Billie
JF-Expert Member
- Aug 13, 2011
- 13,588
- 22,752
- Thread starter
- #21
Sasa kama ni shukrani ya kunilelea msichana wangu kwanini wasije kulipa na kwa wazazi wangu pia kama shukrani coz hata mimi nimelelewa kama yeye mi nafikili sio vizuri kuwepo mambo ya kupangiana mahari ibaki ni kama shukrani tu pale mtu anapoguswa na sio kupangiana viwango inakua kama nimenunua mke bwana.
Nafikiri mahari ni kama token of appreciation kwa kijana kwenda kwa wakwe zake kuwahsukuru kwa kumlea binti ambaye muda si mrefu anaenda kuwa mke wake. Kwa zamani ili kuwa ni maidadi ya kutosha ya ng'ombe na mbuzi na mpaka baadhi ya makabila ya kitanzani ilikuwa kuwa na mtoto wa kike ni "deal"!
Kwa siku za hivi karibuni mambo yamebadilika, mahari inachukua mfumo nilioulezea hapo juu, kama asante fulani kwa wazazi kumlea binti ambaye kijana anataka kumuoa. Kwa fikra zangu nafikiri haina kiwango maalum na haipaswi kuwa na kiwango maalumu, ila kiwe kiwango ambacho ni reasonable na siyo cha kukomoana na ambacho kijana anaweza kukilipa.
Ila wapo wazee wengine bado wana fikra za zamani na wanageuza suala la binti zao kuolewa ni kama mtaji kwao. Nafikiri kwa kesi kama hizo ni vyema wazee hao wakashauriwa na wazee wengine wenye uelewa mkubwa zaidi wa haya mambo.