Maharage Chande: Hatuogopi na tutafanya hiyo miradi na private sekta(Kununua umeme). TANESCO kuuza dhamana(Bonds)

Maharage Chande: Hatuogopi na tutafanya hiyo miradi na private sekta(Kununua umeme). TANESCO kuuza dhamana(Bonds)

Hiyo ni interview ipo clubhouse itafute yote mbona kaongelea yote hayo ila swali la Zitto ni kwanini hawauzi bond Ili wapate Hela ya kufanya miradi au kwanini hawafanyi PPP kuzalisha umeme?

Ndio kajibu hivyo kuwa issue ni tariff, wengine wanataka wawacharge TANESCO gharama kubwa kwa Kila unit, kaongelea wengine kutaka IRR iwe above 15% Ili warudishe pesa aliyowekeza mapema!! Pia akasema bonds huwezi issue mpaka wawekezaji waone financial soundness ya kampuni mfano debt structure, internal processes (Kaongelea automation) n.k

Tuwe optimistic, Mimi Sina Imani na serikali ya CCM ila Kuna wakati tujadili hoja tukiwa na positive mindset sio kupindisha kilichozungumzwa. Maana mgao hautaki wakati huohuo unaambiwa wanataka kujenga Kinyerezi 3 and 4 nako hutaki, Sasa unataka wafanyeje? What's ur solution
Unasikiliza sana porojo za hawa watu

Bond kwenye mashirika in other word ni preference shares.

Na ili investors watoe hela zao, kitu cha kwanza wanachoangalia sio balance sheet tu (yes it’s most important), but so is weledi wa management.

Kuna vitu kama asset returns ya shirika na mambo mengine lukuki. Sasa unadhani shirika ambalo lina mgao wa umeme kwa miezi sita ya mwaka litavutia wawekezaji.

Call it bonds or preferences shares, hakuna mwekezaji timamu ataweka hela yake bila ya government guarantee; vinginevyo kwa madeni ya TANESCO lingeshapelekwa kwenye windup muda mrefu tu.

So usijiongopee kufutiwa kwa madeni ya shirika, wakati management inaonekana bado mbovu na shirika aliwezi kuzalisha umeme at 95%+ ya capacity sio kigezo cha kukopwa.

Only in Tanzania, jamaa wanafanya yao; wanaropoka upuuzi and we think they make sense,
 
Maharage Chande: Fantastic question Zitto, nianze kwenye kuwapa watu binafsi. Ni kweli kama ulivyosema, TANESCO na wizara ya nishati kwa miaka mingi iliyopita, utekelezaji wa miradi kwenda kwa watu binafsi imekuwa inasuasua, inasuasua kwa sababu kihistoria kumekuwa na kujengeka uoga mwingi kutokana miradi mbalimbali ya huko nyuma inayotokea na maneno yanayotokea baada ya hapo na kufuatana fatana kwa watendaji kunakotokea baada ya hapo kiasi watendaji wanakuwa wanaogopa.

Sisi posture yetu hatuogopi na tutafanya hiyo miradi na private sekta lakini kwa private sector pia, hapo zamani kulikuwa na Information asymmetry. Ili uepuke lawama kwenye umeme lazima uwe wazi na sisi ndio posture yetu ya sasa hivi.

Tayari hivi tunavyoongea na wewe kwa mfano, ukisikia tumesaini deal na Mazda ni the open book principle na parameter hizi kwahiyo mpaka tunaingia kaburini tutakuwa na uwezo wa kusimamia decision tuliyoifanya.

Hakuna lolote wezi wa umma tu. Wamewekana kwa nguvu wanajidai hawaogopi. Hawawezi kudeal na private sector bila corruption na hiyo ndio inaharibu kila kitu.

Rushwa inawatoa kwenye malengo matokeo wanatuletea umeme ghali kuliko popote duniani.
 
Haya ni "MakambaMahaharage"

Majizi tupu! Hakuna lolote hapo!

Huyo Zitto mzee wa fursa, hapo ameuliza Swali elekezi!

Tayari na yeye ni sehemu ya mpango Wizi.

Ina maana kuna Deal Na "Mazda" na sasa linakolezwa taratibu.

Hawa tutakuja kuwanyonga hadharani, kama sio sisi basi watoto wetu watawanyonga watoto wao.
Cha muhimu hizi zisiwe tu ni tuhuma za "jumla jumla".
 
Zitto hana uelewa wa biashara na hata uelewa wake wa economics ni very limited.

Ni mropokaji.

Hoja zake nyingi ni kutoka kwa mabeberu, anatumiwa kutoa pressure Serikalini ku adapt sera wanazotaka.

Lakini akikutana na mtu serious anaejua economy and finance; hakuna anachojuwa.

