Maharage Chande wa TANESCO ameingiaje utumishi wa umma akiwa na umri zaidi ya miaka 45?

Kuna nafasi ambazo ni za mkataba, mtu anaweza kuzidi miaka 45 lakini awe chini ya 55, Ambapo unapewa mkataba wa miaka Mitano mitano,
Labda kama amezidi miaka 60 sawa vinginevyo ni sawa hakuna sheria ilivunjwa, kwani atapewa mkataba unaomstahili.
 
Ukurugenzi wa Halmashauri ni kazi ya Mkataba ?

Halmashauri sina uhakika ila nahisi sio parmanent pia maana rais anateua yoyote na kutengua yeyote muda wowote...

za mashirika ya uma kama tanesco ni za mkataba. Mkurugenzi wa shirika hapewi parmanent contract.

Huyo maarage chande anaeongelewa kwenye uzi nafasi yake sio ya parmanent contract
 
He Verrazanno hebu punguza povu na umuache afanye kazi kwanza. Angalau ikipita miezi sita ndiyo uje kutupa sababu kwa nini ameshindwa kazi.

Kila anayeteuliwa ni majungu tu.
 
Nakukatalia nafasi za ukurugenzi sio za (fixed) mikataba kama nimekuelewa ila tambua hakuna ajira ambayo haina mkataba.
Ajira ya ukurugenzi wa halmashauri ni ajira iliyo katika mkataba wa kudumu na kulipwa pension ambayo kuna kipengele cha umri wa kuingia pia nafasi za ukurugenzi wa halmashauri ni nafasi za uteuzi kwa watumishi wa umma waliofanya kazi vizuri kwenye utumishi wa umma kwa zaidi ya miaka 12 na kufikia ngazi ya uprinsipo katika vyeo vyao serikalini
Nafasi za ukuruenzi (CEOs)wa mashirika mara nyingi zinakuwa kwa mujibu wa sheria iliyoanzisha taasisi usika
 
Nadhani ifike mahala tuwe na vigezo vitakavyokua na maslahi ya taifa na visivyogawa watu kwa kuangalia wapi walikua wanatumikia

Sawa ana miaka 45, na hajawahi kuwa na checknumber kama public service employee sawa; lakini tujiulize huko nbc na kwengine alikokua anatumika alikua anahudumia umma wa watanzania? au alikua anahudumia familia yake binafsi

Wapo watu wazuri sana kiutendaji kwenye private sector wanaojua bila uzalishaji endelevu hakuna maendeleo ya taasisi wala nchi; ifike mahala serikali iwachukue na kuwatumia kama huyu Maharage Chande

Sio mbaya tukareview policy na taratibu zetu kwenye vipengele kama umri na wapi na nini amefanya huko ili tuweze kupata watu competent hata kama wana miaka50.


KAZI IENDELEE
 
Mama tunakusihi tuondolee januari makamba. Hapo umekosea sana. Umemtoa waziri nishati na ceo tanesco watu wenye Phd za kiukweli na waadilifu. Umeweka wajanja wenye kujua kupiga hela ya umma. Huyo maharage tayari anaweka mazingira ya yeye na rafiki zake kuchota mishahara na marupurupu makubwa. Tusisahau magufuli alipoingia alifuta mishahara na malipo ya kinyojaji wakubwa kulipana mamilioni.
 
Uteuzi wa bodi ya Tanesco umeongea mengi kuhusu umakini, uwezo na mtazamo (kilichoujaza moyo)wa mteuaji. Zaidi ya yote unaweza kujua malengo na vipaumbele vya mteuaji kama kiongozi wa umna.
 
We tatizo lako nini?
 
Ndugu mbona una_panick sana? Ngoja nikwambie. Inalipa sana kuleta private sector experience kwenye public sector.
Private sector experience iwe kwa watu qualified. Sio marafiki wa January Makamba.

Maharage inabidi wamfundishe kazi, hajui chochote cha TANESCO. He is a dear in the headlight.
 


Anaweza kuwa amefanya kazi serikalini na tena ofisi ya Rais kabla ya haya unayo copy & paste na kuuliza hapa 🤣
 
Kama wewe sio mwenzao sahau hizi post za mashirika yenye ulaji.
Kama huna uhusiano wa karibu nao sahau. Unaweza ukajiuliza mbona mkurugenzi Fulani Ni boya na mwizi mbona hawamgusi?
Wanachoangalia kwanza Ni allegiency, utiifu, chama chako, Kama Ni muislamu lazima uwe BAKWATA , Kama Ni mkristo uwe wa dhehebu linaloeleweka,. Sio unasali kwa mzee wa upako au sijui maganga au misukule gani.
Age, education , experience , kabila, sexual orientation etc Ni secondary.
Jiulize kina Kibatala & co wako very smart, mbona kwenye teuzi huwaoni? Lkn ma miss ambao utaalamu wao Ni kusuka nywele wamo...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…