifungu vingine vya sheria) ni kuwa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi akishamtangaza mgombea kuwa mshindi ni kuwa ushindi huo ni halali na hauhojiwi na mahakama yoyote.
Wapinzani walishiriki kwenye uchaguzi wakijua hilo. Katiba na sheria za Marekani na Uingereza nazo zina Mambo yake. Electoral college ndio waamuzi wa mwisho hata Kama rais amepata kura nyingi za wananchi wa kawaida. Uingereza malkia/mfalme ndio mkuu wa nchi na dini ya anglikana. Hii haijalishi Kama kuna waingereza wa dini nyingine.
Watanzania tuchape kazi.
Amani