"Maharage ya Mbeya maji mara moja" ni kauli ya kweli? Ni kwenye maharage tu au hadi kwa wanambeya? Kama kauli huumba, Jibu sahihi ni Oktoba 2020!

"Maharage ya Mbeya maji mara moja" ni kauli ya kweli? Ni kwenye maharage tu au hadi kwa wanambeya? Kama kauli huumba, Jibu sahihi ni Oktoba 2020!

Pasco my brother ulikumbwa na nini ulipoitwa kwa Ndugai siku ile manake uandishi wako unaanza kufanana na ule wa makanjanja kwamba unasema waliojitambua wakahamia ccm kwa hiyo kuhamia ccm ni kujitambua, mwaka huu hakuna uchaguzi kuna maigizo na kuharibu hela za walipa kodi tu there is no fair ground for uchaguzi si umewasikia wataiba mchakato kama walivyofanya kwenye serikali za mitaa
 
Wanabodi,
Namalizia kwa lile swali la msingi la uzi huu, Kauli ya "Maharage ya Mbeya Maji Mara Moja" Ina Ukweli?, Ni Kwenye Maharage tu au Hadi kwa Wanambeya?:

Je, October 28, 2020 Wana Mbeya WaTatulia, au kwa sababu wameisha zoea shida hadi wameota Sugu hivyo badala ya KuTulia, wao wataendelea za Sugu zao walizozoea?

Kauli Huumba!, Jibu la kama WanaMbeya ni kama Maharage ya Mbeya ya maji mara moja au au hapana ni October 28, 2020!.

Mbeya Oye!.

Paskal
Jibu la swali hili ni leo, tunasubiri kwa hamu...
P
 
Wanabodi,
Kuna hoja kuwa kauli huwa zinaumba, sasa kuna hii kauli ya "Maharage ya Mbeya Maji Mara Moja", Jee kauli hii ina ukweli wowote kuwa ukipika maharerage ya sehemu nyingine zote, ili yaive lazima uongeze maji zaidi ya mara moja, lakini ukipika maharage ya Mbeya, ukiweka maji, ni mara moja tuu hadi yanaiva?.

Kama kauli hii ni kweli kwa maharage ya Mbeya, maji ni mara moja tuu, jee ni kwa maharage tuu au hata kwa wana Mbeya wenyewe yaani Wambeya, nao pia ni ukiwa na shida yoyote, maji ni mara moja tuu, wanatepeta, wanalainika, na kufikia maamuzi ya kukubali au kukataa jambo lolote, mara moja tuu, kirahisi rahisi, kiulani?.
Hata Wakili Mwabukusi ni mtu wa Mbeya, Pindi Chana kaonekana kupwaya hauwezi muziki wa Mwabukusi, sasa ameletewa Baba lao, Prof. Palamagamba Kabudi, amini nawaambieni mtamshuhudia jinsi Mwabukusi atakavyo lainika kama mkate mbele ya chai, mtamshuhudia Mwabukusi kama ni maharage ya Mbeya au la...!
P
 
Back
Top Bottom