Kivp? Kwasbb sugu amesema kapigiwa simu. Una uhakika gani kama kweli kapigiwa.Dhahiri imeonekana sasa kuwa kumbe biashara ya uhamisho wa wanasiasa inasimamiwa na Katibu Mkuu mwenyewe kwa baraka za Raisi.
Wizi ni sayansi...bwashee pumzika tu...huwezi kulazimisha kupendwa bwasheeMbeya mjini na Iringa mjini wapiga kura wao wanajitambua ila mwaka huu maandalizi ya CCM yamekuwa ya kisayansi zaidi.
Ngoja October ifike tuwe mashuhuda!
Jibu la swali hili ni leo, tunasubiri kwa hamu...Wanabodi,
Namalizia kwa lile swali la msingi la uzi huu, Kauli ya "Maharage ya Mbeya Maji Mara Moja" Ina Ukweli?, Ni Kwenye Maharage tu au Hadi kwa Wanambeya?:
Je, October 28, 2020 Wana Mbeya WaTatulia, au kwa sababu wameisha zoea shida hadi wameota Sugu hivyo badala ya KuTulia, wao wataendelea za Sugu zao walizozoea?
Kauli Huumba!, Jibu la kama WanaMbeya ni kama Maharage ya Mbeya ya maji mara moja au au hapana ni October 28, 2020!.
Mbeya Oye!.
Paskal
Jibu lilipatikana, ni kweli kabisa, maharage ya Mbeya, maji mara moja!.Jibu la swali hili ni leo, tunasubiri kwa hamu...
P
Hata Wakili Mwabukusi ni mtu wa Mbeya, Pindi Chana kaonekana kupwaya hauwezi muziki wa Mwabukusi, sasa ameletewa Baba lao, Prof. Palamagamba Kabudi, amini nawaambieni mtamshuhudia jinsi Mwabukusi atakavyo lainika kama mkate mbele ya chai, mtamshuhudia Mwabukusi kama ni maharage ya Mbeya au la...!Wanabodi,
Kuna hoja kuwa kauli huwa zinaumba, sasa kuna hii kauli ya "Maharage ya Mbeya Maji Mara Moja", Jee kauli hii ina ukweli wowote kuwa ukipika maharerage ya sehemu nyingine zote, ili yaive lazima uongeze maji zaidi ya mara moja, lakini ukipika maharage ya Mbeya, ukiweka maji, ni mara moja tuu hadi yanaiva?.
Kama kauli hii ni kweli kwa maharage ya Mbeya, maji ni mara moja tuu, jee ni kwa maharage tuu au hata kwa wana Mbeya wenyewe yaani Wambeya, nao pia ni ukiwa na shida yoyote, maji ni mara moja tuu, wanatepeta, wanalainika, na kufikia maamuzi ya kukubali au kukataa jambo lolote, mara moja tuu, kirahisi rahisi, kiulani?.