Mahali pote duniani, wanasiasa uchwara ndio chanzo cha machafuko nchini mwao, Watanzania tuwe makini

Mahali pote duniani, wanasiasa uchwara ndio chanzo cha machafuko nchini mwao, Watanzania tuwe makini

Umejitahidi kujificha upande uliopo ila bado inashindikana je suluhu ya dhulma iliyotokea ni nini halafu Electoral College ni nini na kwa hapa bongo inapply?
 
Baada ya chaguzi kuu 6 za vyama vingi tangu 1995 na kuona matokeo yake ninaweza kusema na kushauri yafuatayo:
1. Tanzania ililazimishwa kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi. Chama cha Mapinduzi hakikuwa tayari, hakiko tayari na hakitakuwa tayari kuondoka madarakani kwa njia za kawaida za ushindani wa kisiasa. Chama hicho kimejichimbia mizizi katika mifumo yote ya kisiasa, kiserikali, kifedha na kiusalama kuhahikisha kinabaki madarakani kwa njia yoyote ile. Huwezi kushiriki kufanya siasa za ushindani katika mazingira ya namna hii.
2. Hata pale upinzani unapoonekana kuwa na nguvu kiasi chake, kama ilivyokuwa kwa NCCR-Mageuzi (1995-2010), CUF (Zanzibar), Chadema (2005-2020), nguvu hiyo au uhuru huo ni kutokana na kudra za mkuu wa nchi. Bila shaka upinzani ulishamiri enzi za awamu ya Kikwete kwa sababu mzee huyu kwa asili yake ni mwanadiplomasia anayeamini katika falsafa ya give and take, na si mtu wa shari. Hii personality ya Kikwete sio wote watakuwa naye -- na kwa mtu kama JPM ambaye kwake suala la kuongoza nchi si mchezo wa kuigiza, mtu asiyetaka ujinga ujinga na ubishi ubishi kwenye visions zake, bila shaka upinzani usingeweza kufanya vyema katika awamu hii. Kwangu mimi suala la ushamiri wa upinzani kutegemea kudra za yule aliyeshikilia mpini siwezi kukubaliana nalo, siwezi shiriki kwenye mchezo ambao matokeo yake yanajulikana.
3. Kwa maana hii wapo wanasiasa bora kabisa ndani ya vyama vya upinzani wenye maono na uwezo wa kufanya vizuri sana katika utumishi wa nchi. Lakini kwa mazingira haya ya kisiasa ndoto zao hazitakuja kufanikiwa maana wamepandikiza mbegu zao kwenye udongo usio na rutuba (vyama vya upinzani ambavyo system haiwezi kuwa fair kwao). Kama nchi haipo tayari kuweka uwanja sawa wa ushindani wa kisiasa, kwa nini tusivunjilie mbali mfumo wa vyama vingi ili wote tuingie ndani ya chama kimoja tushindanie humo humo?
4. Hata pale atakapotokea kiongozi mwenye moyo wa kuweka uwanja sawa wa ushindani, yapo mambo fulani ya kitaifa "non-negotiable". Katika haya hakuna suala la demokrasia. Kwa mfano, muungano wa Tanganyika na Zanzibar umeshakomaa vya kutosha kiasi kwamba mwanasiasa yeyote anayetaka kuupasua ni sawa na kupasua mapacha waliounganika viungo vyao, halafu eti unataka kuwatenganisha ukubwani. Kama ungetaka kufanya hiyo operation ya upasuaji ungefanya hivyo wakiwa wachanga. Kufanya hivyo sasa ni kuigawa nchi na no way tutafanya hivyo bila kuiua nchi. Kuna mambo mengine kama hayo, na ushauri wangu ni kwamba chama cha kisiasa cha upinzani credible lazima kirejee kwenye misingi na miiko ya taifa na kuhakikisha hakuna sera yake hata moja itakayocompromise hiyo miiko. Mbona kuna mambo mengi tu kibao ya kutofautiana na CCM? Yaani nchi imekaa tangu mwaka 1961 ikiwa stable na systems zake halafu kamtu kanakuja mwaka 2020 kanahubiri kwamba katavunjilia mbali nguzo na kujenga nguzo mpya za hili taifa? Taifa lipi hilo lisilo na miiko isiyovunjwa?
 
Amani Msumari!!! Pole na hongera sana!! Umesoma miaka mingapi??? Naona umetulia tuli!!!

Jaribu kuongea na watu zaidi uelewe kinachodaiwa ni nini na kwa nini kabla ya kuwaita watu wachwara!!!
Pia elewa tofauti kati ya utulivu na amani! Ukiwa mtulivu haina maana kuwa una amani kama hujatendewa haki!!

Je aliyeiba kura si mwanasiasa uchwara!!!
Ama uchwara ni gani??

Ama ukiruhusiwa kuuza nyanya barabarani kwa kuwa wewe unaitwa mnyonge na umekubali basi wewe una amani kwa kuwa tu umeruhusiwa kuuza nyanya zako????Wakati viongozi wasiowanyonge wanakula kivulini kwa mirija kwa kodi uliyolipa wewe baada ya kuuza hiyo nyanya???

Watanzania amkeni!! Daini katiba mpya kwa nguvu ili watanzania wote wafurahie maisha na siyo wachache tu!!!

Mwaka jana tumelipa kodi jumla Trilioni 18. Zaidi ya nusu ya hiyo inaliwa katika matumizi ya kawaida! Chini ya nusu ndiyo maendeleo!!!
Sheria ya bajeti yoyote ni kwamba matumizi ya kawaida yasizidi 30%! Tz ni zaidi ya 60%???

Kama hatuelewi katiba mpya faida yake ni nini tuulize!! Wote tukiidai tutafika pazuri!! Tusidanganyike!!!

AmaniMsumari, usidanganyike anayekuambia kuwa anayedai katiba mpya ni mchwara huyo umwogope kwa sababu huyo ni mtu anayekula kivulini kwa jasho lako akikudanganya kuwa yeye ni mwokozi wako wewe mnyonge kwa hiyo ufunge mdomo wako!!!!
 
Back
Top Bottom