Mpaka unajiuliza sasa vitabu vyote anavyosoma kila mwaka anajifunza nini.

Jamaa ni kilaza, kweli kweli.

Ngumu kwa watanzania kumuona for what he is kwa sababu ni anaejinasibu kama msoma vitabu and he has friends in high places.

Lakini deep down Zitto ni mtu ambae anaongea ujinga muda mwingi and very limited on his knowledge.

Ujinga mtupu

Nashauri kwamba kwenye spaces ambazo DG wa TANESCO huwa anafanya uwe una shiriki, unamsikiliza, kama una maswali unamuuliza.

Utapata fafanuzi za mambo mengi na pia utapata fursa ya kushauri ni nini kifanyike, hii itakusaidia sana wewe, yeye, TANESCO pamoja na "sisi" (watanzania wenzio).
 
Sikutaka hata kusikiliza upuuzi wake wote for starters shirika kama TANESCO linatakiwa kuwa limeshafanya investment appraisal option zote wanazotaka na kualika wawekazaji kwenda kwenye maeneo ambayo wanadhani kwa wao wenyewe walipo maeneo fulani awawezi given their cash flow limitations.

Lakini sio kuwaita wawekazaji halafu wao ndio waamue the cost of investment and return they want, huko ni kuto kujitambua.

Kama ukimsikiliza raisi Samia alipo toka marekani alisema kuna wawekezaji wanaotaka kuja kuwekeza kwenye nishati jadidifu from my understanding that means (Green energy).

Sasa basi inabidi uelewe pia how carbon trading works in their countries given the global pressure; ili na wewe uweke mazingira gani ya kualika wawekezaji kwa manufaa yako.

Ni hivi hayo mambo yanataka watu wanayoyaelewa ndio maana Museveni akawajibu EU upuuzi kuhusu hoja za mazingira kwenye EACOP na uwezi kusikia nchi ikimjibu, kwa sababu wanaelewa rights za third world, wenye kumjibu labda wanaharakati tu au wabunge binafsi.
Tatizo linaweza kuanzia hapo ulipoandika SIKUTAKA HATA KUSIKILIZA....

Hapo pana tatizo kubwa sana, kubwa mno.

Inawezekana kabisa kwamba "sisi" tuna uelewa mkubwa na maarifa mengi zaidi kuliko watu wengine. Hili ni jambo jema sana na ni jambo la asili (ni majaaliwa).

Lakini hii haitoi haki wala uhalali wa kutokuwasikiliza wengine tunaodhani wana uwezo mdogo kuliko "sisi".

Masikilizano ni nyenzo muhimu sana katika kujenga kwa pamoja.

Hii nchi ni yetu sote, angalau tuanze kwa kuwa tayari kusikilizana.
 
Kitu nilichokiona Watz wengi wanaongozwa na emotions pamoja na sentiments badala ya uweledi. Ni ajabu mtu kusema sijamsikiliza Maharage mpaka mwisho at the same time anakuja na tantalila za kukosoa! Pia kusema ZZK ni agent wa mabeberu kila kitu anachoongea ametumwa ni sweeping statements.

Maharage has been so transparent so far and the best CEO ambaye anashiriki mikutano ya wadau, anajibu maswali na nzuri zaidi anapokea ushauri. Pia anajitahidi kuwa mkweli na kuepuka kutoa ahadi za kufurahisha umati. Kwahiyo, kwa wale wenye chuki na husda better you man up mje na hoja, mawazo mbadala na solutions na sio kuita watu wezi, wapigaji n.k
 
Sekta ya nishati kama kawaida yake ndio ziwa la ukamuaji.
 
Maharage Chande: Fantastic question Zitto, nianze kwenye kuwapa watu binafsi. Ni kweli kama ulivyosema, TANESCO na wizara ya nishati kwa miaka mingi iliyopita, utekelezaji wa miradi kwenda kwa watu binafsi imekuwa inasuasua, inasuasua kwa sababu kihistoria kumekuwa na kujengeka uoga mwingi kutokana miradi mbalimbali ya huko nyuma inayotokea na maneno yanayotokea baada ya hapo na kufuatana fatana kwa watendaji kunakotokea baada ya hapo kiasi watendaji wanakuwa wanaogopa.

Sisi posture yetu hatuogopi na tutafanya hiyo miradi na private sekta lakini kwa private sector pia, hapo zamani kulikuwa na Information asymmetry. Ili uepuke lawama kwenye umeme lazima uwe wazi na sisi ndio posture yetu ya sasa hivi.

Tayari hivi tunavyoongea na wewe kwa mfano, ukisikia tumesaini deal na Mazda ni the open book principle na parameter hizi kwahiyo mpaka tunaingia kaburini tutakuwa na uwezo wa kusimamia decision tuliyoifanya.

