Mahamoud Ali wa Djibouti ashinda nafasi ya Uenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AUC) dhidi ya Raila Odinga kutoka Kenya

Mahamoud Ali wa Djibouti ashinda nafasi ya Uenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AUC) dhidi ya Raila Odinga kutoka Kenya

Waziri wa Mambo ya nje wa Djibouti Mahamoud Ali Youssouf ameshinda nafasi ya Uenyekiti wa Umoja wa Afrika maarufu (AU)

Katika Uchaguzi ambao ulikuwa nchini Ethiopia Mahamoud alishinda dhidi ya Raila Odinga ambaye alikuwa mwakilishi pekee kutoka Afrika Maahariki

Raila alishinda duru mbili za kwanza lakini akapoteza duru tatu zilizofuata kwa Mahamoud Ali Youssouf wa Djibouti.

Katika duru ya kwanza, Odinga alipata kura 22 huku Mahamoud akipata kura 18 na Randriamandrato alipata kura 10.


Katika duru ya pili, alipata kura 20, Mahamoud 18, na Randriamandrato 10. Hata hivyo, Mahamoud alimshinda Odinga kwenye duru ya tatu kwa kura 23 dhidi ya 20 za Raila.

Odinga alikuwa akiwania nafasi hiyo na wagombea wengine ili kumpata atakayemrithi Moussa Faki Mohamed, Waziri Mkuu wa zamani wa Chad anayetarajia kumaliza muhula wake wa pili wa uenyekiti wa AU mapema mwakani.

Hii ni mara ya pili Kenya kutupa karata yake katika kuwania nafasi hiyo, ilifanya hivyo mwaka 2017 alipogombea Amina Mohammed lakini hakufanikiwa.

Katika uchaguzi wa nafasi hiyo, wakuu wa nchi za Afrika, wamepiga kura kwa siri na inahitaji kupata angalau theluthi mbili ya 36 ili kumpata mshindi.

=================================================

Kenya’s candidate in the African Union Commission (AUC) Chairperson elections, Raila Odinga, has lost the race in the exercise that was conducted in Addis Ababa, Ethiopia.

Raila won the first two rounds of voting, but then went on to lose the next three rounds to Djibouti candidate Mahamoud Ali Youssouf.

In the first round, Raila garnered 20 votes against Mahamoud’s 18, while Richard Randriamandrato of Madagascar bagged 10 votes. There was one abstained vote.

In the second round, Raila secured 22 votes, Mahamoud got 19, and Randriamandrato received 7 votes. One nation abstained from the second round as well.
The former Kenyan Prime Minister, however, came up short in the third round after receiving 20 votes, losing to Mahamoud who rose to first place with 23 votes, while Randriamandrato came third with 5 votes.
There was still one abstention, and Randriamandrato was eliminated from the election, leaving Raila head-to-head against Mahamoud.

Mahamoud maintained his lead in the fourth round, scoring 25 votes against Raila’s 21 votes. There was one spoilt vote while one nation abstained.
In the fifth round, Mahamoud garnered 26 votes while Raila scored 21 votes, and one nation abstained from the vote.
Mahamoud maintained his lead into the sixth round, garnering a similar 26 votes, while Raila got 22 votes with one abstention.

Source: Citizen Digital
Raila ana gundu mbaya sana
 
Wanasema hawajapendezewa na mdimamo wake katika Congo Crisi kwa hiyo hawataka kumsapoti Raila.
Halafu Raila was crying like a baby.
 
Raundi ya kwanza

Odinga 20, mgombea wa Djubut 18 na Mgombea wa SADC 10

Round ya pili

Raila Odinga 22, mgombea wa Djubut 19 na Mgombea wa SADC

Unadhani kwanini Raila Odinga amefeli? 🐼
Kumekua na kutunishiana misuli kati ya jumuiya hizo mbili. EAC nayo inataka iwe kubwa kuliko SADC, ndo maana wakamua wamuunge mkono huyo Mhabeshi.
Sasa Baba akale jeuri yake.
 
Raundi ya kwanza

Odinga 20, mgombea wa Djubut 18 na Mgombea wa SADC 10

Round ya pili

Raila Odinga 22, mgombea wa Djubut 19 na Mgombea wa SADC

Unadhani kwanini Raila Odinga amefeli? 🐼

..Rais Samia Suluhu ameshindwa kuwashawishi viongozi wenzake wampigie kura Raila Odinga.

..enzi za Nyerere, Mwinyi, Mkapa, na Kikwete, mgombea aliyeungwa mkono na Tanzania ilikuwa lazima ashinde.
 
Mbona salim Ahmed hakuwa katibu wa UN licha ya kutakiwa na Hyyo unayemwita ana yshawishi lakini koffi Annan aliweza justify your comment
Swali lako halina maana yoyote Iile wote tunajua nini kilitokea kwa Salim au unachuki na Mwalimu?.
 
..Rais Samia Suluhu ameshindwa kuwashawishi viongozi wenzake wampigie kura Raila Odinga.

..enzi za Nyerere, Mwinyi, Mkapa, na Kikwete, mgombea aliyeungwa mkono na Tanzania ilikuwa lazima ashinde.
nilitegemea Tanzania kwa ushawishi wake kimataifa ingeshawishi wajumbe wa AU wamchague Raila, kama ilikaa kimya matokeo yake ndiyo hayo
 
Mbona salim Ahmed hakuwa katibu wa UN licha ya kutakiwa na Hyyo unayemwita ana yshawishi lakini koffi Annan aliweza justify your comment
mwalimu alifuata siasa za kijamaa dhidi ya siasa za kibepari ziliathiri kuchaguliwa salim
 
nchi zote za kiarabu ziliamua kwamba huu ni wakati wao kuongoza chombo hicho kikubwa barani Africa,

lakini pia,
ECOWAS, COMESA NA SADC zilipendelea zaidi mtu wa eneo lao, ambae pia anazungumza kifaransa, kiarabu kireno na kihispania kwa ufasaha kitu ambacho Raila Odinga alikosa 🐒

Yaani kutojua lugha za mabeberu ndiyo kunamfanya akose kuchaguliwa. Masikini Afrika inatia huruma
 
Yaani kutojua lugha za mabeberu ndiyo kunamfanya akose kuchaguliwa. Masikini Afrika inatia huruma
ni wazi hiyo ni miongoni mwa sababu muhimu zilizomkwamisha muungwana,

Mahamoud Yusuph anazungumza zaid ya lugha5 za kigeni ukilinganisha na Raila anaezungumza kiingereza na kiswahili pekee :NoGodNo:
 
Back
Top Bottom