Maharage Chande: Tuache kupeana maneno tamutamu; bei ya Tsh 27,000/= haitoshi kuunganisha umeme

Nimesikiliza huyu mkurugenzi nikabaki nimeduwaa. Hivi concept ya serikali kusambaza umeme ikoje? Nilidhani kwamba gharama za kuunganisha zingekuwa as minimum as possible ili waunganishe wateja wengi halafu fedha zirudi kwa kuuza units za umeme. Ndiyo maana makampuni ya simu yanatafuta yenyewe fedha kwa ajili ya infrastructure installation (kuweka minara na vituo kadhaa then returns zao wanazipata kutoka kwa wateja kupitia airtime, msg na miamala.
 
Sawa ni hasara kwa 27,000 walitoe kwenye monopoly waanzishe mashirika 3 au 4 yashindane kama mashirika ya simu tuone
 
Kwaninimtu analipia ili kuunganishiwa umeme lakini vifaa vinakuwa Mali ya TANESCO?
 
Wanachokosea Tanesco ni kutaka pesa ya papo papo kwa huduma ambayo mtu lazima atumie baada ya kuunganishwa.

Wapige hesabu gharama halisi, Kisha mwananchi alipie 30% ya gharama halisi siku ya kwanza baada ya hapo 70% alipie kidogo kidogo kila anponunua umeme.

Unaweza kukata 40% ya kila pesa inayowekwa kwenye meter husika mpk kumaliza deni.

Dawasa wameweza kutoa maji ya mkopo mpaka raia wa chini kabisa mwenye kibanda ana Bomba la maji wao Tanesco kwa nini hawafikirii nje ya box?
 
Telecom and electronics engineer.......tujipange 27000 itaua Kampuni sio halisi acha kijijini walipe 27k
Mkuu utaiuaje TANESCO wakati bei hiyo ya 27, 000/- ni kwa ajili ya
vijijini chini ya miradi wa REA. Tatizo la Tanesco ni kuwa na bajeti kubwa ya Matumizi ya Kawaida wakati bajeti ya Miradi ni ndogo. Mradi wa REA ni msaada toka Ugaibuni na ilitakiwa tufungiwe bure. Leo TANESCO inataka kuuteka mradi ambao ulikuwa unafanya kazi zake kwa ufanisi. Waacheni watu wa vijijini waendelee na REA yao, mbona ninyi wa town mnafaidi sana: lami, maji, mwendokasi, viwanja vikubwa vya michezo n.k
 
Huyu ni Mkurugenzi bwege! Ni makosa ya rais kuendelea kuamini kwamba 'vijana' wanaweza kuendesha mashirika makubwa kama haya bila uzoefu. Siyo yeye tu, ilikuwa hivyo kwa NHC ya mchechu, PPF ya Erio, nk. Mashirika makubwa ya uzalishaji hutakiwi kumpa mtu asiye na rekodi ya mafanikio ktk nchi yeyote ile! Hilo ni jaribio la kishenzi tu!

Tanesco haipati faida kwa kuunganisha umeme. Tanesco wangeweza hata kuunganisha bure maana vyote vinavyolipiwa na mteja ni mali yao. Nguzo, nyaya, mita na upuuzi wote ni mali ya Tanesco sasa kwa nini anataka mteja alipie? Yeye auze umeme kwa faida, basi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…