Maharage kuchacha!
 
Kitu nilichokiona Watz wengi wanaongozwa na emotions pamoja na sentiments badala ya uweledi. Ni ajabu mtu kusema sijamsikiliza Maharage mpaka mwisho at the same time anakuja na tantalila za kukosoa! Pia kusem ZZK ni agent wa mabeberu kila kitu anachoongea ametumwa ni sweeping statements.

Maharage has been so transparent so far and the best CEO ambaye anashiriki mikutano ya wadau, anajibu maswali na nzuri zaidi anapokea ushauri. Pia anajitahidi kuwa mkweli na kuepuka kutoa ahadi za kufurahisha umati. Kwahiyo, kwa wale wenye chuki na husda better you man up mje na hoja, mawazo mbadala na solutions na sio kuita watu wezi, wapigaji n.k
Umeongea vizuri sana mkuu. Saluti
 
Huyu ni mpiga dili mzuri sana. Anayoyafanya Tanesco ni upuuzi mtupu.
Can you mention wizi mmojawapo aliowahi kufanya Maharage ku-substantiate hoja yako? Maharage alikuwa DSTv for years, Hebu tutajie skendo mojawapo ya wizi aliowahi kufanya huko. Otherwise ni wivu tu wa wananchi wa nchi hii dhidi ya kila mwenye mafanikio kumuita mwizi, freemasonry n.k . Ushauri wa bure wape elimu bora watoto wako ili baadae uepuke kuwa mchawi na mlozi ukishazeeka
 
Huyu ni mpiga dili mzuri sana. Anayoyafanya Tanesco ni upuuzi mtupu.
Mkuu hebu weka hoja mezani (kama zipo), hizi tuhuma za jumlajumla sidhani kama zina msaada sana.

Tunaweza kutumia platforms kama hizi kushauri nini kifanyike, kifanyike vipi, wapi waliopo sasa hivi wanakosea, n.k n.k

Kwa sababu wameamua kuwa wasikivu, wanasikiliza ushauri na maoni ya wadau, wanajibu changamoto na kutoa ufafanuzi, wanaeleza nini kinaendelea, nk basi nasisi tuitumie fursa hiyo vizuri.

Hii mambo ya yule ni mwizi, ni mpiga dili, kwanza jina lake maharage, mara oooh maharage yamechacha.... nadhani tunaweza kufanya zaidi ya hapo
 
Maharage Chande: Fantastic question Zitto, nianze kwenye kuwapa watu binafsi. Ni kweli kama ulivyosema, TANESCO na wizara ya nishati kwa miaka mingi iliyopita, utekelezaji wa miradi kwenda kwa watu binafsi imekuwa inasuasua, inasuasua kwa sababu kihistoria kumekuwa na kujengeka uoga mwingi kutokana miradi mbalimbali ya huko nyuma inayotokea na maneno yanayotokea baada ya hapo na kufuatana fatana kwa watendaji kunakotokea baada ya hapo kiasi watendaji wanakuwa wanaogopa.

Sisi posture yetu hatuogopi na tutafanya hiyo miradi na private sekta lakini kwa private sector pia, hapo zamani kulikuwa na Information asymmetry. Ili uepuke lawama kwenye umeme lazima uwe wazi na sisi ndio posture yetu ya sasa hivi.

Tayari hivi tunavyoongea na wewe kwa mfano, ukisikia tumesaini deal na Mazda ni the open book principle na parameter hizi kwahiyo mpaka tunaingia kaburini tutakuwa na uwezo wa kusimamia decision tuliyoifanya.

Duuh...Kwahiyo kama ni open kwanini Mazda na siyo Ame? Tangazo la hilo deal lilitolewa lini wapi? These guys bwana!
 
Mkuu hebu weka hoja mezani (kama zipo), hizi tuhuma za jumlajumla sidhani kama zina msaada sana.

Tunaweza kutumia platforms kama hizi kushauri nini kifanyike, kifanyike vipi, wapi waliopo sasa hivi wanakosea, n.k n.k

Kwa sababu wameamua kuwa wasikivu, wanasikiliza ushauri na maoni ya wadau, wanajibu changamoto na kutoa ufafanuzi, wanaeleza nini kinaendelea, nk basi nasisi tuitumie fursa hiyo vizuri.

Hii mambo ya yule ni mwizi, ni mpiga dili, kwanza jina lake maharage, mara oooh maharage yamechacha.... nadhani tunaweza kufanya zaidi ya hapo
Watu wamelishwa propaganda fake, na zimewakaa kweli kweli.
 
Back
Top Bottom