Maharage Chande: Hatuogopi na tutafanya hiyo miradi na private sekta(Kununua umeme). TANESCO kuuza dhamana(Bonds)

Unasikiliza sana porojo za hawa watu

Bond kwenye mashirika in other word ni preference shares.

Na ili investors watoe hela zao, kitu cha kwanza wanachoangalia sio balance sheet tu (yes it’s most important), but so is weledi wa management.

Kuna vitu kama asset returns ya shirika na mambo mengine lukuki. Sasa unadhani shirika ambalo lina mgao wa umeme kwa miezi sita ya mwaka litavutia wawekezaji.

Call it bonds or preferences shares, hakuna mwekezaji timamu ataweka hela yake bila ya government guarantee; vinginevyo kwa madeni ya TANESCO lingeshapelekwa kwenye windup muda mrefu tu.

So usijiongopee kufutiwa kwa madeni ya shirika, wakati management inaonekana bado mbovu na shirika aliwezi kuzalisha umeme at 95%+ ya capacity sio kigezo cha kukopwa.

Only in Tanzania, jamaa wanafanya yao; wanaropoka upuuzi and we think they make sense,
 
Hakuna lolote wezi wa umma tu. Wamewekana kwa nguvu wanajidai hawaogopi. Hawawezi kudeal na private sector bila corruption na hiyo ndio inaharibu kila kitu.

Rushwa inawatoa kwenye malengo matokeo wanatuletea umeme ghali kuliko popote duniani.
 
Cha muhimu hizi zisiwe tu ni tuhuma za "jumla jumla".
 

Nashauri kwamba kwenye spaces ambazo DG wa TANESCO huwa anafanya uwe una shiriki, unamsikiliza, kama una maswali unamuuliza.

Utapata fafanuzi za mambo mengi na pia utapata fursa ya kushauri ni nini kifanyike, hii itakusaidia sana wewe, yeye, TANESCO pamoja na "sisi" (watanzania wenzio).
 
Tatizo linaweza kuanzia hapo ulipoandika SIKUTAKA HATA KUSIKILIZA....

Hapo pana tatizo kubwa sana, kubwa mno.

Inawezekana kabisa kwamba "sisi" tuna uelewa mkubwa na maarifa mengi zaidi kuliko watu wengine. Hili ni jambo jema sana na ni jambo la asili (ni majaaliwa).

Lakini hii haitoi haki wala uhalali wa kutokuwasikiliza wengine tunaodhani wana uwezo mdogo kuliko "sisi".

Masikilizano ni nyenzo muhimu sana katika kujenga kwa pamoja.

Hii nchi ni yetu sote, angalau tuanze kwa kuwa tayari kusikilizana.
 
Kitu nilichokiona Watz wengi wanaongozwa na emotions pamoja na sentiments badala ya uweledi. Ni ajabu mtu kusema sijamsikiliza Maharage mpaka mwisho at the same time anakuja na tantalila za kukosoa! Pia kusema ZZK ni agent wa mabeberu kila kitu anachoongea ametumwa ni sweeping statements.

Maharage has been so transparent so far and the best CEO ambaye anashiriki mikutano ya wadau, anajibu maswali na nzuri zaidi anapokea ushauri. Pia anajitahidi kuwa mkweli na kuepuka kutoa ahadi za kufurahisha umati. Kwahiyo, kwa wale wenye chuki na husda better you man up mje na hoja, mawazo mbadala na solutions na sio kuita watu wezi, wapigaji n.k
 
Sekta ya nishati kama kawaida yake ndio ziwa la ukamuaji.
 
Maharage kuchacha!
 
Umeongea vizuri sana mkuu. Saluti
 
Huyu ni mpiga dili mzuri sana. Anayoyafanya Tanesco ni upuuzi mtupu.
Can you mention wizi mmojawapo aliowahi kufanya Maharage ku-substantiate hoja yako? Maharage alikuwa DSTv for years, Hebu tutajie skendo mojawapo ya wizi aliowahi kufanya huko. Otherwise ni wivu tu wa wananchi wa nchi hii dhidi ya kila mwenye mafanikio kumuita mwizi, freemasonry n.k . Ushauri wa bure wape elimu bora watoto wako ili baadae uepuke kuwa mchawi na mlozi ukishazeeka
 
Huyu ni mpiga dili mzuri sana. Anayoyafanya Tanesco ni upuuzi mtupu.
Mkuu hebu weka hoja mezani (kama zipo), hizi tuhuma za jumlajumla sidhani kama zina msaada sana.

Tunaweza kutumia platforms kama hizi kushauri nini kifanyike, kifanyike vipi, wapi waliopo sasa hivi wanakosea, n.k n.k

Kwa sababu wameamua kuwa wasikivu, wanasikiliza ushauri na maoni ya wadau, wanajibu changamoto na kutoa ufafanuzi, wanaeleza nini kinaendelea, nk basi nasisi tuitumie fursa hiyo vizuri.

Hii mambo ya yule ni mwizi, ni mpiga dili, kwanza jina lake maharage, mara oooh maharage yamechacha.... nadhani tunaweza kufanya zaidi ya hapo
 
Duuh...Kwahiyo kama ni open kwanini Mazda na siyo Ame? Tangazo la hilo deal lilitolewa lini wapi? These guys bwana!
 
Watu wamelishwa propaganda fake, na zimewakaa kweli kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…