Mahamoud Ali wa Djibouti ashinda nafasi ya Uenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AUC) dhidi ya Raila Odinga kutoka Kenya

Baadhi ya nchi za SADC zilimuunga moja kwa moja mgombea wa kutoka Madagasca (m-SADC mwenzao). Sasa tumekosa Bara na Pwani (SADC na EAC). Kiti kimeenda Pembe ya Africa..!
 
Sometimes odinga itabidi akubali uongozi si his calling
 
Umri wa Wassira ni Tatizo!!!!
 
Mwache akose. Tulikuwa tunamuita baba wa mageuzi Afrika Mashariki lakini akaja kutugeuka baada ya kuungana na Ruto.
 
Raundi ya kwanza

Odinga 20, mgombea wa Djubut 18 na Mgombea wa SADC 10

Round ya pili

Raila Odinga 22, mgombea wa Djubut 19 na Mgombea wa SADC

Unadhani kwanini Raila Odinga amefeli? 🐼
Hapa mimi sijamuelewa kabisa mleta mada.
Yaani round ya pili Odinga kapata kura 22 na mpinzani wake wa karibu kura 19, halafu Odinga kashindwa!
Kivipi?
Wenye D mbili embu njooni mtueleweshe, sisi wengine hatukufika kidato.
 
Raundi ya kwanza

Odinga 20, mgombea wa Djubut 18 na Mgombea wa SADC 10

Round ya pili

Raila Odinga 22, mgombea wa Djubut 19 na Mgombea wa SADC

Unadhani kwanini Raila Odinga amefeli? 🐼
nchi zote za kiarabu ziliamua kwamba huu ni wakati wao kuongoza chombo hicho kikubwa barani Africa,

lakini pia,
ECOWAS, COMESA NA SADC zilipendelea zaidi mtu wa eneo lao, ambae pia anazungumza kifaransa, kiarabu kireno na kihispania kwa ufasaha kitu ambacho Raila Odinga alikosa 🐒
 
Raundi ya kwanza

Odinga 20, mgombea wa Djubut 18 na Mgombea wa SADC 10

Round ya pili

Raila Odinga 22, mgombea wa Djubut 19 na Mgombea wa SADC

Unadhani kwanini Raila Odinga amefeli? 🐼
Kumpa Raila Odinga uenyekiti wa AU ingekuwa ni kumzawadia Ruto na wafuasi wake. Kumbuka Kenya ni "Mshirika Mkuu Asiye wa NATO"!

Djibouti ni taifa linalohangaika bila ushawishi mkubwa. Hakuna mtendaji mkuu mwenye ushawishi.

Lakini nadhani baadhi ya kambi za wapiga kura wa Afrika zilikuwa na sababu tofauti za kukataa kupanda kwa Kenya kwenye nafasi hiyo ya ushawishi. Odinga ni mwathirika wa sera mbovu za kigeni za nchi yake chini ya Ruto.

Ni hoja halali ya kimaendeleo, lakini si lazima iwe muhimu kwa kambi za wapiga kura wa AU. AU hupiga kura kulingana na maslahi ya kambi. Hatujui jinsi SADC ilivyopiga kura, hasa ikizingatiwa kuwa Marekani inatishia kuiwekea vikwazo Afrika Kusini.
 
Hapa mimi sijamuelewa kabisa mleta mada.
Yaani round ya pili Odinga kapata kura 22 na mpinzani wake wa karibu kura 19, halafu Odinga kashindwa!
Kivipi?
Wenye D mbili embu njooni mtueleweshe, sisi wengine hatukufika kidato.
Ukijibiwa nistue👃👃
 
Waziri wa Mambo ya Nje wa Djibouti, Mahamoud Ali Youssouf ameshinda nafasi ya Uenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) dhidi ya #RailaOdinga kutoka Kenya ambaye alikuwa mwakilishi pekee kutoka Afrika Mashariki.

Uchaguzi huo uliofanyika nchini Ethiopia, Odinga alishinda duru mbili za kwanza lakini akapoteza katika duru tatu zilizofuata kwa kupata kura 20 huku Mahamoud akishinda kwa kura 23.

Aidha, Mahamoud atarithi nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti Moussa Faki Mohamed ambaye ni Waziri Mkuu wa zamani wa Chad anayetarajia kumaliza muhula wake wa pili wa Uenyekiti wa #AU mapema Mwaka 2026.

Chanzo: Mtandao wa JamiiForums

Kushindwa kwa Odinga kumeonyesha kuwa Viongozi wote wa EAC waliokuwa wakimpigia Chapuo ni 'Kipa Katoka' tupu.
 
Odings Sasa atulie ale mali zake
Kama pesa anayo, anagombea anashindwa na kujitoa aibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…